07 January 2011

Serikali yasalimu amri kwa CHADEMA

*Yakubali kutatua mgogoro kwa mazungumzo

Na Reuben Kagaruki
SIKU mbili baada ya kutokea vurugu zilizosababisha watu wawili kuuawa na polisi kwa risasi, sita kujeruhiwa huku viongozi wa kitaifa na wabunge wa CHADEMA wakikamatwa, serikali imesalimu amri na kutangaza kushughulikia mgogoro wa
Arusha kisiasa ili kuupatia ufumbuzi.

Uamuzi huo ulitangazwa Dar es Salaam jana na Waziri wa Mambo ya Ndani, Bw. Shamsi Vua Nahodha, alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu vurugu zilitokea mkoani Arusha juzi zikihusisha polisi waliokuwa wakidhibiti wafuasi wa CHADEMA waliodaiwa kuandamana kupinga uchaguzi wa meya, uliofanyika bila kufuata taratibu.

"Serikali imedhamiria kukutanisha wanasiasa wa pande husika (CCM na CHADEMA) ili kuupatia ufumbuzi mgogoro wa Arusha, kwa kuwa wakati wa pande mbili kuridhiana umewadia," alisema Bw. Nahodha.

Alipoulizwa serikali ilikuwa wapi kushughulikia mgogoro huo hadi isubiri damu imwagike, Bw. Nahodha alisema hiyo ilitokana na kuwapo kwa nadharia na taaluma za aina tatu za kusuluhisha migogoro.

Alisema kabla migogoro haijatatuliwa ni lazima wahusika wakuu waamini kuwa kuna mgogoro.

"Pia kabla ya kutatua mgogoro huo ni lazima upate watu wanaokubalika kuutatua," alisema na kuongeza kuwa kigezo cha tatu ni kujua ni watu gani wanahusika.

"Kwa sasa naamini kuwa wahusika wakuu wanaamini hapa (Arusha) kuna tatizo," alisema, Bw. Nahodha.

Hata hivyo alisema jitihada za siri zimekuwa zikifanyika kusuluhisha mgogoro huo, lakini hazikutoa matokeo yaliyotarajiwa na sasa kilichobaki ni kuutafutia ufumbuzi kwa uwazi.

Alipoulizwa na waandishi wa habari ni lini suluhu hiyo itapatikana, Bw. Nahodha alijibu;

"Nadharia ya kusuluhisha migogoro ni lazima wasiwepo watu ambao wana haraka, ni vigumu kusema usuluhishi utatumia muda gani, sana sana itategemea weledi wa wale wasuluhishi na wahusika."

Alipoulizwa ni kwa jinsi gani wananchi watamwamini yeye, hasa kwa kuzingatia tukio la mauaji ya juzi mkoani Arusha ni la pili kutokea kwake akishikilia nafasi nyeti serikalini, baada ya lile ya Januari 21, 2001 akiwa Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, ambapo wafuasi 21 wa CUF waliuawa; Bw. Nahodha alijibu;

"Mbona unihukumu kuwa mimi nimechangia maridhiano ya kikatiba Zanzibar iliyounda Serikali ya Kitaifa ambayo waandishi wa habari mnasifia?

"Mbona hamnisifii kwa mema? Hivyo ndivyo maisha yalivyo, ndiyo maana kuna wakati bahari inachafuka na kutulia."

Alisema Tanzania ni nchi yetu wote, hivyo tuna wajibu wa kuilinda amani iliyopo.

Akieleza kiini cha vurugu za juzi, Bw. Nahodha alisema  viongozi wa CHADEMA hawakufuata ushauri wa polisi wa kuwataka kufanya mkutano peke yake na kuacha maandamano.

Alisema polisi walizuia maandamano hayo baada ya kubaini hayatakuwa na mwisho mwema. "Viongozi wa CHADEMA hawakufuata ushauri wa polisi na badala yake waliendelea na dhamira ya kuandamana," alisema na kuongeza kuwa baada ya wafuasi na viongozi wa CHADEMA kuandamana polisi walilazimika kuwatawanya.

Alisema baadhi ya viongozi wa chama hicho ambao hawakukamatwa, walikimbilia kwenye mkutano ulioendelea vizuri, lakini baada ya kumalizika waliamuru wafuasi wao waende polisi kuwatoa wenzao waliokamatwa.

Bw. Nahodha alisema ili kuepusha shari baada ya kuona magari yakipigwa mawe, nyumba na vibanda kuchomwa moto, polisi walilazimika kuepusha shari.

