20 January 2011

Nitaendelea kupinga malipo Dowans-Sitta

*Ataka wananchi wasifikiri amebadili msimamo

Na Mwandishi Wetu

SIKU moja baada ya vyombo vya habari kuripoti kuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Samwel Sitta amefungwa mdomo na
Baraza la Mawaziri ili aache kuzungumzia suala la Dowans, ameibuka na kusema hawezi kufungwa mdomo kupinga malipo ya sh bilioni 94 kwa kampuni ya kitapeli.

"Naomba wananchi wafahamu kuwa siwezi kufungwa mdomo kupinga malipo kwa kampuni ya kitapeli ya Dowans," alisema Bw. Sitta  alipozungumza na baadhi ya vyombo vya bahari Dar es Salaam jana.

Kulingana na taarifa za gazeti moja jana, Bw. Sitta pamoja na Naibu Waziri wa Ujenzi, Dkt. Harrison Mwakyembe wamebanwa katika kikao cha Baraza la Mawaziri na kutakiwa wasizungumzie tena suala hilo hadharani 'ili waache mipango ya serikali iende kama ilivyopangwa'.

Bw. Sitta ambaye alikuwa Spika wa Bunge la Tisa wakati mjadala wa Mkataba wa kampuni ya feki ya Richmond na baadaye Dowans unatikisa nchi, alisema hajawahi kutishwa wala kufungwa mdomo kuhusu msimamo wake.

"Sijawahi kuitwa popote wala na mtu yeyote na kuambiwa nisizungumze suala hilo, nitaendelea kupinga malipo ya Dowans. Hivyo wananchi wasifikiri nimebadili msimamo.

"Taarifa zinazosambaa ni za kupikwa tu, zisije zikawapotosha wananchi wakadhani nimewasaliti katika hili, narudia tena sijafungwa mdomo," alisisitiza Bw. Sitta ambaye pia ni mbunge wa Urambo Mashariki.

Mbunge huyo ambaye alitemwa asigombee uspika kwa mara ya pili na Kamati Kuu ya CCM kwa kilichodaiwa kuzingatia suala la jinsia, alifafanua kwamba sauti yake haitasikika tu kwa suala la Dowans pakee, bali ataendelea kupinga mambo yote machafu nchini.

"Nchi inahitaji viongozi wenye kusimamia vema maslahi ya taifa bila hofu ili kulinda haki za wananchi na kuboresha maisha yao, alisema Bw. Sitta.

Akizungumzia madai ya kukiuka kiapo cha uwajibakaji wa pamoja, Waziri huyo alisema kama dhana hiyo ingekuwa inaheshimika uamuzi wa kuilipa au kutoilipa Dowans ungefanywa kwa pamoja, badala ya kutangazwa tu na Waziri wa Nishati na Madini.

Alisema haiwezekani dhana ya uwajibikaji wa pamoja ifanyike bila kushirikisha wengine halafu mwisho itolewe taarifa ya uwajibakaji wa pamoja.

"Halafu kuna watu wanazungumzia nimekiuka dhana ya uwajibikaji wa pamoja, uwajibikaji wa pamoja ni lazima uamuzi ushirikishe wengine si mmoja kuamua halafu ifahamike ni uwajibakaji wa pamoja," alisema.

Kiongozi huyo alisisitiza madai yake dhidi ya uharaka wa kulipa tuzo ya Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Kiabiashara (ICC) kuwa unatia mashaka."Hii haraka ya kuilipa Dowans ni ya nini? Nchi hii ina madeni ya muda mrefu kama yale ya Benki ya Dunia na IMF lakini hakuna uharaka wa kulipa kama huu, sasa kasi hii inatoka wapi?" alihoji.

Kauli hiyo ya Bw. Sitta imekuja ikiwa ni siku moja baada ya Hukumu ya Dowans kudaiwa kuwasilishwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania kwa ajili ya usajili ili taratibu za malipo zianze, huku wanaharakati wa haki za binadamu, wakiongozwa na Kituo cha Sheria na Utawala Bora (LHRC) wakiwa wameshatangaza nia yao ya kufungua kesi kupinga malipo hayo.

