07 January 2011

Mbowe, Slaa kizimbani

*Washtakiwa kwa kukusanyika bila kibali
*Serikali yakubali kuzungumza na CHADEMA


Glory Mhiliwa na Reuben Kagaruki

WAFUASI 31 wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akiwemo Mwenyekiti wake
Bw. Freeman Mbowe wamepandishwa kizimbani kwa shtaka la kufanya kusanyiko bila ya kibali.

Akisoma shtaka hilo jana  mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha,  Bw. Charles Magesa, Mwendesha mashtaka wa Serikali Bw. Zakaria Elisaria aliiambia mahakama kuwa washtakiwa hao Januari 6  mwaka huu walivunja sheria kwa kufanya kusanyiko bila ya kuwa na kibali hivyo kusababisha uvunjifu wa amani katika jiji la Arusha.

Hata hivyo mahakama hiyo ililazimika kuendesha kesi mara mbili ambapo washtakiwa 26 walisomewa mashtaka yao mahakamani na  washtakiwa wengine akiwemo mchumba wa Dkt. Willbrod  Slaa Bi. Josephine  Mushumbusi, mahakama ilihamia hospitali ya  Mkoa wa Arusha ya Mount Meru ambapo walisomewa mashtaka yao.

Baada ya mwendesha mashtaka kusoma shtaka hilo kwa washtakiwa waliokuwepo mahakamani, Hakimu Magesa, alisema dhamana ni haki ya mtuhumiwa hivyo aliwataka kama wanawadhamini kwa sharti kwamba mmoja lazima awe mkazi wa Arusha, wanaweza kudhaminiwa.

Washtakiwa hao 26 waliokuwemo mahakamani ambao ni pamoja na  Bw. Freeman Mbowe, Dkt. Wilbroad Slaa, Bw. Godbless Lema, Bw. Basil Lema, Bw. Philemon Ndessamburo  Bw. Joseph Selasini, wote walidhaminiwa.

Baada ya hapo mahakama ilihamia Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru na kuwasomea mashtaka washtakiwa sita ambao hali zao zilikuwa mbaya kutokana na kujeruhiwa kwa risasi za polisi  waliokuwa wakizuia maandamano.

Baada ya kusomewa mashtaka  na  Wakili wa Serikali Bw. Elisaria, washtakiwa hao nao walipata dhamana baada ya kutimiza masharti.

Kesi hiyo iliahirishwa hadi Januari 21 itakapotajwa tena baada ya upande wa mashtaka kuiambia mahakama kuwa upelelezi haujakamilika.

Watuhumiwa hao wote wanatetewa na mawakili Bw. Method Kimbogoro  na Bw. Albert Mtando huku upande wa Jamhuri ukiwa na Bw. Elisaria, Bw. Haruni Madaga pamoja na Bw. Robert Rogert.

Jana kesi zingine zote zilisimama mahakamani hapo na wananchi waliokuwa na kesi zao kuamriwa kutoka nje ya eneo hilo.Kitendo hicho kilisababisha mvutano kati yao na polisi. Hata hivyo baadae hali hiyo ilitulia.

Msajili wa mahakama hiyo, Bw. George Hubert alipoulizwa kuhusu kesi hiyo kusababisha zingine kusitishwa, alisema kesi zingine ziliendelea kama kawaida isipokuwa zilisikilizwa mapema.

‘Kesi zingine zimesikilizwa mapema tangu asubuhi hakuna kesi ambayo haikusikilizwa ila tulimaliza mapema ndio maana hamuoni kama kuna kesi zinaendelea’ alisema Bw. Hubert.Wakati huo huo watu watatu wamethibitika kufa kwa kupigwa risasi na wengine 26 kujeruhiwa na polisi katika vurugu za juzi

Jana, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Dkt. Salesh Toure alithibitisha vifo hivyo ambapo alisema  watu hao walikufa muda mfupi baada ya kufikishwa hospitali.

"Ni kweli tulipokea majeruhi wakiwa na majeraha ya risasi, wengine 26 wanaendelea vizuri. Waliofariki tumewatambua kwa kuwa ni Dennis Machael mkazi wa sakina yeye alikuwa na majeraha ya risasi mbavuni, George Mwita ambaye risasi ilipita kwenye utumbo, mwingine jina lake halikuweza" alisema Dkt.Toure.

Alisema majeruhi wengine wanaendelea kupatiwa matibabu.
Kamanda wa  Polisi Mkoa wa Arusha Bw. Thobias Andengenye akizungumza na waandishi wa habari alisema CHADEMA walikuwa na kibali cha mkutano si cha maandamano."Tuliwakubalia kufanya maandamano na mkutano lakini baada ya kupata taarifa za kiintelijensia kwamba fujo zitatokea tulisitisha lakini wao waliendelea na maandamano," alisema Kamanda Andengenye.

Alisema kutokana na ghasia hizo mbali ya watu kujeruhiwa jengo la CCM liliharibiwa pamoja na  mali za wananchi.
Aliwataka wakazi wa Arusha kujiepusha na ghasia zozote na watoe ushirikiano wa polisi pindi watakapobaini watu wanaotaka kuharibu amani.
Aidha alipoulizwa kuhusu  waandishi wa habari kujeruhiwa kwa kupigwa na askari alisema hana taarifa hizo."Sijui kama kuna waandishi waliopigwa au waliokamatwa wakiwa kwenye mkutano wa CHADEMA nitafuatilia," alisema.

Aidha Kamanda Andengenye alisema askari watakaobainika kuchochea ghasia kwa kuharibu mali za raia watachukuliwa hatua."Kwa sasa ni mapema kuzungumzia ila hata askari hakuna aliye juu ya sheria wakibainika kuharibu mali za wananchi  nao  tutawachukulia hatua," alisema.

Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha (APC),kimetoa tamko kulaani  kupigwa waandishi kwenye tukio hilo.Akitoa tamko hilo kwa waandishi wa habari Katibu APC Bw. Eliah Mbonea alisema  APC inalitaka Jeshi la Polisi kuomba radhi kwa  kuwapiga na kuwanyanganya vifaa vyao vya kazi.

"Tunataka watuombe radhi wasipofanya hivyo APC tunatangaza rasmi kuwa hatutafanya kazi za Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha" alisema Bw. Mbonea.

Alisema ni jambo la kushangaza kuona waandishi wakipigwa na kunyang'anywa vifaa vyao vya kazi na polisi wakati  wakitekeleza majukumu yao ya kila siku.Waandishi waliojeruhiwa kwa kupigwa na polisi ni Musa Juma, Mosses Mashalaa, Mosses Kilinga na Ashraf Bakari.

Serikali yakubali mazungumzo SIKU mbili baada ya kutokea vurugu zilizosababisha watu wawili kuuawa na polisi kwa risasi, sita kujeruhiwa huku viongozi wa kitaifa na wabunge wa CHADEMA wakikamatwa, serikali imesalimu amri na kutangaza kushughulikia mgogoro wa Arusha kisiasa ili kuupatia ufumbuzi.

