Na Grace Michael
MBUNGE wa Jimbo la Tarime, Bw. Nyambari Nyangwine (CCM), amesema hatavumilia kuona mikataba ya wawekezaji ambayo wameingia na wananchi katika masuala ya huduma za kijamii ikiwa haina maslahi kwa
wananchi wa jimbo lake.
Kutokana na hali hiyo, ameitisha mikataba yote ya wawekezaji wa mgodi wa Nyamongo ili aweze kuiangalia na kuona kama ina maslahi kwa wananchi katika huduma walizokubaliana.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Bw. Nyangwine alisema kuwa katika uongozi wake angependa kuacha alama ambazo atabaki akikumbukwa ikiwa ni pamoja na kuifanya Tarime kuwa ya mfano katika maendeleo lakini pia kuondokana na migogoro na mapigano ambayo yamedumu kwa kipindi kirefu.
"Niseme tu kwamba nisingependa kuona wananchi wa Tarime wakinyanyasika katika haki zao...nimeamua kuitisha mikataba waliyokubaliana na mgodi wa Nyamongo ili nione kama una maslahi kwa wananchi wa jimbo langu...nataka ifike mahali kila mtu achangie pato kutokana na nafasi aliyonayo ili hatimaye jimbo letu liwe na maendeleo makubwa," alisema Bw. Nyangwine.
Alisema kuwa awali Tarime ilizoeleka katika mtazamo hasi, na sasa hali hiyo haipo tena kutokana na wananchi wake kujitambua na kuachana na mambo ambayo yalikuwa yakifanyika kama ya mapigano ya baadhi ya koo.
Katika kuhakikisha anaifanya Tarime kuwa ya mfano, alisema kuwa patajengwa Chuo cha VETA ambacho kitawasaidia vijana wengi kuweza kupata elimu ya kujiajiri wenyewe hivyo kuachana na vitendo vingine ambavyo havikubaliki ndani ya jamii.
Akizungumzia changamoto zilizoko jimboni kwake alizitaja ni pamoja na maji kero ambayo alisema iko ndani ya mikakati ya kushughulikiwa na hatimaye wananchi waweze kupata huduma hiyo bila matatizo.
Alitoa mwito kwa wana Tarime wote kuhakikisha kila mmoja anajiuliza anaifanyia nini Tarime na sio kushiriki kuchochea migogoro ya kisiasa na mingine.
SAWA ANGALIA NA SUALA LA WANAFUNZI AMBAO WAKO SHULENI LAKINI BARICK WAMESITISHA KUWALIPIA KARO,HIYO NAYO NI KERO PAMOJA NA WOTE WANAOCHAKACHUA FEDHA HIZO ZA MUHISANI ZA KARO,KWA HILI NIMEKUPA KAMA CHANGAMOTO KWANI NA WEWE UMEINGIA KWA KUCHAKACHUA SIJUI KAMA UTAFUATILIA KAZI KWAKO KWA SABABU KAZI UMEINUNUA KWA GHARAMA KUBWA
ReplyDelete