Habari zilizotufikia wakati tunakwenda mitamboni zimesema kuwa Waziri Sitta na Dkt. Mwakyembe kwa pamoja wamewasilisha nia ya kulishtaki gazeti moja la kila siku ambalo liliripoti taarifa za kunyamazishwa kwa viongozi hao, wakidai kuwa ni za uongo.

Katika barua yao kwa Mhariri Mtendaji wa gazeti hilo, mawaziri hao walisema: "Tunakuandikia barua hii upime mwenyewe utuombe radhi kwa uongo huo uliotutungia ukurasa wa mbele wa gazeti lako au usubiri tukuburuze mahakamani kukukumbusha kuwa Tanzania si "Banana Republic" bali ni nchi yenye kuheshimu utawala wa sheria.

31 comments:

  1. Naomba kumsahihisha mwandishi wa habari hizi kituo(LHRC)kinachotarajia kuwasilisha pingamizi mahakamani haitwi "kituo cha haki za binadamu na utawala bora" kinaitwa "kituo cha sheria na haki za binadamu"

    ReplyDelete
  2. JAMANI RICHMOND,RICHMOND,RICHMOND TUMECHOKA WANAOTAKA PESA ZISILIPWE WAONYESHE NJIA MAANA HILI NI SUALA LA KISHERIA,HAKIMU HAWEZI KUKUHUKUMU KULIPA DENI USEME TU SILIPA,ZIPO TARATIBU ZAKE AMA KUKATA RUFAA AU ULIPE ACHENI SIASA KWENYE MAMBO YA MSINGI. UNAPOSEMA DENI HILO TUSILIPE ONYESHA NJIA TUFANYEJE? MAANA NI AMRI YA MAHAKAMA. ITAFIKA MAHALI HATA MTU AKINYA KAMA KUNA UWEZEKANO WA KUJIPATIA UMAARUFU BASI NDIO HAPOHAPO.

    ReplyDelete
  3. Hilo gazeti lililoandika habari kuhusu kufungwa mdomo Sitta na Mwakyembe ni Tanzania Daima la tarehe 19.01.2011 katika ukurasa wake wa mbele kabisa. Ni kweli waliandika na hata wao wenyewe Tanzania Daima leo wameripoti Luhanjo kuikana taarifa hii. Tusizunguke sana kwani gazeti hilo lilisomwa na wananchi wengi. Sasa hili gazeti lilipata wapi habari hizi? Mbona mimi ni mmoja wa wananchi wanaoliamini na kuwaheshimu waandishi wake wa habari pamoja na uongozi mzima wa gazeti hilo kuanzia Managing Director Bwana Absalom Kibanda pamoja na Deputy Managing Director - mwandishi nguli wa makala ya Maswali Magumu - Bwana Ansbert Ngurumo? Niliamini ni viongozi makini, lakini kwa hili wametetereka. labda walitolee kauli. Na hii ni mara ya pili kwa shutuma kuliendea gazeti hili baada ya ile ya waziri Ngeleja akilishutuma kuwa walimbambika maneno asiyoyasema.

    Mhariri Mkuu na Makamu wako, turudisheni kwenye mstari wa imani na gazeti lenu ili tuendelee kuliamini na kulisoma. Kuomba radhi pale mtu alipotetereka ni kitendo cha kuungwana sana.

    Kila la heri!

