Na Mwandishi Wetu
RAIS Jakaya Kikwete amesema bado kuna hisia na madai ya uadilifu mdogo wa baadhi ya watoa haki katika mfumo wa mahakama na kuwa
wasiokuwa na uwezo wa kifedha ni vigumu kupata haki.
Kutokana na hali hiyo, Rais Kikwete amezitaka mahakama zote nchini kufanya mabadiliko kwa kuwa uwezo wa kuondoa hisia na imani hiyo uko mikononi mwao.
Akizungumza katika sherehe ya maadhimisho ya siku ya sheria nchini alisema mahakama ziongeze bidii katika utendaji wake na kwa kuzingatia hayo, itasaidia kuboresha taswira ya mahakama kwa wananchi.
"Natambua si majaji au mahakimu wote ambao uadilifu wao unatiliwa shaka. Natambua pia kwamba mnafanya juhudi kubwa za kupambana na wale wasiokuwa waadilifu miongoni mwenu. Nafahamu kuwa wapo waliokwisha wajibishwa kwa ajili hiyo. Nawaomba muongeze bidii na maarifa katika mapambano haya.
"Kama hapana budi kubuni maarifa mapya mfanye haya, mafanikio yenu katika mapambano hayo, yataboresha sana taswira ya mahakama yetu mbele ya umma wa Watanzania. Ni sifa na heshima kubwa kwetu sote," alisema Rais Kikwete.
Aliongeza kuwa kwa yale yote aliyohaidi kuyatekeleza ili kuboresha utendaji wa kazi za mahakama atayatekekeleza na mengine ameshaanza kuyatekeleza.
Naye Jaji Mkuu Othman Chande alisema atahakikisha mahakama zinaongeza kasi ya usikilizaji wa kesi kwa wakati kwa kubadilisha utaratibu uliokuwa ukitumika awali ambao umeshapitwa na wakati.
Pia alisema uelewa wa wananchi kuhusu sheria bado ni mdogo na ni kitendawili ambacho hakijulikani kitateguliwa lini, hivyo jitihada katika utoaji wa elimu zinahitajika.
Alisema kutokana na hali hiyo mahakama ina jukumu zito la kuhakikisha kuwa kila mwananchi anakuwa na uelewa kuhusu sheria ili aweze kutetea haki yake ya msingi anapofika mahakamani.
Jaji Chande alisema kwa kuzingatia umuhimu wa elimu kwa wananchi kuhusu sheria, mahakama ilishatoa vijarida vinavyoelezea haki za msingi za kila mwananchi, pia mwaka jana walizindua tovuti ambayo itawasaidia kuielewa sheria vizuri.
"Dira ya mahakama ni kuhakikisha inatoa maamuzi ya haki kwa wateja wake lakini kama uelewa wa wananchi utaendelea kuwa mdogo mahakama itakuwa kwenye wakati mgumu," alisema.
Jaji Chande alisema katika kuhakikisha mahakama zinapunguza adha kwa wananchi, atahakikisha wanashirikiana bega kwa bega na wahisani wao wanaochangia wawazo kwenye maboresho katika sekta ya sheria.
Hata hivyo, alisema mahakama zinakabiliwa na changamoto katika utendaji wake wa kazi hivyo kusababisha kesi kurundikana mahakamani.
Mkuu haitoshi kusema tuu,hayo ni mambo ya jukwaa la siasa,mahakamani kunahitaji nguvu ya ziada ili kupaweka sawa,masikini hapati haki hapo,hukumu zinategemea wadhifa wa mtu,sio lazima uwe mkubwa serikalini tu,hata uwe kwenye chama kikubwa cha siasa au uwe na fedha,kesi kama hapo mahakama ya Kisutu zinaendeshwa na makarani na mawakili na si mahakimu,wao kazi yao mwisho ni kupokea rushwa na kutoa hukumu mbovu,tatizo hata ukilalamika kunakohusika husikii hakimu kufukuzwa kazi au karani wake.uwajibikaji ni mdogo sana nchini kwetu watu wanapenda blablaa za siasa tu
ReplyDeleteWatwambie zile kesi za EPA zilitolewa hukumu sitahiki? je kesi ya chenge kuuwa je ile hukumu ni ya haki? hukumu ya zombe aliyoshiriki kuuwa waziwazi kwa kutoa amri iliisha vipi? Mahakama za tanzania ni usanii mtupu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!NGOJA TUTAONA KESI ZA UCHAGUZI AMBAO CCM IMEJITANGAZA WAKATI IMESHINDWA UTAONA MADUDU YA MAHAKAMA MUDA SI MREFU KWANI FORM ZA MATOKEO ZINAONYESHA CHADEMA AMESHINDA LAKINI MATOKEO YANAGEUZWA MDOMONI KAMA KULE SHINYANGA,KARAGWE,KIGOMA MJINI NA UKONGA KWA MPENDAZOE NK.....ILA IPO SIKU MTASITAFU NA NYIE MTANYONGWA NA KAMBA HIYOHYO KAMA SI WEWE NI MTOTO WAKO TENDENI HAKIII!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
ReplyDeleteKwa kweli utendaji wa mahakama zetu Tanzania unakatisha tamaa kabisa. Wakati mwingine naamini huenda Tanzania hatihitaji mahakama hata kidogo. Tazama kesi za akina Costa Mahalu, Mramba, EPA, DECI, n.k. hizi zote zilianza zamani sana ukilinganisha na kesi kama ya Madoff kule USA. Madoff kesi ilikwisha siku nyingi na kufungwa. Prof. Costa Mahalu yupo tu mtaani.
ReplyDeleteMahakama Tanzania ni kwa ajili ya wanyonge tu. wao ndiyo wanofungwa pingu wanapopelekwa mahakamani. Wanaoiba peasa nyingi kama Mahalu, EPA, Mramba n.k. wanakwenda wakijidai. Kwa nini?
Atuambia ni Wizara ipi yenye uadilifu: polisi? afya? elimu? kilimo? mali asili? nishati na madini? TRA? TAKUKURU? Tume ya Uchaguzi? Bandari? Ardhi? Ote ote bofu!
ReplyDelete