Uamuzi huo ulitangazwa Dar es Salaam jana na Waziri wa Mambo ya Ndani, Bw. Shamsi Vua Nahodha, alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu vurugu zilitokea mkoani Arusha juzi zikihusisha polisi waliokuwa wakidhibiti wafuasi wa CHADEMA waliodaiwa kuandamana kupinga uchaguzi wa meya, uliofanyika bila kufuata taratibu.

"Serikali imedhamiria kukutanisha wanasiasa wa pande husika (CCM na CHADEMA) ili kuupatia ufumbuzi mgogoro wa Arusha, kwa kuwa wakati wa pande mbili kuridhiana umewadia," alisema Bw. Nahodha.

Alipoulizwa serikali ilikuwa wapi kushughulikia mgogoro huo hadi isubiri damu imwagike, Bw. Nahodha alisema hiyo ilitokana na kuwapo kwa nadharia na taaluma za aina tatu za kusuluhisha migogoro.

Alisema kabla migogoro haijatatuliwa ni lazima wahusika wakuu waamini kuwa kuna mgogoro.

"Pia kabla ya kutatua mgogoro huo ni lazima upate watu wanaokubalika kuutatua," alisema na kuongeza kuwa kigezo cha tatu ni kujua ni watu gani wanahusika."Kwa sasa naamini kuwa wahusika wakuu wanaamini hapa (Arusha) kuna tatizo," alisema, Bw. Nahodha. Hata hivyo alisema jitihada za siri zimekuwa zikifanyika kusuluhisha mgogoro huo, lakini hazikutoa matokeo yaliyotarajiwa na sasa kilichobaki ni kuutafutia ufumbuzi kwa uwazi.

Alipoulizwa na waandishi wa habari ni lini suluhu hiyo itapatikana, Bw. Nahodha alijibu; "Nadharia ya kusuluhisha migogoro ni lazima wasiwepo watu ambao wana haraka, ni vigumu kusema usuluhishi utatumia muda gani, sana sana itategemea weledi wa wale wasuluhishi na wahusika."

Alipoulizwa ni kwa jinsi gani wananchi watamwamini yeye, hasa kwa kuzingatia tukio la mauaji ya juzi mkoani Arusha ni la pili kutokea kwake akishikilia nafasi nyeti serikalini, baada ya lile ya Januari 21, 2001 akiwa Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, ambapo wafuasi 21 wa CUF waliuawa; Bw. Nahodha alijibu;

"Mbona unihukumu kuwa mimi nimechangia maridhiano ya kikatiba Zanzibar iliyounda Serikali ya Kitaifa ambayo waandishi wa habari mnasifia?

"Mbona hamnisifii kwa mema? Hivyo ndivyo maisha yalivyo, ndiyo maana kuna wakati bahari inachafuka na kutulia."

Alisema Tanzania ni nchi yetu wote, hivyo tuna wajibu wa kuilinda amani iliyopo.

Akieleza kiini cha vurugu za juzi, Bw. Nahodha alisema  viongozi wa CHADEMA hawakufuata ushauri wa polisi wa kuwataka kufanya mkutano peke yake na kuacha maandamano.

Alisema polisi walizuia maandamano hayo baada ya kubaini hayatakuwa na mwisho mwema. "Viongozi wa CHADEMA hawakufuata ushauri wa polisi na badala yake waliendelea na dhamira ya kuandamana," alisema na kuongeza kuwa baada ya wafuasi na viongozi wa CHADEMA kuandamana polisi walilazimika kuwatawanya.

Alisema baadhi ya viongozi wa chama hicho ambao hawakukamatwa, walikimbilia kwenye mkutano ulioendelea vizuri, lakini baada ya kumalizika waliamuru wafuasi wao waende polisi kuwatoa wenzao waliokamatwa.

Bw. Nahodha alisema ili kuepusha shari baada ya kuona magari yakipigwa mawe, nyumba na vibanda kuchomwa moto, polisi walilazimika kuepusha shari.

Alisema katika vurugu hizo watu wawili waliuawa, na wengine sita kujeruhiwa. Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Said Mwema alithibitisha watu hao kuuawa kwa kupigwa risasi na polisi.

Bw. Mwema alisema wakati wa kushughulikia tukio hilo watafuata utaratibu wa kisheria na iwapo wao (Jeshi la Polisi) wakishitakiwa wataenda kujitetea. Bw. Mwema alielezea kusikitishwa na vifo vya watu hao.

"Hata akifa mtu mmoja au kuumia ninasikitika, hatuna sababu ya kuficha idadi ya waliokufa...sisi hatupendi mtu afe au kujeruhiwa," alisema wakati akijibu swali kuhusu tetesi kwamba waliokufa katika tukio hilo ni 10.

Alipouzwa madai kuwa hivi sasa anatumika kisiasa, Bw. Mwema alijibu; " Natumika kwa mujibu wa sheria, sheria hizo hizo ndizo zinatumika kutuhukumu."

Kauli hiyo ya IGP iliungwa na Bw. Nahodha ambapo alisisitiza kwamba hajaona kama, Bw. Mwema anatumika kisiasa. "Kama anatumika kwa namna fulani kusaidia chama fulani hilo sijaliona," alisema Bw. Nahodha.

Bw. Mwema alipoulizwa sababu za kuongeza askari mkoani Arusha kutoka Chuo cha Polisi Moshi, Ukonga Dar es Salaam na Manyara, alikanusha askari wa Ukonga kupelekwa Arusha.

"Hakuna askari waliotoka Ukonga, lakini kuweka askari wa akiba kwa ajili ya kukabili yaliyotokea, sio kosa," alisema.

Katika hatua nyingine, wananchi mbalimbali wamelaani kitendo hicho, akiwamo Mhadhiri Msaidizi wa chuo cha Diplomasia jijini Dar es Salaam, Bw. Abdallah Majura aliyesema Jeshi la Polisi limeirudisha Tanzania hatua kadhaa nyuma kwa kutumia nguvu nyingi badala ya kuacha mgogoro wa uongozi wa Arusha kutatuliwa kwa mazungumzo.

Mhadhiri huyo alisema Tanzania imeshapiga hatua ndefu mbele kwa kusaidia kutatua migogoro mikubwa nje ya nchi, lakini kitendo hicho kimemsikitisha kwa serikali kushindwa kutatua mgogoro huo mdogo wa ndani."Ninakilaani kabisa kitendo hiki, polisi wanatakiwa kupewa elimu maalumu katika kutatua migogoro na kilinda haki za binadamu. Napendekeza turudi chini katika mazungumzo na ikiwezekana uchaguzi uliozua mgogoro ufanyike upya," alisema Bw. Majura.