Alisema katika vurugu hizo watu wawili waliuawa, na wengine sita kujeruhiwa. Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Said Mwema alithibitisha watu hao kuuawa kwa kupigwa risasi na polisi.

Bw. Mwema alisema wakati wa kushughulikia tukio hilo watafuata utaratibu wa kisheria na iwapo wao (Jeshi la Polisi) wakishitakiwa wataenda kujitetea. Bw. Mwema alielezea kusikitishwa na vifo vya watu hao.

"Hata akifa mtu mmoja au kuumia ninasikitika, hatuna sababu ya kuficha idadi ya waliokufa...sisi hatupendi mtu afe au kujeruhiwa," alisema wakati akijibu swali kuhusu tetesi kwamba waliokufa katika tukio hilo ni 10.

Alipouzwa madai kuwa hivi sasa anatumika kisiasa, Bw. Mwema alijibu; " Natumika kwa mujibu wa sheria, sheria hizo hizo ndizo zinatumika kutuhukumu."

Kauli hiyo ya IGP iliungwa na Bw. Nahodha ambapo alisisitiza kwamba hajaona kama, Bw. Mwema anatumika kisiasa. "Kama anatumika kwa namna fulani kusaidia chama fulani hilo sijaliona," alisema Bw. Nahodha.

Bw. Mwema alipoulizwa sababu za kuongeza askari mkoani Arusha kutoka Chuo cha Polisi Moshi, Ukonga Dar es Salaam na Manyara, alikanusha askari wa Ukonga kupelekwa Arusha.

"Hakuna askari waliotoka Ukonga, lakini kuweka askari wa akiba kwa ajili ya kukabili yaliyotokea, sio kosa," alisema.

Katika hatua nyingine, wananchi mbalimbali wamelaani kitendo hicho, akiwamo Mhadhiri Msaidizi wa chuo cha Diplomasia jijini Dar es Salaam, Bw. Abdallah Majura aliyesema Jeshi la Polisi limeirudisha Tanzania hatua kadhaa nyuma kwa kutumia nguvu nyingi badala ya kuacha mgogoro wa uongozi wa Arusha kutatuliwa kwa mazungumzo.

Mhadhiri huyo alisema Tanzania imeshapiga hatua ndefu mbele kwa kusaidia kutatua migogoro mikubwa nje ya nchi, lakini kitendo hicho kimemsikitisha kwa serikali kushindwa kutatua mgogoro huo mdogo wa ndani.

"Ninakilaani kabisa kitendo hiki, polisi wanatakiwa kupewa elimu maalumu katika kutatua migogoro na kilinda haki za binadamu. Napendekeza turudi chini katika mazungumzo na ikiwezekana uchaguzi uliozua mgogoro ufanyike upya," alisema Bw. Majura.

Naye Catherine Malila alipiga simu cha habari na kulaani hatua hiyo ya polisi, akisema bunduki hazikuwa zinastahili kutumika kwa watu wanaopigania haki ya kidemokrasia, na kama ni muhimu zingetumike kwa mafisadi wanaofilisi uchumi wa nchi.

35 comments:

  1. WANAOTAKIWA KUSHTAKIWA HAPA NI POLISI WALIOWARUSHIA RAIA RISASI HADHARANI KAMA MAJAMBAZI. KITENDO CHA KUWAPIGA RISASI RAIA WAKIWA WANAANDAMANA NI KINYUME CHA SHERIA ZA NCHI KWANI KOSA LA KUANDAMANA ADHABU YAKE SI KIFO.POLISI WOTE WALIOWARUSHIA RAIA RISASI WALIPASHWA WAPANDISHWE KIZIMBANI KWA KUTUMIA EXCESSIVE FORCES KINYUME CHA SHERIA ZA NCHI.
    MIMI KM MWANASHERIA NILITEGEMEA CHADEMA WANGEWAFUNGULIA POLISI HAWA KESI ZA MAUAJI THE NEXT DAY KWANI NI KINYUME NA HAKI ZA BINADAMU NA PIA NI KINYUME CHA SHERIA ZA NCHI KUWAPIGA RISASI RAIA ETI KWA KOSA KUANDAMANA.KIKWETE ANA HASIRA ZA WATU KUMKATAA KWENYE UCHAGUZI ULIOPITA KUTOKA USHINDI WAKE WA ASILIMIA 84 MPAKA 60 KWAHIYO ANAJARIBU KUTUMIA MABAVU KUWATAWALA WATANZANIA WA ARUSHA WALIOMKATAA KWA USANII KAMA MUGABE WA ZIMBABWE BAHATI MBAYA WATANZANIA HATUTAMRUHUSU KUFANYA HIVYO KWANI KUANZIA SASA TUTAANZA KUKUSANYA MIKANDA YOTE YA MASHAMBULIZI YAKE ANAYOYAFANYA DHIDI YA RAIA TAYARI ANA DAMU MIKONONI MWAKE KWAHIYO BADO ATAENDELEA NA OPERATION YAKE YA KUUWA RAIA ILI KUMFIKISHA KWENYE MAHAKAMA ZA KIMATAIFA.