    ReplyDelete
  4. Sitta kutafuta umaarufu kutalifikisha taifa pabaya. Ni wabunge wakiongozwa na Sitta walipelekea kuvunja mkataba, na sasa Sitta anasema tusilipe, lakini haongelei consequences za kutolipa. Ndiyo, tusilipe halafu nini? Sitta inatia kinyaa jinsi unavyokosoa serikali adharani. Hivi nyie mawaziri hamna ofisi zenu mkaongea hayo mambo yenu badala ya kuyapeleka kwa waandishi wa habri mkapingana. Serikali inayopingana hadharani haileti maslahi kwa taifa. Sitta kama kutokana na nafsi yake anaona anatofautiana sana na mawaziri wenzie na hawezi kujadiliana nao badala yake anachukuwa nafasi ya kuwapinga hadharani ni afadhali akaachia ngazi. Mawazari wapo kwa kumsaidia rais na serikali yake, kupingana kwao adharani kunaweza kuharibu amani ya nchi. Sitta ataitendea nchi hii mema akiamia upinzani (wanamhitaji) kuliko kuendelea kuleta mvurugano katika serikali. Inatisha kusikia mawaziri wakipingana. Kuna watu watamuona Sitta ni shujaa, mimi namuona ni mtu wa hatari kwa umoja wa taifa letu.

    ReplyDelete
  5. Huyu aliyetoa maoni hapo juu ni kibaraka wa wakina Rostam na wenzake wa kampuni hii fex ya Dowan. Hivi huyu kweli haelewi kwamba Dowan ni mchezo mchafu wa watu wale wale wa Richmond? Kila mtanzania hata wa asiyeenda shule lakini anafuatilia anajua kabisa mchezo mchafu unaofanyika hapa. Sasa hebu fikiria shahidi wa Tanesco anayekwenda kwenye hii kesi ni Idrisa Rashid, yaani kesi ya panya unampelekea paka kweli! ajabu. Lazima tuseme ukweli kwamba hii ni Dowason ni ya wakina Rostam na wenzake watatu na wanajulikana tatizo ni uoga wa watu kujitokeza na kusema. Dili imesukwa kupitia makaratasi ya mkataba. Halafu huyu ndugu yangu wa hapo juu anasema kwamba Sitta hasemi tukikataa kitakachotokea. Sasa mimi nimjibu huyu ndugu kwa niaba ya Sitta ni kwamba halitatokea lolote. Sisi tulioko huku nje mataifa mbalimbali yanatushangaa ufisadi unaofanywa na baadhi ya watanzania wenzetu wakitumia wageni ili kuexploit maskini watanzania. Ili wasipate social services zao zinazowasitahili. Sasa unadhani hao wahisani watafurahi matapeli wachache wafaidi hayo malipo? Zaidi ya yote kutetea uhuru wetu ni jambo la mhimu sana kuliko kufanya watumwa ndani ya nchi yetu kwa kigezo cha kulinda misaada ya wahisani. Sitta anaitetea nchi yake. Nchi inahitaji watu jasiri wachache sana ili waibadilishe. Mabadiliko kote duniani hayakufanywa na kundi kubwa isipokuwa mtu mmoja tu alijitoa akaleta mabadiliko. Sitta hatafuti umaarufu kama unavyofikiri ila anasimamia lile analoliamini kwenye nafsi yake. Wewe nawe hapo juu unaweza kuendelea kuwaamini hao wahindi wakina Rostam kwa kuwa unapata misaada kidogo ya kukufunga midomo nawe ujitoe kuwatetea.

