* Wanafunzi kuandamana leo
Na Tumaini Makene
SAKATA la kashfa ya kampuni tata ya Dowans ambayo inatakiwa kulipwa sh. bilioni 94 jana lilitikisa katika mdahalo wa
wasomi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ambako lilielezwa kuwa ni 'sehemu ndogo ya familia kubwa ya ufisadi' unaoendelea nchini ambayo kama haitachukuliwa hatua stahili, itahatarisha amani na utulivu nchini.
Ilielezwa kuwa kashfa hiyo ni dalili ya tatizo kubwa katika sekta mbalimbali ikihusisha mikataba ya kilaghai, huku ikiathiri maendeleo ya nchi kisiasa na kiuchumi, kiasi ambacho viongozi wameshindwa kutumikia umma wa Watanzania, badala yake wanatumikia maslahi binafsi.
Kashfa zingine zilizotajwa kukuhusishwa katika hicho kinachoitwa 'familia ya ufisadi' zilikuwa ni pamoja na ununuzi wa rada, mikataba ya IPTL, ubinafsishaji wa mali za umma, matatizo ya ardhi ambapo wawekezaji wamekuwa na sauti kubwa kuliko wananchi wa maeneo husika, ukitajawa mgogoro wa wakulima na wawekezaji huko Babati.
Hayo yalisemwa jana katika mdahalo juu ya sakata la Dowans,
ulioitishwa na Chama cha Wanataaluma UDSM (UDASA), ambapo pia ilitolewa njia mbadala ya kutatua matatizo
kama ya Dowans kwa kutaifisha mali za wahusika.
Akiwasilisha maada yake juu ya sakata la Dowans katika mlengo wa Sayansi ya Siasa, Bw. Bashiru Ally ambaye pia ni mhadhiri wa idara hiyo UDSM, alisema kuwa kashfa hiyo ni sehemu ya familia kubwa ya ufisadi inayoendelea kuitafuna nchi katika nyanja ya uchumi na siasa, kiasi cha kupandisha hasira za makundi mbalimbali ya watu katika jamii.
Kwa upande wake, Dkt. Adolf Mkenda aliwasilisha mada yake kwa mlengo wa uchumi, alisema kuwa soko huria haliwezi kuwa sababu ya kulaumiwa pale kashfa kama hizo zinazonuka makosa ya jinai kama rushwa, zinapotokea, bali hiyo ni dalili ya watumishi wa umma wakishirikiana na wale wa sekta binafsi kujinufaisha wao.
Akiwasilisha mada yake kwa mlengo wa kisheria, kwa kutoa historia ya Dowans, kuanzia Richmond, mpaka hukumu ya kesi ya ICC, Bw. Jesse James kutoka Shule Kuu ya Sheria Chuo Kikuu Dar es Salaam, alisema kuwa mkataba ulioifikisha nchi katika sakata la Dowans hauna tofauti na ile iliyokuwa ikisainiwa na machifu wajinga, wakati wa enzi za kuingia
ukoloni (Chifu Mangungo wa Msovero).
Kwa upande wake, mwanasheria na mwanaharakati Bw. Tundu Lissu alisema kuwa wanasheria waliowakilisha upande wa serikali wakati wa uendeshaji kesi, hawakuzungumza dalili za uwepo wa rushwa katika sakata zima la Dowans, kuanzia katika Kampuni ya Richimond, suala ambalo lingeweza
kusababisha ICC isisikilize kesi hiyo, kwa mujibu wa mikataba ya kimataifa.
Wakati huo huo Majira limepata habari ya kuwepo kwa maandalizi ya maandamano ya amani ya wanafunzi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam ambapo moja ya hoja zitakuwa ni kudai ongezeko la fedha za kujikimu kutoka sh. 5,000 ya sasa mpaka sh. 10,000.
Habari kutoka vyanzo mbalimbali zilisema kuwa hoja nyingine ambayo imewasukuma kuandaa maandamano hayo ni kupinga tamko la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) la kutaka kuvunjwa kwa Uongozi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kwa madai kuwa umeshindwa kuwahudumia wanafunzi inavyotakiwa.