Naye Catherine Malila alipiga simu cha habari na kulaani hatua hiyo ya polisi, akisema bunduki hazikuwa zinastahili kutumika kwa watu wanaopigania haki ya kidemokrasia, na kama ni muhimu zingetumike kwa mafisadi wanaofilisi uchumi wa nchi.

42 comments:

  1. WANAOTAKIWA KUSHTAKIWA HAPA NI POLISI WALIOWARUSHIA RAIA RISASI HADHARANI KAMA MAJAMBAZI. KITENDO CHA KUWAPIGA RISASI RAIA WAKIWA WANAANDAMANA NI KINYUME CHA SHERIA ZA NCHI KWANI KOSA LA KUANDAMANA ADHABU YAKE SI KIFO.POLISI WOTE WALIOWARUSHIA RAIA RISASI WALIPASHWA WAPANDISHWE KIZIMBANI KWA KUTUMIA EXCESSIVE FORCES KINYUME CHA SHERIA ZA NCHI.
    MIMI KM MWANASHERIA NILITEGEMEA CHADEMA WANGEWAFUNGULIA POLISI HAWA KESI ZA MAUAJI THE NEXT DAY KWANI NI KINYUME NA HAKI ZA BINADAMU NA PIA NI KINYUME CHA SHERIA ZA NCHI KUWAPIGA RISASI RAIA ETI KWA KOSA KUANDAMANA.KIKWETE ANA HASIRA ZA WATU KUMKATAA KWENYE UCHAGUZI ULIOPITA KUTOKA USHINDI WAKE WA ASILIMIA 84 MPAKA 60 KWAHIYO ANAJARIBU KUTUMIA MABAVU KUWATALA WATANZANIA KAMA MUGABE WA ZIMBABWE BAHATI MBAYA WATANZANIA HATUTAMRUHUSU KUFANYA HIVYO KWANI KUANZIA SASA TUTAANZA KUKUSANYA MIKANDA YOTE YA MASHAMBULIZI YAKE ANAYOYAFANYA DHIDI YA RAIA TAYARI ANA DAMU MIKONONI MWAKE KWAHIYO BADO ATAENDELEA NA OPERATION YAKE YA KUUWA RAIA ILI KUMFIKISHA KWENYE MAHAKAMA ZA KIMATAIFA.

    ReplyDelete
  2. Utawala Wa CCM Umefika Mwisho. Kwa kuwa ni utawala dhalimu. Unauwa raia wake wenyewe.
    Polisi wametangaza uadui na wananchi. W

    Serikali inapoanza kuwadhuru wanachi wake inapoteza uhalali. Kutokuitii ni sawa kabisa na hakuna Consequences zozote.

    ReplyDelete
  3. Tunaomba sana askari waaliouwa watu wasio na hatia wafikishwe mahakamani. Kwani hata kama polisi walitasema waliandamana kinyume cha sheria adhabu yake haikuwa kuwapiga risasi. Mbona mafisadi Kikwete akiwaambia awakamate anasema anafuata utawala wa sheria? Kwanini asifuate utawala wa sheria wananchi wanapoandamana kwa amani kudai haki yao ya kidemocrasia? Wao wangeliwakamata viongozi wa chadema na kuwapeleka mahakamani na si kuuwa raia wasio na hatia. Yote hiyo ni hasira ya Kikwete kukataliwa na watanzania. Anajua fika kwamba watanzania hawamtaki tena. Kwa sababu ya kukumbatia mafisadi wanaotumia mtandao uliomuingiza madarakani kwenye awamu yake ya kwanza. Sasa watanzania tunasema kwamba lazima katiba iandikwe na wale wote walioua raia wasio na hatia wapelekwe kwenye vyombo vya sheria ili haki itendeke. Damu ya watanzania iliyomwagika bila hatia haiwezi kumwagika bure hivi hivi tu. Lazima wote waliowauwa wapelekwe mahakamani na kushitakiwa. La sivyo hakutakuwa na amani lazima wale ambao ndugu zao wameuawa bila hatia watakuja kulipa kisasi siku moja. Kikwete ana watoto je ana hakika ya kuwapa watoto wake ulinzi kila waendako? Au kuua watoto wa wenzake ni sawa ila kuuwa watoto wake si sawa? Kama tu Denis alivyouwa kwa amri ya Kikwete kwani tunajua kabisa ni yeye aliyeamua dakika ya mwisho kusitisha maandamano wakati kibari tayari kilishatolewa. Hotuba yake mwaka mpya ni kilelezo tosha kwamba amehusika kuua damu isiyo na hatia. vile tu ambavyo damu ya Denis, Omar na mwenzo ilivyomwagika ndivyo inavyotakiwa damu ya Riwadhi Kikwete imwagike ili baba yake aone uchungu wa kuuliwa mtoto. Watanzania hatutakubali na awape ulinzi watoto wake wote mchana na usiku. Lakini itakuja siku watanzania tutalipa kisasi. Ili Kikwete naye aone uchungu wa kuuliwa mtoto.

    ReplyDelete
  4. mazungumuzo ya nini? na uchaguzi wa meya ni wa nini ? kwani hamjuikuwa CHADEMA ni wengi basi wapen umeya wao. hili ni tatizo la nchi kutawaliwa na wanajeshi waliojifanya raia makamba ndio hana akili wala busara kikwete mtoe atakufikisha kusiko

    ReplyDelete
  5. kwani tuna jeshi Tanzania ya leo jeshi lolote ni la Nyerere kama alivyo imba Komba AMANI imetoweka na Nyerere. polisi woooooooote mguu pande nyuma geuka!Akili geuka ! bangi vuta ! MWEMA ni kijembe ! jina lako SIO hilo kinyume cha mwema ni.........? mguu sawa mwili legeza ...... mwema NO katili endelea kuua raia.

    ReplyDelete
  6. Matatizo yote haya ni kwa ajili ya makamba. tunaomba tuungane wote kwa pomoja tumngoe kwa maandamano arudi kwao. Sasa yeye anaongoza TZ au yeye ni kibaraka wa nani? Angekubali mwanzoni haya yote yangetoka wapi. Makamba kwa taarifa yako ningekuwa na uwezo wa kukufikia hata kwa garama yeyete ningekuja tupambane. Blali shiti ngozi nyesi kama roho yako

    ReplyDelete
  7. Kwa kweli inasikitisha sana polisi kutumia risasi badalaa ya mabomu ya machozi, hayo ni maandamano wananchi walikuwa wakidai haki zao na sio majambazi inakuwaje watumie risasi? ona sasa tumepoteza watanzania watatu waliomwaga damu yao bila hatia yoyote, Mh. Kikwete unalichukuliaje hili swala kwakeli huu siuungwana kabisa hii sio vita bali ni siasa watu wanadani haki zao.

    Polisi kuweni makini sana katika utendaji wenu wa kazi ipo siku mtakuja kuijutia hiyo kazi yenu, mnafanya tu ilimuonekne mnabidii kumbe hamna lolote ikitokea vita wa kwanza kukimbia majambazi wenyewe mnawaogopa. Fanyeni kazi kikamilifu sio kufuata mkumbo wakuone nawewe unajua kutumia Bunduki huo ni upumbavu siku moja hiyo bundi itakuja kuwa chungu kwenu.