    Mungu ibariki Africa, Mungu ibariki Tanzania na watu wake

    ReplyDelete
  6. Hivi wewe uliyeandika hapo juu una akili timamu? mtu akitoa mawazo yake ni kibaraka,nadhani una kasoro au hujui kusoma kitu na kukijadili.Huyo bwana kajenga hoja kwa kuwa Sitta anasema tusilipe hilo deni aonyeshe njia ya kutolipa maana hukumu imetolewa na mahakama ambayo hata Tanzania ilinufaika nao ilipovunja mkataka wa ile kampuni ya CITY WATER iliyokuwa imepewa tenda badala ya DAWASCO,hili ni suala la kisheria na unapokataa lazima utoe hoja za kisheria,huko sio mahakama zetu Bwana wenu Slaa kachukua mke wa mtu na bado anatesa naye na vyombo vya dola vinamuangalia tu,huko kuna watu wenye taaluma iliyobobea kisheria,hawaamui kwa kumuangalia mtu usoni,lazima uwe na hoja ya kimsingi ya kisheria,sasa Mheshimiwa Sitta anatakiwa aonyeshe njia na mahakama ziko wazi kusikiliza hoja za kisheria na si za mitaani za kutafutia umaarufu kwa wasiojua sheria.hivyo usimuite mwenzio kibaraka kwani hoja aliyotoa ni nzuri na pengine hata huyo Rostam hamjui,pia usizungumzie wahindi kwani SABODO ni mhindi na Bwana wenu Slaa na Mbowe wamepokea pesa kutka kwake..SITTA TUONYESHE NJI AU NENDA MAHAKAMANI KUPINGA MAANA SISI WOTE TUNATAKA PESA ZISILIPWE LAKINI HUWEZI TU KUSEMA SILIPI.

    ReplyDelete
  7. Bwana wewe umebadili mjadala kuwa matusi, hivi wewe ni mtanzania kweli? Napata wasiwasi kuwa tukifuatilia chimbuko lako utakuwa kama sio Muhindi basi ni mwarabu au wewe ni ndugu yake Bagbo wa Ivory Cost? wewe kama ni mtanzania huwezi kutoa maoni ya kipuuzi kiasi hicho. Unajua maisha ya watu waliopo kule Mlandizi Kibaha au waliopo Singida Vijijini? acha upuuzi wahurumie watanzania wenzako kwa kukataa malipo ya Dowans ili hiyo pesa iwapelekeee hata Vijumba vya tope kuliko wanavyoishi kwenye makuti. Au kwa sababu wewe uko mjini unaelewa kutumia Computer? Tena ikiwezekana hata hiyo Computer umejifunza kifisadi, ndio maana haujui hata umuhimu wa kuitumia, huwezi kuwa na sifa ya kutumia afu unafanya mambo ya hivyo unaiaibisha kwani naona inakuzidi hata akili uwe na Timamu kichwani kwako siku moja moja.

    ReplyDelete
  8. Sitta endelea kukomaa nasi watanzania wenzio tupo pamoja katika kuitetea nchi yetu usiyumbishwe na watu wachache wasiokuwa na fikra msingi za nchi yao kama sisi watu wa upinzani sahihi tunapoona mtu amefanya jambo la maana hata kama ni wa ccm tunampongeza, ndio uzalendo huo, sio kushadadia tu mambo kwa kuogopa eti watachukia. Kwani wao ni kina nani katika taifa hili la Mungu?