    ReplyDelete
  2. huyo Mwema hana ufahamu wowote yeye hawezi sema anaumia kuona mtu anaumia.Police wa tanzania ni aibu bora vibaka kuliko police si lolote ni wendawazimu wasio jua wanafanyanini.Na huyo kikwete mtu wa visasi tuuuu.Na raisi mchovu kuliko wote waliotangulia hana maana wala nini.na sidhani akija marekani atatamani kukutana na Oboma tena .mjinga alikuja huku anajifanya kondoo kumbe mgaidi tu.Police nimakosa kumshambulia mtu asiyefanya vulugu.

    ReplyDelete
  3. Mh.Nahodha, ninakupongeza kwa kauli yako nzuri yenye faraja.Lakini ninaomba ukae na Mh.Makamba umfunde awe na kauli nzuri aache kauli za kihuni wakati yeye ni Mzee na heshima zake.Na istoshe ni Katibu mkuu wa CCM kitaifa.
    Mh.Nahodha ninaomba ufunde Afande Mwema aache kutumiwa na CCM afuate Job discription zake zinavyo muongoza.

    ReplyDelete
  4. Ama kweli kuna watu na watu. Hivi hawa watu wanaomtaka IGP Mwema na Waziri Nahodha wajiuzulu kutokana na fujo za huko Arusha zilizosababisha vifo vya watu WAWILI TU wanasema kutoka moyoni au mchezo wa siasa tu?
    Sikusikia kelele kama hizi za kumtaka IGP Mahita kujiuzulu pale wazanzibari ZAIDI YA ISHIRINI walipopigwa risasi na polisi kule Pemba kwenye maandamano kama hayo

    Hivi wa Pemba si watu au uraia wao ni daraja la pili? IGP Mwema na Nahodha msijiuzulu. Mliofanya ni tone kwenye bahari ya waliofanya wenzenu na hakuchukuliwa hatua yoyote.

    ReplyDelete
  5. Polisisiem na Usalamapinduzi wa Taifa ndio wanavunja amani ya nchi hii.

    ReplyDelete
  6. Huyu waziri na Mwema nadhani mpaka sasa hawajatambua kwamba watanzania kadhaa wameuliwa kwa kupigwa risasi na polisi. Hiyo ni jinai. Ni kitendo ambacho maneno matamu hayatafuta. Nani alitoa amri ya kutumia risasi? Waaandishi wa habario hawakuuliza swali hilo. Nani alitoa amri ya kutumia risasi dhidi ya wanatanzania waliokuwa wakiandamana na kupeleak maafa na majeruhi ? Kama ni Kikwete, au huyo Waziri au Mwema - wanapaswa kufunguliwa mashtaka ya jinai. Hakuna lingine.

    ReplyDelete
  7. Bwana Nahodha - the police using live bullets shot dead innocent demonstrators and at the same time caused widespread mayhem including serious injuries. Someone has to be accountable for these crimes. Who gave the orders to use live bullets. Who, we ask ? This is a serious matter. That the people demonstrated is not an excuse to shoot them. The dead should not have died in vain; justice must be seen to be done.

