Na Stella Aron
WAZIRI wa Maji, Prof. Mark Mwandosya amezawadiwa visima 100 na mfanyabiashara maarufu wa jijini Dar es Salaam Bw. Mustafa Sabodo kwa
ajili ya kupunguza kero ya maji mkoani Mbeya.
Prof. Mwandosya alitunukiwa zawadi hiyo mara baada ya jana kufika nyumbani kwa mfanyabiashara huyo kumshukuru kwa niaba ya ya serikali kwa ajili ya msaada wa visima 600 vyenye thamani ya sh. bilioni 1.8 kwa wananchi wanaoishi vijijini isipokuwa Mkoa wa Dar es Salaam.
Waziri huyo alimshukuru mfanyabiashara huyo kwa kuona kero inayowakabili wananchi katika maeneo mengi ya nchi.
Prof. Mwandosya alisema kuwa kutokana na msaada huo serikali itashirikiana na mfanyabiashara huyo kupitia kamati yake aliyounda kwa ajili ya kufanikisha ujenzi wa visima hivyo.
Alisema kuwa serikali itakuwa tayari kutoa maelekezo ya kitaalamu katika maeneo yanayostahili kuchimbwa visima vya maji pamoja na ushauri mbalimbali.
"Tunakushuruku kwa msaada wako kwa kuwa hili si jukumu la serikali peke yake bali ni mpango shirikishi ambao utafanikisha kupunguza kero ya maji nchini hivyo nasi tutakuwa tayari kushirikiana na kamati hiyo ili kutekeleza azma hiyo, " alisema.
Kutokana na shukrani hizo mfanyabiashara huyo aliaongeza idadi ya visima 100 kwa serikali kutambua mchango wake.
"Umekuja kwa ajili ya kutoa shukrani kwa kutambua mchango wangu hivyo kutokana na ujio huo sasa naongeza visima vingine 100 na kuwa visima 700 ambavyo vitachimbwa katika maeneo mbalimbali nchini isipokuwa Dar es Salaam, " alisema Bw. Sabodo.
Katika hotuba yake, Sabodo aliitaka serikali isiingilie matumizi visima hivyo vyenye lengo la kuwasaidia wananchi kupata huduma za maji bila masharti.
Alisema ni jambo la ajabu kwa viongozi wanaotuhumiwa kwa ufisadi, kuendelea kuhodhi fedha nyingi na kushindwa kuisaidia jamii inayowazunguka.
"Visima hivyo ninavyosaidia katika wilaya hizo sitapenda serikali iingilie kwa chochote kwa kuwa matengenezo madogo madogo yatafanywa na wananchi wenyewe. Hakuna yeyote atakayelipia katika kutumia visima hivyo," alisema.
prof. mwandosya hongera kwa kupewa visima 100 kwa ajili ya mkoa wa mbeya. lakini tunaomba sana visima hivyo usivijaze wilaya ya Rungwe kwenye jimbo lako tu na hii imejionyesha muda mrefu umekuwa na tabia ya kupeleka vitu vingi Rungwe bila kujali kuwa wewe ni kiongozi wa kitaifa. hebu angalia miradi ya maji Rungwe umepeleka miradi ya bilioni 16 KATIKA KIPINDI CHA 2009/10, wakati kyela ambayo ni jirani kabisa haina maji na hujapeleka hata mradi mmoja! hivi wananchi hawa kyela ambao wamekuwa wakikuunga mkono mbona unawatenga? huo ni uchoyo Prof. ninakuheshimu sana lakini imebidi niseme. Mwalimu JK Nyerere amekufa huku Butiama ikiwa haina lami unafikiri alikuwa hapendi? kuweka au kupeleka vitu vingi wilayani kwako bila kuzingatia uwiano ukitumia nafasi yako ya uwaziri ni ufisadi.
ReplyDeleteMmh! Tumefikia hapa? Yaani mtu binafsi anakwenda kushukuriwa na Serikali nzima kwa ajili ya kutoa huduma! Yaani serikali imeshindwa kutoa huduma hiyo mpaka kuomba kupitia bakuli la ndani! La nje limeshindwa kazi!
ReplyDeleteLeo hii mtu wa kawaida kabisa anakuwa na moyo wa kusaidia watanzania wenziwe bila masharti?! Serikali imeshindwa!! Mmmmmh! Haya Sabodo nashukuru sana umepunguza tatizo kubwa la maji ila sasa nakuomba uangalie mikoa ya kusini hakuna hata maji ya visima! Watu wanapata taabu sana na maji ya kunywa huu mwaka wa 50 tangu uhuru!
Nakushauri Mzee Sabodo miradi hii ili iwe endelevu ni budi wananchi pia wachangie kama si hela basi hata nguvu zao, tusitowe bure tu, kwani miradi itakufa pindi Sabodo atakapoondoa ufadhili wake! Hali kama hii imeshajitokeza hapo awali enzi za Mwalimu Nyerere na hasara zake tumeziona.
Nia ni njema akini sasa Ushiriki wa wananchi katika kila hatua ya Mradi ni muhimu sana!
Tunaomba watanzania wachache wenye moyo kama Sabodo mjitokeze kusaidia watanzania wenzenu, hali ni mbaya sana huko vijijini! Si maji, barabara, umeme, fursa za elimu nk! Bado ni tatizo.
Tuendelee kujitolea hivi, maana kwa sasa hakuna jinsi.