    ReplyDelete
  8. CHadema Chadema mbona mnataka kubadili nchi iwe kama Ivory Coasrt? mmeambiwa msiandamane nyie mnaandaman kwani hamjui sheria ? mnachokitaka nyinyi basi kiwe tu hata kama kupoteza amani!! mkumbuke kwamba kupeleka mambo yenu kingivunguvu haitawasaidia tumieni busara zaidi. Kwani msingefanya maandamanao hoja zenu zisingesikikia? mntaka umaarufu at the expense of peoples lives! that is not acceptable. Mmepta wabunge wengi huo nio ushindi mzuri mjipange vizuri. sio kila kitu kuandamana kuandamana . Mi nadhani Chama chenu sasa Kiwe hiv: Chama Cha Deokrasia na MAANDAMANO.

    ReplyDelete
  9. Wanaotakiwa kufunguliwa kesi ni Polisi kwa kuua raia na si CHADEMA, Police hawana haki ya kutoa kibali cha mikutano na maandamano wajibu wao ni kulinda raia wanoandamana ili isitokee vurugu.Polisi wamekuwa wanasiasa na kutii amri kutoka kwa viongizi wao wasanii ili kuedeleza usanii wao.Hamna maana nyie majambazi yana vamia benki mchana kweupe mnashindwa kudhibiti na kusema hamna Polisi wakutosha hao waliodhibti maandamano wametokea wapi au mnalipa fadhila za kununuliwa Maprado yenye A/C.

    ReplyDelete
  10. Nani kageuza nchi kuwa kama Ivory Coast ? Chadema haijaua mtu. Nani kaua. Ni polisi chini ya uongozi wa CCM. Huo ndiyo ukweli. Waandamanaji wamepigwa risasi na polisi; serikali inakiri kwamba polisi walitumia risasi dhidi ya waandamanaji na kuua. Hilo ni kosa kubwa mnoooo. Suali ndugu ni kwamba: NANI KAUA watanzania. Mpaka sasa hawajaeleza makosa ya wale waliouliwa. Pengine walikuwa wapita njia tuu! Rambi rambi za Raisi ziko wapi !

    ReplyDelete
  11. wananchi msiwe na hasira na police, police ni watanzania kama sisi, tunahenya nao na familia zao katika huduma mbovu mbalimbali zinazotolewa na serikali ya CCM. Walichofanya police kupiga watu risasi sio kwa matakakwa yao wenyewe, kwani nature ya kazi ya askali yoyote ni kupokea na kutekeleza amri na kuhoji baadaye. kuna chain of command inayoanzia kwa wanasiasa (CCM)kwenda kwa amiri jeshi mkuu (mwenyekiti wa CCM taifa)kupitia kwa IGP Mwema kwenda kwa kamanda wa police mkoa wa Arusha kwenda kwa makanda mbalimbali wa mkoa na wilaya kwenda kwa vijana (police) ambao wanatekeleza amri ya kuchapa na kuua. hivyo wa kulaumiwa hapa sio police ila CCM. maana kama A=B na B=C basi A=C.

    ReplyDelete
  12. Well done Police force. askari utakae subiri uje uchinjwe na waandamanaji kama ilivyotokea Pemba wewe utakuwa si askari sahihi,wewe utakapo chinjwa watafunga midomo yao kwa sababu ni haki askari kuchinjwa,kama ningekuwa mimi hao watatu ni kidogo sana,wa kulaumiwa ni Slaa aliyewaambia waende ktuo cha polisi kuwatoa viongozi wao,kwa nini asiende yeye peke yake kwa dhamana inahitaji mamia ya watu.Polisi wa Tanzania fanyeni kazi yenu hao wanasiasa wanagombea hazina ya nchi kwa manufaa yao,mtu akija polisi kwa taratibu zake mpokeeni vizuri akija kwa shari mpokeeni kwa shari.NASEMA TENA WELDONE USINGOJE UKATWE KICHWA ANZA WEWE,NA HAO WANAOTAJA OCAMPO WAMESOMA HISTORIA YA KENYA AU WANAJISEMEA TU,OCAMPO INASHUGHULIKIA WALIOFADHILI NA KUCHOCHEA WANANCHI KUFANYA UNYAMA ULIOFANYIKA HUKO,NA WAFUASI WA CHADEMA WAMECHOCHEWA NA VIONGOZI WAO WAENDE POLISI KUWATOA VIONGOZI WAO NA AKATAMKA WAZI WENYEWE WATAJUA LA KUFANYA YEYE ASILAUMIWE,KWA MAANA HIYO WAKIUA,WAKICHOMA MALI ZA WATU,WAKIUMIZA WATU KWAKE NI SAWA,HIVYO JUENI KWA OCAMPO SIO MAHAKAMA ZA TANZANIA KAMA INAVYOMUANGALIA ALIVYOBEBA MKE WA MTU NA LICHA YA KUFUNGULIWA MASHTAKA BADO ANATESA NAE,OCAMPO HAMNA HILO HAKI INATIZAMWA PANDE ZOTE MCHOCHEZI NA MUUAJI.

    ReplyDelete
  13. pETRO eUSEBIUS mSELEWAJanuary 7, 2011 at 2:56 PM

    Mimi niliwahi kusema siku moja baada ya uteuzi wa Baraza 'jipya' la Mawaziri kuwa usanii wa CCM utatufanyia mambo ya hatari sana....ndo kama haya ya mauaji ya watu kule Arusha.CCM hawataki kuamini kuwa zile zama za chama chao kukubalika kila mkoa na kila wilaya zimeshakwisha.Zipo sehemu kama Arusha,Mwanza,Mbeya,Tarime,Kigoma,Ubungo,Mbulu,Ukerewe,Karatu,Iringa Mjini na Moshi CCM itake isitake itashindwa tu kuzitawala kwa amani kwakuwa watu wa huko hawaitaki tena.Kwanini wasikubali matokeo? Kwanini waue watu wanaotaka viongozi wao binafsi wa kuwaongoza? Uchaguzi kwanini usifanywe kwa haki? Hatari kubwa yanukia....si nzuri kabisa.CCM,tuepushieni haya tafadhali.

    ReplyDelete
  14. Wale wanaoshangilia vitendo vya kikatili vya polisi na waajiri wao wameonyesha dhahiri shahiri mawazo yao ya kinyama. Je, wangefurahia hivyo iwapo wale waliouliwa au kujeruhiwa vibaya wangelikuwa watoto wao au ndugu zao. Jamani tumepatwa na mkasa. Leo kuna matanga sehemu nyingi na vilio katika nyumba nyingi za Tanzania.Ni wajibu sote tusoneneke. Leo sio siku ya kusherekea au kusuta maiti. Hayo ni kama una akili timamu.Tangu lini adhabu ya kuandamana ikiwa kifo! Pole kwa jamii zote zilizofikiwa na mkasa huo.