    ReplyDelete
  8. Maridhiano sawa lakini baada ya maridhiano wale wanaohusika na mauaji ya raia wasio na hatia wapelekwe kwa Bw. O Campo kule The Hague, na tuanze na Benjamin kwa mauaji ya makumi ya watu kule Pemba mwaka 2001

    ReplyDelete
  9. Watu wa Pemba waliopigwa risasi ilikuwa jinai. Na inafaa jinai hiyo na nyingine huko Zanzibar zifuatiliwe na mashtaka kufunguliwa. Haikuwa haki.Hoja kwamba kwa kuwa hayo yalijiri Unguja basi tufumbe macho kuhusu Arusha ni udhalimu wa kijinga. Mnasema kuwa wale watu waliouliwa Arusha ndiyo waliowauwa watu huko Pemba na kwingineko. Wote ni victims. Hatua kaliya kisheria isipochukuliwa dhidi ya serikali kuhusu maafa ya Arusha basi ngoma itakuwa ile ile iliyoanzia, pengine, Pemba. Mhalifu ni mhalifu, yeye si mjumbe au mwakilishi wa eneo lolote.

    ReplyDelete
  10. Nahodha ulikuwa wapi kujua kama kuna tatizo Arusha au ulikuwa nje ya nchi ndo umekuja jana hufai wewe,Mwema na polisi wake wajinga waliofeli wakapata zero ndo wameona kuwa Police ndo kila kitu ni mambumbumbu wa sheria na wasiojua kusoma na kutafsiri vifungu vya sheria ni ibara gani na kifungu kipi ambacho kinasema polisi wana haki ya kutoa vibali vya mikutano kama si ujinga wao wajue wajibu wao ni kulinda raia na mali zao si kuzuia mikutano Mwema elewa baba liishia darasa la ngapi wewe yaani unazidiwa busara na kamanda Polisi aliye isoma katiba na akaruhusu maandamano,hivi sasa nyie mnalinda viongozi na mali zao,hufai bora hata Mahita.

    ReplyDelete
  11. Makamba umeamkaje hadi kuanza kutumia Biblia?au una taka viongozi wa dini nao waongee kwa kutumia biblia mtaanza kusema kuna udini,au wewe unaona uchaguzi wa mayor Arusha ulikuwa sahihi kwa wewe tunafahamu ulichofukuziwa ualimu wako hata communication skills hujui una kauli mbovu kama mwendawazimu nenda kasuluhishe basi kule Arusha na si porojo CCM(Chama Cha Majambazi) kinawafia mtake msitake mwisho wenu umewadia.

    ReplyDelete
  12. Huko kwa Ocampo na Slaa apelekwe,kuna mali za watu na roho za watu zimeteketea.

    ReplyDelete
  13. wananchi msiwe na hasira na police, tulaumu tulikojikwaa sio tulikoangukia. police ni watanzania kama sisi,ni wadogo, wapwa na binamu zetu, huwa tunahenya nao na familia zao katika huduma mbovu mbalimbali zinazotolewa na serikali ya CCM. Walichokifanya police kupiga watu risasi sio kwa matakakwa yao wenyewe, kwani nature ya kazi ya askali yoyote ni kupokea na kutekeleza amri kwanza na kuhoji baadaye. kuna chain of command inayoanzia kwa wanasiasa (CCM)kwenda kwa amiri jeshi mkuu (mwenyekiti wa CCM taifa)kupitia Waziri wa mambo ya ndani kwenda kwa IGP Mwema kwenda kwa kamanda wa police mkoa wa Arusha kwenda kwa makamanda mbalimbali wa mkoa na wilaya kwenda kwa vijana (police) ambao wanatekeleza amri ya kuchapa na kuua. hivyo wa kulaumiwa hapa sio police ila CCM. maana kama A=B na B=C basi A=C. Ukiangalia chanzo cha mgogoro wenyewe ni uchaguzi wa Meya wa jiji la Arusha ambao CCM ilishauchakachua kama kawaida yake. Hata zile taarifa za kiintejensia alizodau IGP huwenda zilitolewa na makada wa CCM nani anajua? Si wangeacha maandamano yafanyike na kumpiga risasi yule tu anayefanya vurugu wakati wa maandamano?

    ReplyDelete
  14. Wewe (mwandishi)Kagaruki haufahamiki. Umeona wapi serikali kusalimu amri? Mbona unapandikiza chuki baina ya serikali na raia wake. Umesomea wapi wewe. Rekebisha articles zako na uwache tabia na ukereketwa wa kipuuzi!

    ReplyDelete
  15. CCM, Kikwete and his government will pay for every drop of innocent blood spilled in this fracas. There was no reason to prohibit the demonstration and after all who gave the police to act against the very constitution they swore to safeguard? The constitution says of freedom to meet, demonstrate and express views while the police who have of recently demonstrated to be CCM bootlickers act the opposite.
    Shame to Kikwete and his government! we want an independent inquiry on what transpired at Arusha. It is disgusting and in fact a great shame to see Mr Mwema the IGP defending this ruthless act by his Police. In the culture of good governance The Minister of Home Affairs, IGP, and Arusha RPC could have resigned to pave way for an independent inquiry but not here in Tanzania. Where is the good governance trumpeted several times by Mr Kikwete? The International Court of Justice should take action on all involved.