    ReplyDelete
  9. Msimamo wa Mzee wetu Samuel Sitta kama siyo wa kuchochewa na Wanahabari unapaswa kuigwa na wapenda amani na wenye uchungu wa Tanzania yetu ambayo kila kukicha inaendelea kuchakachuliwa tu. Hongera Mzee wetu Sitta, Kaza buti na simamia kile unachokiamini kuwa ni kwa maslahi ya nchi na siyo maslahi ya wachache wenye nia na lengo la kuuchakachua uchumi wetu ambao tayari unayumba. Wale wanaosema kesi ya Dowans hatuwezi kuishinda akiwemo ndugu yetu aliyetajwa kama wakili maarufu Bwana Kennedy Fungamtama kwenye gazeti moja la kila siku kuwa “Dowans itadhohofisha nchi” , binafsi nimevutiwa sana na maelezo yake kiasi kwamba nimelazimika nikumegeeni kidogo yahusuyo sheria ambayo kwa waraka wa mwanasheria maarufu imeonekana amesahau ama amelazimika kuacha makusudi kwa nia ya kuficha ukweli wa mambo.
    Hivi ni kweli kwamba shauri likiisha katika mahakama yoyete haliwezi kurudiwa kuzungumzwa? jibu ni hapana. Kuna ‘REVIEW, REVISION REFERENCE, WACHA APPEAL’, hilo moja lakini kisheria katika hilo hilo moja ni hivi na hii ni kwa mujibu wa sheria no. 15 ya mwaka 2002 tena sheria ya Tanzania sheria ya namna ya kuamua mashauri kwa njia ya suluhu yaani nje ya mtindo wa kawaida unaofahamika.
    Kwamba shauri linalopitia njia ya usuluhishi linatakiwa liheshimiwe na linakuwa na nguvu za kisheria sawa na mashauri mengine yoyete yaliyopitia mfumo wa kawaida wa kisheria ispokuwa pale ambapo moja, pataonekana kuwa mwamuzi hakufuata taratibu za kisheria, lakini pia endapo pataonekana kuwa hukumu yenyewe ilipatikana isivyo kwamba palikuwa na usahaulifu wa kifungu fulani cha sheria na au ushahidi muhimu uliachwa au haukuzingatiwa ( if the judgment was obtained or decided by per incuriam) angalia shauri la Zambia Tanzania Road Service Ltd (TAZARA). v J.K. Pallangyo Civil Appeal No. 9 of 1982,.
    Lakini pia hapa hata shauri lenyewe lazima liwe lina msingi wa haki na lizingatie mkataba wa kweli ulioingiwa kwa uhuru na utaratibu uliowekwa na sheria zilizopo za nchi husika ambayo pia inajali na kukubaliana na sheria za kimataifa.
    Unajua, katika sheria hatuangalii tu kifungu fulani eti kinasemaje lakini pia tunafungua milango mingine (to open the Pandora Box OR PAN + ndorom) na kujiuliza kwamba kwa mashauri kama haya na labda endapo yalishawahi kufanyika penginepo na kama ndio basi tuna wajibu wa kufuata pia hapa nina maana kuwa kama paliwahi kutokea mashauri yahusuyo mkataba wa kitapeli (void contract and yet either of the parties successfully enforced a right or derived a right as from that ennuity) na maamuzi hayo eti sasa yafae kufuatwa tukizingatia kuwa shauri hili linafanana kwa kila hali, hakika dunia itakuwa imefika maendeleo ambayo yanafahamika kwa wakili huyu peke yake.
    Lakini cha msingi sana hapa na ambacho watu wote wanapaswa kuelewa ni hiki ambacho ni cha kisheria na ambacho pia huyu mwanasheria maarufu anapaswa kukifuata. Kwamba huwezi kutafuta haki kutoka kwenye batili (you can not Deriver a Right from Ennulity ). Huu ndio msingi mkuu wa mkataba wowote duniani. Nini maana ya hii, maana ya hii ni kuepusha aina zozote za kitapeli ambazo zingeweza kujitokeza kwa njia yoyote ile. Mkataba na Richmond kampuni mama ya Dowans MKATABA WAKE NA TANESCO ULIKUWA BATILI kwa vile ulionekana kuwa ni wa kitapeli na hili lilitamkwa na bunge Tukufu la Tanzania.
    Kwa upande mwingine sishangai sana kwa Mtanzania kusema haya huenda ndio wale wachakachuaji wa mambo.
    Lakini waelewe kuwa fedha hizi ni Kodi ya watanzania wanaoshi chini ya kiwango cha Dola moja kwa siku. Upeo wa kuelewa wa Mzee Sitta sote tunaufahamu na jinsi alivyochakachuliwa ili asiwe Spika tunaelewa sasa wanapotokeza wanajiita Wanasheria Maarufu na kutupotosha tusikubali. Ombi langu ni hili, Tanzania ina bahati ya kuwa na Wanasheria wenye upana wa mawazo na busara ya kufanya mambo tunaomba wajitokeze na watueleze wapi tumekosea na nini kifanyike ili kuinusuru nchi kulipa kampuni ya kitapeli mapesa yote hayo ambayo ni jasho la wanachi. Inawezekana tunaendeshwa na watu wawili ama watatu kwa faida yao. Tuwe macho sasa.