    ReplyDelete
  15. Polisi pia ni binaadamu kama waliouwawa,je wewe angekuwa polisi ni ndugu yako amewahiwa na waandamanaji akakatwa shingo kama ilivyotokea Pemba ungefurahia kitendo hicho,au polisi waliojeruhiwa kwa mawe wao sio binaadamu? kila mtu ana haki yake,je hao walioharibiwa mali zao na waandamanaji wa Chadema? ilikuwa ni haki yao kufanya hivyo? Haki yako isiingilie haki ya mtu mwingine kwa utashi wa kushabikia chama.

    ReplyDelete
  16. Tunaomba Makamba aache kutumia Biblia. Atumia kitabu cha dini yake. Kwa nini anakebehi Ukristo.

    Hata siku moja humsikii akitumia kitabu cha dini yake. Kazi kuchakachua tu!

    ReplyDelete
  17. Hata Nyerere alikuwa akitumia Quran katika hotuba zake mbona hamkumwambia aache?

    ReplyDelete
  18. Naam,polisi ni binadamu. Hii haimanishi wawauwe watu. Kama mtu kafanya fujo au kachoma nyumba au mali ya mtu, basi afikishwe mahakama kwa hatia hiyo. Hiyo ndiyo kazi ya polisi. Maisha yana thamani. Mambo ya Pemba yanahusu vipi Arusha; kwani Arusha pana polisi aliyekatwa kichwa. Wale ambao hakizao ziliingiliwa walindwa kwa mujibu wa sheria. Siyo kwa kuwanyonga raia au kuwajeruhi. Umeona mashtaka dhidi ya viongozi wa Chaema: kufanya mkutano usio halali. Hivi ukiharibiwa mali, mtindo ni kuua. Na ushahid upo wapi iwapo mpaka sasa polisi hawaja mshtaki yeyote kuhusu hatia hiyo. Hizo ni dhana tupu.

    ReplyDelete
  19. Mwema alikwepa maswali kwamba waandamanaji hawakufanya fujo kwa mwendo wa kilomita mbili. Ghasia zilianza baada ya polisi kuwashambulia. Pana ushahidi mwingi kwamba polisi ndiyo walianzisha mashambulizi bila sababu. Pili, waandishi wa habari pia walishambulia na kuvuliwa zana zao za kufanyia kazi. Wengi walipigwa bure bure.La muhimu ni kwamba polisi wangedhibiti mambo kwa busara pasingetokea maafa. Ni dhahiri kwamba walipokea amri kuhakikisha kwamba mkutano huo uzimwe. Sasa nani atawajibika kisheria.Ikiwa haki itafanya kazi viongozi wa ngazi za juu lazima wajiuzulu na pia wafikishwe mahakamani. "Damu" ya myonge lazima sasa iende joshi.

    ReplyDelete
  20. Slaa alipotuma maelfu ya watu kwenda polisi kuwatoa watuhumiwa alijuwa wazi ni ngumu kupata ushahidi wa uharibifu wowote utakaofanywa na washenzi wake. nami nakuambia naam kama mtu kakosa haki afikishwe mahakamani,kiutaratibu huko ndio kwenye haki kama alivyokimbilia masikini mume wa kimada wa Slaa,sasa hata Slaa na kundi lake bado angetumia mahakama kudai jambo lolote analoliona si haki kwake na chama chake,na sio kuharibu mali za watu,kuhusu polisi ulingoja achinjwe ndio upate ushahidi.BADO NAKUAMBIA HAKI ZENU NI SAWA LAKINI PIA KUNA HAKI ZA WENGINE ZINAZOINGILIWA NA NYIE.UNATAKA USHAHIDI GANI WA POLISI KUPIGWA MAWE,UHARIBIFU WA MALI ZA WATU. NA KWA UJINGA WAKO ATI UNASEMA MAMBO YA PEMBA YANAHUSU NINI ARUSHA,WALE WA PEMBA NI BINAADAMU KAMA WA ARUSHA WALIO KATIKA JAMHURI YA TANZANIA,PIA WALIOUWAWA MWEMBECHAI HAWANA TOFAUTI NA WA ARUSHA KOTE NI NCHI MOJA NA SHERIA MOJA. HOJA HAPA HAKI YA KILA MTU IHESHIMIWE IWE YA POLISI,YA RAIA NA MALI ZAO. MAANDAMANO YENU YANALETA USUMBUFU MWINGI KWA JAMII NA NI BORA MFANYE SAA SITA USIKU MKIWA PEKE YENU NA KAZI ZA WATU ZITAKUWA ZIMEFUNGWA NA BARABARA ZITAKUWA WAZI. WEWE HUJUI ATHARI ZILIZO WAPATA WATU KICHUMI NA MALI ZAO SIKU HIYO YA MAANDAMANO? AMA KWELI UKIPENDA CHONGO HUONA KENGEZA

    ReplyDelete
  21. Mwanzo, nadhani matusi hayafai. Tuzungumze kiutu uzima laa sivyo basi hapatakuwa haja ya kujadili.Ninapo zungumza kuhusu Pemba ni kwamba hatia iliyofanyika huko sio kisingizio kufanya hatia nyingine Arusha. Nasikitishwa na yalifanywa Pemba na wajibu ni wa CCM ambayo imekuwa madarakani katika visa hivyo vyote kuchukua hatua - Pemba pamoja na Arusha na hata kwingineko. Maandamano hufanyika kote duniani. Ni njia inayokubalika kisheria kwa watu kudhihirisha matakwa yao katika nchi zinazofuata mfumo wa kidemocrasia. Hayo unayozungumzia kuhusu uhalifu na madai mengineo, hata Nahodha wala Mwema hawakutaja katika maelezo yao kwa taifa.Isitoshe,polisi hawajawafungulia mashtaka hayo ya uharibifu watu 31 waliokamatwa.Wameshtakiwa kwa kosa la kushiriki katika maandamano ambayo hayana kibali. Mbona hawajafunguliwa mashataka hayo unayotaja ? Waandishi wa habari na mashahidi wengine wamebainisha kwamba waandamanaji walitembea kwa mwendo wa kilomita mbili hivi bila fujo wala ghasia. Ghasia ilianza baada ya mashambulizi ya polisi. Mwema aliulizwa mara tatu swali hilo naye alikwepa- hakujibu. Mimi si mfuasi wa Chadema lakini naeleza mawazo yangu huru. Na mauwaji ya watu si jambo sahala. Hivi sasa watu wanahudhuria matanga - chanzo hatua za polisi chini ya uongozi wa CCM ya mauwaji holela. Peleka kesi hii katika mahakama huru yoyote duniani - hapana shaka itasajiliwa kama kitendo cha jinai.Uadilifu ni sifa moja ya utu.