    ReplyDelete
  16. Tanzanians, this a day of mourning, a day of shame. Our fellow citizens have been cut down by the ruthless CCM machine.The killers are not even remorseful. As I write, nobody has been charged for murdering or severely injuring our people for ostensibly demonstrating. When did peaceful protest become an act deserving of capitol punishment.We are indeed living in very dangerous times.And,to make it worse, the CCM leadership is going about its business -smiling- as if nothing serious has happened! I hope and expect men and women of moral substance will resign from the CCM cabinet imediately otherwise they will be complicit of the Arusha massacre and blood-letting. Pinda ,Tabaijuka - where are you. Those who are supporting the CCM action should be ashamed ;in fact I don't have time for them because they are exhibiting sub-human tendencies. Ewe Mola tulinde kutoka katika shari ya wakatili, nyamaume na mijitu isiokuwa na mipaka katika maisha. Amin,Amin ,Amin.

    ReplyDelete
  17. You didn't see Slaa and Mbowe laughing when they came out from court as if there is nothing happened? ooh God punish these peoples who are pretending to be with poor while they rob from poor their house wives because of their wealth from our tax. Aaamin

    ReplyDelete
  18. I am not supporting Mbowe or Slaa at all. In fact, I think some of their politics is odious,divisive and dangerous. What I am supporting is the right to demonstrate, the right to life and the right to the due process of law.I believe the govt mismanaged the demostration and as such we have to live with the consequences of their ineptitude. Lives, some very young, have been lost. Is there any justification. Who was incharge and is there a case of incomptetence,lack of pre-planning or foresight. Oh no, I am not in the Mbowe/Slaa mad bandwagon but I will support their rights (and of their supporters) though I disagree with their style and brand of politics. As for their laughing, I think it is all a show off, "You see, we are out" - gangster style. I wouldn't bother, it is to be expected from the lot. Maybe the deaths and the mayhem to them is a "political gain". Still that does not stop me and you to fight for RIGHTS and JUSTICE. The standards of many politicians are very low; I am sure you don't want to be judged by those sub-standards. - Mohamed

    ReplyDelete
  19. Sasa Mimi (Makamba) nawapa pole walioathirika na maandamano hayo lakini pia nalilia mali za CCM zilizoharibiwa. Gari la katibu wangu wa Mkoa limevunja vioo na ofisi yetu imeharibiwa vibaya," alisema Makamba mwisho.

    Hii ni kauli ya kiongozi anaeongoza watu. Yaani ndugu zangu watanzania tunakubali upumbavu huu. Kweli watu wameuwawa, wamejeruhiwa bila sababu yeye analilia mali wakati hiyo mali imeharibiwa baada ya polisi kupoteza amani. Na isitoshe Roho ya mtu, uhai wa mtu haupatikani lakini yeye analilia magari, malandicruza. Ninaomba watanzania mtafakari mnisaidie kumjibu. Makamba upo njia ya parapanda .........

    ReplyDelete
  20. Bwana Mohamed pengine ungeandika kwa kiswahili maana wengi wetu kiingereza kimetupiga chenga,mimi nakubaliana na wewe bila shaka yoyote kuhusu uhru wa watu kuandamana lakini pia hoja yangu ni kuwa uhuru huu usiingilie uhru wa watu wengine katika shughuli zao za kawaida. Ningeandika kwa kiingerza lakini wapo wasioelewa ndio maana nimeandika kwa kiswahili,na kuna wengine wanadhani kuwa unapopingana nao basi wewe ni moja kwa moja unasapoti mauaji ya raia yaani kama vile waliokufa/walioathirika ni wafuasi wa chadema pekee,hili jambo linatuathiri wote sisi hasa sehemu husika ya tukio. Wafuasi wa chama chochote msijipe madaraka ya kuwaamulia Watanzania