    ReplyDelete
  10. jamani wote tunataka maendeleo ya nchi yetu matusi sio dawa,cha msingi kama tumeshahukumiwa kulipa, yapo mambo 2. au tulipe kama tulivyohukumiwa au tukate rufaa ya kupinga hukumu hiyo na sio kurumbana sisi wenyewe wakati hukumuipo palepale tunawaomba wataalam wa sheria waangalie kipi kinachotufaa kwa maslai ya taifa letu

    ReplyDelete
  11. Inawezekana Bwana Sita kakosea kwa mujibu wa kanuni za utawala,lakini je, kufuata kanuni kunasaidia nini ikiwa mwisho wa mchezo tunaumia? Hivi ni kweli tukilipa deni lililopatikana kwa njia haramu tunakuwa wastaarabu zaidi? Mbona wanaotaka tulipe hawasemi chochote kwa waliohusika na kadhia hii?Hata kama ni Sita au Bunge liwajibike japo binafsi siamini kama Bunge lilikosea kwani tume iliwasilisha ushahidi wa utapeli wa mkataba mzima.Iweje tapeli ampasie mpira mwingine na huyo asiwe pia tapeli? Si inajulikana kuwa 'ndege wa rangi moja huruka pamoja'?

    ReplyDelete
  12. Wakitajwa wahusika wa kweli katika sakata hilo ndio itakuwa faraja kwa watanzania kwani watajua anayelipwa ni nani na sababu za kumlipa ni zipi. Lakini wahusika wa kufanikisha malipo haya ni hawa mimi niwaseme japo wanisamehe kwa kusema ukweli : Mh. Kikwete, Rostam, Lowasa, Nazir Kalamagi, William Ngeleja, pia wahusika ni pamoja na Dr Idriss Rashid hapo hatujawataja wote, na ndio sababu Ngeleja karudishwa katika nafasi yake ile ile na wizara ileile ni ili kufanikisha malipo hayo kwa urahisi kwani walijua katika hiyo kesi kitakachokuja kutokea ni nini hivyo waliisha anza maandalizi mapema na ndio sababu ya kuchakachua hata matokeo ya uchaguzi mkuu uliopita ili wakamilishe dili lao. wawe na huruma kwani sote ni watanzania na mimi nawahurumia sana watu walioko vijijini kwani wanamaisha magumu sana yeyote ambaye hajaenda vijijini aende sasa akaone hali ilivyo. Mtu asiende vijiji vyenye umeme au mfano ni kama kule Mlandizi Pwani njia ya kuelekea bagamoyo. kuna watu wanaishi kama hawako Tanzania wakati ndiko anatoka kikwete na Mh. Shukuru Kawambwa, afu sogea pale Singida kuna baadhi ya vijiji hata watu wamebadilika rangi yao halisi na kuwa nyekundu kama vijumba vyao maarufu kama Biskuti ajabu wachache wanafurahia maisha utadhani kina Hayati Mwl. Nyerere na Mzee Kawawa na wengineo waliohangaikia uhuru walikuwa wanawatafutia wapo. Inasikitisha sana wajaribu kubadilika na kuwa hata na chembe ya huruma. Na ili muamini kuwa malipo hayo ni feki ni jinsi kiwango cha kulipa kinavyopungua kutoka 185. Bilioni hadi sasa tunapotaarifiwa ni 95. Bilioni, je wamekaa na wamiliki wa hiyo Dowans wakaomba kupunguziwa ghalama za malipo? waache uhuni kwani watanzania wa sasa sio wale wa Enzi za Mwl. waliokuwa wakikubali kila kitu japo kwa wakati ule walikuwa na Kiongozi mwenye busara na mwaminifu, na ndiyo sababu walimuamini na kumkubalia kwa kila japo kwani waliamini anatenda mambo sahihi na mema kwao. It's enough and i dislike this issue i hear all day about this Dowans what Dowans Bwana.

    ReplyDelete
  13. Mh! hii habari imeangukia mikononi mwa ma-academicians, ma-laymen, ma-idiots na wafuata upepo! basi imekuwa kazi kweli kweli!