    ReplyDelete
  22. Mimi ninadhani aliyeandika hapa juu anahitahika Muhimbli haraka sana kabla mambo hayaja mwaribikia. huyu ni kichaa, mwenda wazimu, au ni nyang'au tuinaishinalo huku mitaani. Sasa subiri maandamano hayoooo yanakuja tuone mshezi ni nani. Na huo mfano uliotoa Zanzibar uchunge sana. Kwa hiyo kisasi cha Zanzibar ndio mmekuja kukilipizia Arusha. Ndugu watanzania mambo hayo mjue kunakisasi cha kuchinjwa askari Zanzibar. Ndio maana makamba anatumia biblia kutukejeli.

    ReplyDelete
  23. Mwenda wazimu ni wewe usiyejua kujadili hoja,kutukana ni kukosa hoja. kuhusu mashtaka yaliyofunguliwa hayakuhusu uharibifu kwa mawazo yangu huo ni upofu,yale magari yaliyoharibiwa,moto uliochomwa hapa mtaa wa Pangani,ofisi ya ccm iliyovunjwa na watu wengine kuumizwa na mawe yaliyo rushwa na wafuasi wa chadema,mambo hayo yalijitokeza yenyewe? kesi hufunguliwa kwa ushahidi usio shaka,sasa wewe kama ungekuwa mwanasheria katika kundi kubwa la watu waliofanya uhalifu huo ungemshtaki nani? unatakiwa utoe ushahidi usio shaka kumuona mtu akitupa mawe,akichoma nyumba na kadhalika hiyo ndio sheria. Kuhusu wewe si mwanachama wa chAdema hiyo ni siri yako ya moyoni si rahisi kwa maumbile ya binaadamu kukuelewa ni wa chama gani? lakini hapa si hoja. hoja ni kuwa UHURU WAKO KIKATIBA USIVURUGE UHURU WA KIKATIBA WA MTU MWINGINE.NDIO MAANA TUNAUNGA MKONO HOJA YA KATIBA MPYA AMBAYO ITATOA KWA MAPANA ZAIDI UHURU WA RAIA. PIA KUNA UMUHIMU WA KUANGALIA MAANDAMANO YANAYOSABABISHA VURUGU NA MALI KUHARIBIWA,HIZI MALI ZILIPWE NA NANI,KAMA NI SERIKALI AU ALIYEHAMASISHA VURUGU. BADO NASEMA MAANDAMANO YENU YANAKERA WATU YAWE YA CCM,CUF,CHADEMA AU WENGINE

    ReplyDelete
  24. We mtu wa pili kutoka hapa huna akili, kwa hiyo ulitaka aandamane na nani? shwaini, wanaodai haki zao ni nani? kwanza hukuwepo Arusha, walionzazisha fujo ni askari kwa kuwapiga mabomu raia, kwahiyo ulitegemea raia wachukulie poa tu, lazima nao wajihami. na washukuru Mungu Arusha hakuna mawe mengi kama Mwanza shwaini. na hiyo nyumba ya mfanyabiashara iliyoungua ni bomu lililorushwa na polisi ndio lilisababisha kuungua kwa jengo hilo. Muwe mnafuatilia kabla hamjaanza kuropoka ovyo. watu waliokufa ni 4 akiwemo Mkenya mmoja kwa taarifa yenu. na siyo 3 kama mnavyodai. Arusha sasa hivi hatutaki mafisadi, ndo mwisho wenu huku. kaeni huko huko. mnajali mali za ccm kuliko maisha yaliyopotea. na rais wenu anakuja kuongelea suala la Arusha kwenye party aliyowaandalia mabalozi, mbona asiongee kabla ya hapo. Alikuwa anajishaua mbele ya mabalozi aonekane ni mwema wakati tunajua ni yeye ndo aliyeagiza haya kupitia mgongo wa iGP, shwaini.

    ReplyDelete
  25. Mwingine huyo anashindwa hoja anatukana,mimi sikutukani kwani nimefunzwa na wazazi wangu tabia njema na tabia ya kujadili kitu bila jazba,mimi ni mzaliwa wa Arusha,pengine wewe ni wakuja. Ndio maana nasema HAKI YAKO AU UHURU WAKO KIKATIBA ISIINGILIE AU KUVURUGA HAKI YA MTU MWINGINE na kama nilivyosema hapo juu ni kwamba maandamano yenu mnaoshabikia siasa yanakera kwa maana wanaoumia ni waliomo na wasiokuwemo,sasa huyo Mkenya uliyemtaja wewe ni mfuasi wa chadema? kuna hospital hapo mlikuwa mna wagonjwa ndani,je hawakuathirika na maandamano yenu? au watu wa kawaida wanaoishi karibu na maeneo yaliyotokea vurugu hawakuathirika na fujo hizo? ni biashara ngapi zilifungwa siku hiyo kutokana na kuogopa hayo yaliyo tokea? (TUKIO LA JAMBO LOLOTE HUSABABISHWA NA KITU) BADO NASISITIZA HAKI NA UHURU WAKO WA KIKATIBA USIINGILIE HAKI NA UHURU WA KIKATIBA WA MTU MWINGINE. Suala la ufisadi samahani sana sina muda wa kuimba nyimbo hiyo isiyokwisha kwani pengine hata wewe ni fisadi kwa maana ya ufisadi sio wa viongozi wa serikali tu ni hata walio nje ya serikali,au fungua kamusi au walionzisha msamiati huo wakupe tafsiri ya ufisadi,na hapa kwetu Arusha ndio kambi ya mafisadi na ndio walioingiza chadema madarakani hapa Arusha,au unataka nikutajie? au utajiri wa hao jamaa zako unaujua ulipatikana vipi? ni ufisadi mtupu,taswira ya ufisadi ni fisadi tu awe raia,kiongozi,mhindi,muafrika,mtanzania.

    ReplyDelete
  26. wewe ambaye umetoka kutoa comment zako,we ndo ngetwa kweli mafisadi wako ccm au chadema ulishasikia mafisadi wakitoka chadema wakati chadema ndo wamewaumbua mafisadi hata mkajua mafisadi ni akina nani/? tumia busara kuongea usiwe kama makamba. wewe unafanya kuishi arusha sisi ni wazawa, unajigamba unajua unajua nini. na huyo makamba wenu mwambie aache kutumia biblia haimhusu kamwe. kwanza ni mzee anapaswa kustaafu umri wake ni mkubwa sana aachie ngazi vijana wafanye kazi kwani akili yake imezeeka mno. na hao police ambao hawana elimu kichwani warudi shule kwanza wanapaswa kushtakiwa na msipowashitaki tutachukua hatua ya kuuwa mmoja baada ya mwingine labda wasije mitaani. wanafanya watu kama wanyama. isitoshe hawa wanaopigana kabla ya kupigwa hata vita hawataiweze ni vichupi tu avadhali hata ya mwanamke kuliko police wa tanzania. jeshi tunalo lakini si police waliotanguliza rushwa mbele. wakienda vitani watakufa wote.police wa arusha wanatakiwa wazalishwe watoto waingie labour kama watakaa waweze tena kupiga watu hovyo. wajinga wakubwa.