    ReplyDelete
  21. Iko hatari kwa VIONGOZI wa Chama Tawala CCM kung'ang'ania MASILAHI YAKO na kufumbia HAKI za Watanzania walio wengi wasio wana CCM. Huu ni UROHO wa madaraka...wanataka waendelee kutawala huku WAKIFUMBIA MACHO ishara za MADILIKO ili wapate KUVUNA WALALE KWA AMANI kwa gharama ya damu za WANYONGE. Kukubali Katiba mpya ni kelele zizowasumbua. HAISHANGAZI kusikia Mheshimiwa KIKWETE KUDAI tukio la ARUSHA ni ISOLATED INCIDENT. Tangu uchaguzi mkuu kwisha KIKWETE, NAHODHA na MAKAMBA na viongozi wa CCM walikuwa hawaoni kuwa DEMOKRASIA haikutendeka Arusha wakati MBUNGE AKIPIGWA na POLISI wa MWEMA...UONGOZI WA CCM ULIKUWA HAUONI ISHARA ZA HATARI ZINAZOJIRI. Kama Mheshimiwa KIKWETE na MAKAMBA wangejiSHUSHA KIDOGO na kushauri uchaguzi wa Mayor urudiwe Watanzania tusingefikia kuona DAMU YA WATU YENYE GHARAMA ISIYONUNULIKA KUMWAGIKA. Viongozi wakuu wa nchi hii JARIBUNI KUWA KARIBU NA MUNGU ILI TUIFURAHIE NCHI ALIYOTUPA MUNGU...UBINAFSI WA KISIASA NA UTENGANO HAUTUFIKISHI PAHALA PEMA. TUNAISHI LEO KESHO HATUPO..TUPENDE KUWA WAJASIRI WA UKWELI JAPO UNAUMA LAKINI ...TUMEKUBALIKA MBELE YA MUNGU NA WATOTO WETU..

    ReplyDelete
  22. Kauli ya Mheshimiwa MAKAMBA haiingii akilini kutaka kufananisha gharama ya damu kumwagika na uharibifu wa vioo vya gari na ofisi ya Katibu wake. Mimi nadhani ushabiki mwingi wa KISIASA na kejeli kwa Watanzania wasio wana CCM hautufishi mbali. Iko haja ya KULIA NA WALIAO na siyo vinginevyo. Ningeona vema CCM ikajiwakilisha kwenye msiba wa Arusha. HII ndiyo namna tukavyoonyesha UKOMAVU WA KISIASA utakaotuwezesha kuacha sifa na mwelekeo mzuri kwa watoto wetu.

    ReplyDelete
  23. Mi nashangaa! eti polisi wanadai kuzuia maandamano kwa sababu ya kulinda amani, sasa kwa mtu wa kawaida ambaye hahitaji mkalimani ili atafsiriwe! aliyefunja amani pale Arusha ni nani kati ya POLISI na WAANDAMANAJI?

    Mi nafikiri polisi ijiangalie kwa upya.

    ReplyDelete
  24. Nyie mnaotukana hovyo walio na mawazo tofauti na nyie someni hili na muwatukane waliosema.: Gazeti la Mwananchi 8/1/2011 :-Maaskofu hao pia waliigeukia Chadema wakisema haiwezi kukwepa kuwa sehemu ya chanzo cha vurugu hizo kwa sababu ilikuwa na uwezo wa kuwazuia wafuasi wake kutoandamana ili kutii amri iliyotolewa na polisi.

    "Lakini pia Chadema walitakiwa kufanya kila jitihada kuwajulisha wafuasi wake kutoandamana licha ya kuzuiwa kufanya maandamano hayo muda mfupi kabla ya kuanza," alisema Askofu Lebulu.

    Kutokana na vurugu hizo, Maaskofu hao walisema Serikali inapaswa kushughulikia mgogoro wa Arusha kwa hekima, busara na uwazi kwani ni dhahiri kuwa taratibu za kumchagua Meya zilikiukwa.

    Askofu Lebulu pia alisema Serikali inapaswa kuchukua tukio la Arusha kama jambo la kitaifa na kufanya jitihada za kulishughulikia haraka na kwa amani.

    Naye, Askofu Thomas Laizer wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Arusha, alisema kutokana na polisi kutumia nguvu kubwa, hawatasitisha mahusiano yao na Serikali pamoja na polisi kwa sababu kufanya hivyo ni kujitenga na majukumu.

    "Ushirikiano wetu hauwezi kukatishwa na vurugu hizi kwani huwezi kutatua tatizo kwa kulikwepa," alisema Askofu Laizer.