Alisema kuwa tatizo la mikopo na migomo ya wanafunzi vyuo vikuu ni mfumo wa uanzishwaji wa bodi yenyewe unaotokana na serikali kushindwa kusimamia na kuiwezesha vya kutosha pamoja na uzembe wa uongozi wa baadhi ya vyuo na Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU), hasa katika kuwasilisha taarifa za wanafunzi mapema.
hii inasikitisha ni jinsi gani walimu wazima na akili zao kujiingiza kwenye siasa kinacho sikitisha tanzania kunachuo kikuu kimoja?sijawahi sikia mwanasiasa huyu kaenda chuo kingine zaidi ya chuo hicho ambacho watoto wa mjini wengi husema chuo cha washamba kutokana kuwa wanafunzi wengi wachuo hicho hutoka mikoana na watoto wengi wa mjini husoma ulaya na vyuo vikuu vya binafsi nia ajabu sana
ReplyDeleteWe anony, kuhoji habari ya madudu yanayoendelea ni jukumu la kila msomi aliyesoma akaelimika! UD imetangulia na inaonyesha ukongwe wake. pia ina mkusanyiko wa kitaaluma wa watu wafani mbali mbali ambazo zinaguswa moja kwa moja na mambo yanayoendelea. habari ndiyo hiyo inaendelea na vyuo vingine tunatrot saa yoyote tunaanza kuingiza timu!
ReplyDeleteHivi wewe Anony wa 10.00 ungependa kuona suala la Dowans linazungumzwa na nani?Na kuhusu hoja yako muflis kuhusu "ushamba" na "utoto wa mjini",si bora hao waliotoka mikoani kuja kusaka elimu kuliko wewe unayehangaika hata katika jambo dogo tu la kupangilia sentensi.Hebu rejea tena kusoma ulichoandika,kisha jiulize "mshamba nani hapo"?
ReplyDeleteUDSM ndio baba lao
ReplyDeletenikweli kabisa, mchangiaji wa kwanza nakubali hoja yake....mbona udom hawaendi? mbona sua hawapo? mbona st augustine hamna. wewe ndo hujui kuchanganua mambo. jua kutofautisha taasisi ya elimu inayofundisha course za siasa na Taasisi ya Elimu inayoshabikia siasa. umenisoma? ahhhh.... udsm imekosa sifa..... na kusema ukweli students from udsm ni washamba, hata wenyewe wanajilitambua hilo. kwa hiyo usikatae best..
ReplyDeletemambo yote yako OPENUNIVERSITY, VYUO VINGINE VIMEPITWA NA WAKATI.
ReplyDeleteNimeupenda saaana mwangaza uliotolewa na gazeti la East African kuhusu DOWANS kupitia mtandao na kuwekwa bayana na mchangiaji. Sasa KIKWETE unasubiri nini kukiri maana nafahamu kuwa unajua ukweli huu utakuumbua siku chache za usoni??? Mjinga Salva Rweyemamu (Msemaji wa Ikulu)pinga ukweli huo basi kama ulivyoainishwa hapo maana umezoea kukanusha in favour of the damn President. PCCB mko wapi kwa sasa?? Kanusheni ukweli huo tuwaone kama nyie ni wajanja!!! You are really stupid!! Yaani kamati ya Mwakyembe ilithibitisha kampuni kuwa hewa kwa kutumia millioni za watanzania bure?? Mwakyembe ulitusaidia, lakini sasa utaumbuka!! (Kumbuka yale uliyoyaficha ili kutokuiathiri serikali ......). Sasa yanaanza kubainika moja baada ya jingine. Je, Una/ Uliiheshimu taaluma yako lakini??? Mnawazidishia watanzania hasira tu ya kuwatoa madarakani kwa nguvu. Tunisia, Misri, Jordan na Yemen ni nchi na si visiwa. Wanaumia sasa. Tanzania haiwezi kukwepa kikombe hiki. Moto umeanza sasa Africa!!! Rostam, siku zako zinahesabika duniani. Utakufa kifo cha ajabu sana FISI WEEE!! Maana huna haya. Halafu unasikitisha kwa jambo moja; Huwa hukumbuki maneno unayoyasema. Maana unatuambia kuwa wewe unafanikisha kuwaleta wawekezaji!! Kashfa lukuki!! Sasa kanusha hili ambalo liko katika mtandao dunia nzima. Shame on you!!! Nasema hiviiiiii Kikwete na serikali yako, mnamuogopa Rostam kwanini; anawalala??? au?? Kumbuka kisa cha Nyerere na yule Mgiriki aliyejinadi kuwa nchi yote aliiweka mfukoni mwake. Siku si nyingi, Mtakiona cha mtema kuni. Nyambafuuuuu!!!
ReplyDelete