    ReplyDelete
  27. Minimi nadhani hapo 2ache ushabiki wa kisiasa kwani walokufanya ni watu,hivyo chakufanya ni utatuzi wa tatizo hasa kwa upande wangu huyu meya kama ameshinda kihalali na anaona kua kashinda kihalali basi akubali achaguzi urudiwe,iliufanyika kwa haki kwa ridhaa ya vyama vyote kama anakubalika anashinda tena kwani tatizo liko wapi?Jamani watanzania tuwe na hofu ya mungu hili ni tatizo uhasana huu hautaisha leo usipotatuliwa kwa busara na hekima kumbukeni kuna bima ya Afya lakini hakuna bima ya Uhai waliokufa ni watu na wameacha familia zao tumuogope mungu.

    ReplyDelete
  28. Jibu hoja usinizungumzie Makamba,ninayeandika ni mimi.NASEMA UHURU NA HAKI YAKO YA KIKATIBA ISIINGILIE HAKI NA UHURU WA WATU WENGINE FULL STOP. KUHUSU MAFISADI UNA AKILI MGANDO UKIWA NA MAWAZO YA KUWA FISADI NI KIONGOZI WA SERIKALI TU,NIMESHADEFINE FISADI NI MTU WA NAMNA GANI,KAMA HUNA UWEZO WA KUFIKIRI NA KUANDIKA KAA KIMYA

    ReplyDelete
  29. Acheni kutukanana someni hii.... Gazeti la Mwananchi 8/1/2010 "Maaskofu hao pia waliigeukia Chadema wakisema haiwezi kukwepa kuwa sehemu ya chanzo cha vurugu hizo kwa sababu ilikuwa na uwezo wa kuwazuia wafuasi wake kutoandamana ili kutii amri iliyotolewa na polisi.

    "Lakini pia Chadema walitakiwa kufanya kila jitihada kuwajulisha wafuasi wake kutoandamana licha ya kuzuiwa kufanya maandamano hayo muda mfupi kabla ya kuanza," alisema Askofu Lebulu.

    Kutokana na vurugu hizo, Maaskofu hao walisema Serikali inapaswa kushughulikia mgogoro wa Arusha kwa hekima, busara na uwazi kwani ni dhahiri kuwa taratibu za kumchagua Meya zilikiukwa.

    Askofu Lebulu pia alisema Serikali inapaswa kuchukua tukio la Arusha kama jambo la kitaifa na kufanya jitihada za kulishughulikia haraka na kwa amani.

    Naye, Askofu Thomas Laizer wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Arusha, alisema kutokana na polisi kutumia nguvu kubwa, hawatasitisha mahusiano yao na Serikali pamoja na polisi kwa sababu kufanya hivyo ni kujitenga na majukumu.

    "Ushirikiano wetu hauwezi kukatishwa na vurugu hizi kwani huwezi kutatua tatizo kwa kulikwepa," alisema Askofu Laizer.

    Katika kikao hicho, pia walihudhulia Askofu Martin Shao wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini, na maaskofu wa makanisa na Kipentekoste ya mkoani Arusha.

    (Mwanzoni nilistuka kwa kauli ya kutomtambua meya nikadhani sasa makanisa yanatuchagulia viongozi ikabidi ninunue gazeti na nikae kitako nilisome.. lakini Kwa kauli hii naungana na nyie Maaskofu maana kauli zingine zilimfanya Slaa na kundi lake kama malaika wasiotenda kosa,hata magazeti hayakuonyehsa uharibifu uliofanywa na mashabiki wa chadema kama vile hakuna maafa mengine zaidi ya waliyoyapata chadema.Meya wa Arusha cheo cha umeya hakina thamani zaidi ya maisha ya watu,chunga kauli zako)

    ReplyDelete
  30. Mimi nakiri kwamba wasema kweli kwamba "uhuru na haki yako ya kikatiba isiingilie (isidhuru) haki na uhuru wa watu wengine".Naam,mawazo murua. Lakini ile hoja niliyotoa kitambo, na mimi si huyu ambaye anatumia matusi, bado hujajibu : kwanini watu waliuliwa na polisi na wengine wengi wakajeruhiwa. Je, adhabu ya kifo na jeraha inastahiki kwa yule ambaye anafanya maandamano? Mali waweza kuzalisha upya,nyumba waweza kuijenga, lakini huwezi kuleta uhai kwa maiti. Nani atafidia maafa hayo.Hoja kwamba polisi hawawezi kuwakamata watu wengi na kupata ushahidi kwa sababu ni halaiki na pana ghasia- huo ni ukosefu wao polisi wenyewe. Lazima wajizatiti kukabili kila aina ya vurugu na ghasia.Tulishindwa huko lakini twaweza kuwauwa rais, huo ni udhuru wa kifisadi -samahani. Wako, Mwenda Pole

    ReplyDelete
  31. Kanisa na Maaskofu tunao uhuru wa kuchagua tunayemtaka. Kwa sasa tunapenda Chadema

    ReplyDelete
  32. Asante sana mwenda pole,tafadhali nielewe kuwa sisapoti mtu kuuawa kwa ajili ya imani yake iwe ya dini au ya siasa,ila ninachosema unapowaambia wafuasi wako wooote walioko kwenye mkutano wako waende kuwatoa viongozi wao na kitakachotokea huko yeye asilaumiwe kwa sababu ni uamuzi wa wananchi wenyewe,wewe unategemea nini kwenye reaction ya hao wafuasi kuwatoa viongozi wao kwa nguvu na polisi wakae wawaangalie tu. Ni kweli gharama ya maisha ya mtu yana thamani kama yalivyo maisha ya wale askari waliopewa jukumu la kulinda amani,na ukumbuke kuwa walioumia au kufa sio wafuasi wa chadema tu hata wengine pengine wasio na itikadi ya chama chochote wamepata madhara hayo,kuhusu fidia wanaostahili kulipa ni Slaa na kundi lake pamoja na serikali.

    ReplyDelete
  33. Polisi walikuwa wanashambulia kila mtu. Yule Mkenya alikuwa anapita zake tu. Wakampiga risasi ya tumbo.

    ReplyDelete
  34. Kuna mtu hapa anatoa comeents zake akijifanya ni mwelewa kuliko watanzania wote. Ndugu yangu unaesema Chadema wamefanyamaandano na kuingilia UHURU NA HAKI YA KIKATIBA KWA WATU WENGINE hayo ni mawazo yako kwa kujikomba kwa JK na serikali yake na Makamba wako, na Polisi wako.