    Katika kikao hicho, pia walihudhulia Askofu Martin Shao wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini, na maaskofu wa makanisa na Kipentekoste ya mkoani Arusha.

    (Mwanzoni nilistuka kwa kauli ya kutomtambua meya lakini Kwa kauli hii naungana na nyie Maaskofu maana kauli zingine zilimfanya Slaa na kundi lake kama malaika wasiotenda kosa,hata magazeti hayakuonyehsa uharibifu uliofanywa na mashabiki wa chadema kama vile hakuna maafa mengine zaidi ya waliyoyapata chadema.Meya wa Arusha cheo cha umeya hakina thamani zaidi ya maisha ya watu,chunga kauli zako) Nilisema mapema hakukuwa na sababu Slaa kuwaambia wafuasi wake kwa maelfu waende polisi kuwatoa viongozi wao kwani dhamana haiihitaji watu wengi,angeenda yeye na viongozi wenzake ingetosha,kujipatia umaarufu kwa kuangamiza maisha ya watu na mali zao hakuna maana yeyote iwe kwa slaa na kundi lake au kikwete na kundi lake. BADO NASEMA UHURU NA HAKI YAKO USIINGILIE HAKI NA UHURU WA WATU WENGINE.

    ReplyDelete
  25. Maneno ya maaskofu ni mazuri. Nadhani wamehitimisha mjadala huu kwa mawazo na kauli za busara kulingana na ulivyonukuu gazeti.Kweli makosa yalifanyika pande zote mbili lakini kila wakati ni sharti tukumbuke kwamba watu walikufa na hawo watu waliuliwa na polisi. Hilo ni la msingi kwani serikali imekiri. Kila raia anahaki ya kulindwa ikiwa pamoja na waandamanaji(hata wahalifu). Kwa kawaida vifo vikitokea maangamzi mengine huchukua mstari wa nyuma. Sisemi kwamba viongozi wa Chadema ni malaika,la hasha. Lakini mauwaji yalifanywa na polisi chini ya uongozi wa serikali. Wajibu ni wa serikali la sivyo basi haitakuwa na haki ya kuchukua wadhifa wa kuongoza kama serikali.Hoja kwamba maisha ya watu yaliingiliwa hapo haina uzito - kwa maoni yangu dhaifu. Lazima serikali ilinde maisha ya raia wote na ijitahadhari kutumia visingizio visivyo na uadilifu. Arusha ni somo zuri kwetu sote. (Ndugu mwandishi nitapunguza kuandika kwa kiingereza) -Mohamed/Mwenda Pole

    ReplyDelete
  26. Ni vyema Slaa na kundi lake viongozi na serkali walipe fidia za watu waliouwawa,kujeruhiwa na mali zilizoharibiwa. wote walitakiwa kuliona hili kwanza

    ReplyDelete
  27. Ni muhimu watanzania tutambue hii serikali haitatupa haki yetu bila kumwaga damu kama ilivyotokea huko Kenya. Huu ni mwanzo tuu hatutasimama na kukaa kimya mpaka haki yetu ya Demokrasia ipatikane VINGINEVYO DAMU ILIYOMWAGIGA ITAKUWA IMEPOTEA BURE. Ufortunately viongozi wa jeshi la polis na serikali wamelewa madaraka hawajali watu kufa mradi tuu walinde maslahi yao.

    ReplyDelete
  28. CCM TUMEWACHOKA NA UNAFIKI NA UZANDIKI WENU. BADO KITAMBO TU DUNIA YOTE ITAJUA MLIVYO. MNANG'ANG'ANIA MADARAKA KAMA WAKOMUNISTI WA URUSI. LAKINI NA WAO WALIPOROMOKA BAADA YA MIAKA 70 TU. MMETUMIA POLISI KUUA, MNADANDAYA WANYONGE, MNANUKA RUSHWA KILA KONA - AU MMESAHAU KURA ZENU ZA MAONI NA WAKATI WA UCHAGUZI MLIVYOKUWA KICHEKESHO NA AIBU, HAMKUBALI MAKOSA, NANI ASIYEWAJUA??? MNA MAADILI KWELI NYIE?? SHAME ON YOU!! KWA KWELI WAPERNDA HAKI NA AMANI WAMECHOKA. HAMNA KAZI ZINGINE ZA KUFANYA? KILIMO KWANZA KINAWAHITAJI, MBONA MNANGANGANIA KUTAWALA WATU WALIOWACHOKA?? HAMNA TOFAUTI NA ZIMBABWE, GGABO, NA MADIKITETA WENGINE. MNATUMIA UNYONGE WA WTZ KAMA MTAJI WENU WA KISIASA MTU AKIWASIFIA MNAFURAHI HATA NI SIFA FEKI, AKIWAKOSOA MNAMPA LABEL YA KIDINI AU UKABILA. CHEAP THINKING!!