    Unakumbuko mwaka jana Vijana wa CCM walifanya nini kule MOSHI mpaka wakaingia hospitali ya KCMS wagonjwa wakaanza kukimbia na madaktari wakajifungia ndani. Katika sakata hili hakuna polisi alieongea wala hakuna hatua zozote zilizo chukuliwa. Sasa ndugu yangu ni uhuru na haki gani unaoongelea wewe? Nyinyi mkifanya ni sawa. WATAFUTA HAKI WAKIFANYA NI KUINGILIA HAKI SASA HAKI YA MTANZANIA NI KUWAPIGA WAGONJWA MAHOSPITALINI NA WATU KAMA TUKIO LA JUZI. SASA HAWA WATU WANGEPITA WAPI KUELEKEA MKUTANONI. KWA SABABU WALIKUWA WANAPITA NJIANI NA NYIMBO ZAO MARA WANAVAMIWA.

    ReplyDelete
  35. Ndugu(maelezo ya tatu juu) naelewa vyema hoja zako. Pia nakushukuru kwa staha, kwa kujadili na kutathmini maafa haya kitaalamu na kiutu uzima.
    Nilieleza,nadhani juzi (sikutaja jina langu), kwamba pana ushahidi wa kutosha kwamba polisi ndiyo walianza mashambulizi.Pia kwamba mpaka sasa hawajafungua mashtaka dhidi ya waandamanaji kwa madai ya kushambulia kituo cha polisi n.k. Lakini tuache hayo kando. Ninapokosoa polisi nina sababu zangu mbali na nilizotaja awali. Polisi wenye umahiri hutumia mbinu nyingi. Mathalan, maadamu waliona waandamanaji ni wengi mno ,mbali na kuwa waandamanaji wamekiuka amri, kwa maslahi ya kiusalama - wange waacha waandamane (huku wakishika doria kikamilifu) na baadaye kuwashtaki viongozi n.k. Mbinu nyingine: wangesubiri mpaka mambo yatulie, pengine kesho yake napo kuwanasa wenye hatia. Kazi yoyote inahitaji akili na busara. Yote hayo yamo katika uwezo/uamuzi(discretion) wa polisi. Kwa mintarafu hayo, wahenga walisema - afadhali nusu shari kuliko shari kamili. Maadamu polisi walifanya mambo kimabavu matokeo ni majonzi kwako na kwangu; na matanga kwa waliofiwa(maskini pengine wengine walikuwa wapita njia tu na mmoja ni Mkenya - pengine aliandamana, sijui). Mwisho, nadhani makosa yalianza mapema ambapo mwanzo mandamano yalipewa kibali na baadaye kupigwa marufuku. Najaribu kusapoti haki wala sina ajenda nyingine, kama wewe tu. Wako, Mohamed-Mwenda Pole

    ReplyDelete
  36. Watu Pekee wanaounga mkono watu kuuawa ni wana CCM na ukiangalia wote wana MIRIJA midomoni mwao kwa kuwa wananufaika na CCM. Wakinyang'anywa mirija tu unasikia nao wamegeuka. Kwa ufupi JUA LIMESHAKUCHWA KWA CCM.

    ReplyDelete
  37. Asante bwana mohamed mwenda pole,makosa yako pande zote kama walivyosema maaskofu,tamko hili la maaskofu ni jema sana kwa mwenye akili timamu,na mwenye upendo na chama chake kwa kuona viongozi wake ni malaika,simzuii ni haki yake. Upande wangu nimeridhika na tamko la maaskofu kwa sababu hawakulalia upande mmoja,kwa maana hiyo hata upande uliokuwa unaona maaskofu wana wavictimize huenda wakaona sasa afadhali na wengine wameonekana makosa yao.

    ReplyDelete
  38. Kuna mtu hapo juu anasema kuna mtu anatoa (commeents zake) swangish mbovu na spelling mbofumbofu,si uandike kiswahili tu ndugu yangu. NAKUOMBA SANA SOMA KILICHOANDIKWA NA USIKURUPUKE KUTOA KICHWANI KWAKO,HAYO YOTE ULIYOANDIKA NI MADUDU MAANA MADA YANGU NA MOHAMED TUMEIJADILI KWA UFASAHA NA KUELEWEKA KWETU,SASA WEWE UMEZOEA FACEBOOK HIVYO SINA MUDA WA KUJADILI NA WEWE KITU MAANA HATA ULICHOANDIKA HAKIELEWEKI NIJIBU NINI.

    ReplyDelete
  39. TULIDHANI SERIKALINI YAKULINDA WATANZANIA, SASA IMEWAGEUKIA NA KUWAUWA TENA KWA KUKUSUDIA, JAMANI SERIKALI ACHENI MAUWAJI BILA HURUMA, KUMBUKENI MNAO WAUWA NI BINADAM KAMA NINYI NA NDIYO WLIYOWAPA KURA, SASA MMEAMUA KUAMRISHA JESHI KUUWA WATANZANIA? KIKWETE HUONI HATA HURUMA TENA? AIBU KUBWA KWA TAIFA. POLENI WAFIWA NA WANACHADEMA MLIOJERUHIWA. CHADEMA ENDELEENI KUPIGANIA HAKI ZA WATANZANIA WANYONGE, NANYI WA VYAMA VINGINE VYA UPINZANI UNGANENI NA CHADEMA KUTAFUTA HAKI ZA WATANZANIA WANYONGE KWANI LEO CCM IMEWAUWA CHADEMA KWARISASI HUENDA KESHO LITAWAUWA WAFUASI WA NCCR AU CUF NK

    ReplyDelete
  40. HII VITA YA WAFANYABIASHARA NDANI YA CCM NA WAFANYABIASHARA WA CHADEMA WA KICHAGA WALIOMZUNGUKA SLAA,MTAUANA BURE,HAO WANAGOMBEA HAZINA YA NCHI IWE MIKONONI MWAO. OLE WENU

    ReplyDelete
  41. WANASIASA WAJINGA WANAWATUMIA WANACHI WAJINGA KWA MASLAHI YAO. Wanajua kabisa serikali imekataa nini wao wanawahamasisha raia waingie kwenye mgogoro wasiouweza.

    WATZ wenzangu basi na tusikubali kuwa madaraja ya WANASIASA wasiopenda tuwe na amani. Wanaotutakia VILEMA. Laiti kama Slaa angelikuwa anasema ukweli kwamba anajali maisha ya Watanzania basi na ANGELIWALINDA kwa kutohamasisha maandamano ya Arusha.

    ReplyDelete
  42. Mhariri jukwaa lako hili ni safi sana maana ukimaliza kuandika unaona imekuwa posted,usikubali maoni ya wale wanaotaka uchakachue maoni,kwa sababu yule anayechagua maoni yapi yaandikwe na yapi yasiandikwe anakuwa naye ana lake,hivyo hupendelea,kama gazeti la Mwananchi lilivyo,ukiiandika vibaya chadema basi maoni yako hayatoki ndio maana tumengangana na gazeti lako huru na ni kweli huru.KEEP IT TUBANANE HAPAHAPA

    ReplyDelete