    ReplyDelete
  29. NYIE WACHAGA MSITUSEMEE TUMEICHOKA CCM,KAMA TUMEICHOKA KIKWETE ANGEKUWA MADARAKANI LEO? CHEAPTHINKING NI WEWE UNAYEONA MAWAZO YAKO NI YA WATANZANIA. KIKWETE NI RAIS HALALI WA TANZANIA NA KAAPISHWA KWA MUJIBU WA SHERIA ZA TANZANIA SUBIRINI 2015,KWA SASA FUNGENI KARO ZENU.

    ReplyDelete
  30. Ukizungumza kuichoka CCM zungumza kwa niaba yakom wenyewe,usizungumzie Watanzania,jibu sahihi unalo ukiangalia bunge letu la Jamhuri,vyovyote utakavyotafsiri shauri yako lakini hali halisi ndiyo hiyo kama ulivyoambiwa subiri 2015,uichoke kwa vitendo na ujaze wasio CCM bungeni,kwa sasa ufunge karo lako kweli

    ReplyDelete
  31. wewe hapo juu unayetetea ubabe na rushwa; wizi wenu wa kura na rushwa yenu hata watoto wa shule ya msingi wanajua!! you have no moral authority hata ya kuzungumza maadili. imebaki matusi na ubabe. ninyi ni milioni 4 tu. wanachama. kwa bahati mbaya mnafurahia umaskinishaji wa walio wengi. rushwa ndio value yenu, na kufurahia uzembe na uporaji wa raslimali ya nchi kupitia EPA, KAGODA, RICH, etc.kenye siasa ni uchakachuaji na kutumia unyonge wa wtz maskini. values zenu zipo upside down si mmnajijua?? kama hamna rushwa semeni na kama hamchakachui semeni basi?? badala ya kusema hoja unasema ni ucghaga what is uchaga here? but a downfall yenu ipo njiani kabisa. it is a matter of time, according to history. I can assure you!!! hata risasi zenu zitawarudi wenyewe kama yaliyotokea kwa Cheuschescu wa romania na makommunisti ya urusi. nawe unazungumza kwa niaba ya 4 out of 40 million??

    ReplyDelete
  32. and the problem siyo fulani kuwa raisi. kuwa rais for doing what?? that is the question. second, sheria yenu inaweza kutangaza mtu yeyote kuwa rais. hata mziray angetangazwa angekuwa rais. si kutangaza tu?? so unafurahia mtu tu kutanganzwa kwa kutumia oppressive law? what a shame!! tunazungumzia principles and valuea and not personalities here. let us talk about performance and not just wielding power; meeting voters needs and not merely exploit their ignorance!! do you see the point.

    ReplyDelete
  33. No,I don't see the point.So you think Tanzanians are fools who are exploited and you are the messiah. What principles and values are you talking about? Tanzanians voted by a huge majority for the President and the Party (CCM) they thought best placed to fulfill their desires including values and principles. The election was acclaimed to have been free and fair by Tanzanians and the international community. Chadema not only lost but lost miserably. That is a fact.Now is the time for you (Chadema) to start preparing for 2015 but by the looks of it you are on the wrong footing.

    ReplyDelete
  34. Bahati mbaya hawa wajinga wa kichaga wanafikiria JK ataanguka leo au kesho,poleni sana hapa ni mpaka 2015,yeye ni rais halali wa nchi hii kwa mujibu wa katiba, WHAT IS HAPPENING NOW WAS PREPARED BY CHURCH AFTER FALLING DOWN WHAT WAS SUPPORTED BY THEM. Msituone kimya mkafikiri tunawaogopa ITS A MATTER OF TIME

    ReplyDelete
  35. Serikali ya Mheshimiwa Dr. Jakaya sina imani nayo kama ita kuwa ina subiri maafa ndiyo ikubali kutatua migogoro ya kisiasa je hawa walio kufa bila hatia yeyote, familia zao ndugu za marehemu na jammii kwa ujumla wata jisikiaje, Serikali yako mweshimiwa haiko makinki hatakidogo.

    ReplyDelete