    ReplyDelete
  14. Ushahidi mazingira ya kampuni feki za richmond na dowans SITTA anazifahamu kwa hiyo wewe unayemlaumu nakushangaa, yeye ndiye aliyekuwa spika kapitia vifungu vyote vya mikataba ya hiyo kampuni na kuunda kamati iliyogundua richmond ni kampuni feki hata waziri mkuu alikiri dowans ni kampuni feki ya watanzania wachache wanaofilisi nchi ila akasema no way watalipwa hana uwezo wa kuzuia hapo ndipo unapopata majibu kumbe ni watu wakubwa sana hapo serikalin Mwaikembe na SItta ndio wapo mstari wa mbele kwa sababu ndio waliofuatilia hilo suala wanalijua vizuri na wao ndio inawezekana walishinikiza kuvunjwwa kwa mkataba we kampin haikusajiliwa ndio inataka kusajiliwa sahizi Tumunge mkono ana akili timamu anjua anachokisema na amaanisha.

    ReplyDelete
  15. Namshukuru Mungu kwa kunipa nafasi na uhai kuweza kuyashuhudia haya, Jambo la msingi tuwe wastaarabu katika kutoa maoni yetu na wala tusitumia lugha za matusi kwani hayasaidii kujenga ama kuepukana na hasara inayokwena kulikumba Taifa. Ni suala la msingi kama jambo hili litachukuliwa na kuwasilishwa kwa vyombo husika hasa Bunge an wataalamu wa kutafsiri sheria watusaidie kwa hili ili Taifa lisiingie kwenye hasara itakayokwenda kugharimu hata Vizazi vijavyo. ukizingatia kwamba kuna watoto wanaozaliwa leo na hawajui kama kuna kitu kinaitwa Dowans na kimeligharimu Taifa mabilioni ya pesa.Ningependa kuwaomba viongozi wetu wapendwa wliopewa jukumu la kuliongoza Taifa hili na Mwenyezi Mungu Kusimamia Haki katika
    kila Jambo lisilo sawa na linalopindishwa walinyooshe maana dhamana hii wamepewa na Mungu na siku moja watatoa Hesabu. Naomba tusitumie Lugha chafu za Matusi kwani hazijengi bali huchefua...

    ReplyDelete
  16. MR SITTA, MIMI NAPATA KIGUGUMIZI KUKUITA MHESHIMIWA!!! HUWENDA SALUTE INAYOKUFAA SANA NI MCHONGANISHI SAMWELI SITTA !!!
    MCHONGANISHI SITTA UNAPOZUNGUMZA NA VYOMBO VYA HABARI UNAONEKANA UNA HASIRA KKKALI SANA ZINAZOTOKANA NA KUUKOSA USPIKA ILIYOKUPELEKEA KUSHINDWA KUTEKELEZA MIPANGO YAKO YA KUMSUMBUA NA KUMKOSESHA RAHA RAISI WETU KIKWETE KUPITIA BUNGE!!! ULIKUA NA MIPANGO MINGI SANA KWA KUSHIRIKIANA NA CHAMA CHAKO TARAJALI(CHADEMA) KWA MAANA KWAMBA UNASUBIRI UFUKUZWE UWAZIRI NA CHADEMA LIWE KIMBILIO LAKO NA LENGO LAKO NI KUZIDI KUKIPA UMAARUFU!!!MATEGEMEO YAKO YAKIWA NI KUSHIRIKIANA NA KANISA KATOLIKI KUSHINDA UCHAGUZI WA 2015!!!!
    TUKIRUDI KWENYE MADA, ISSUE YA DOWAN ILIJADILIWA KWENYE BUNGE LILILOPITA NA HOJA ZIKATOLEWA JUU YA ATHARI ZITAKAZOTOKANA NA KUVUNJA MKATABA BILA KUFUATA TARATIBU, SITA AKASIMAMIA BUNGE HADI MKATABA UKAVUNJWA BILA KUFUATA TARATIBU ZA KISHERIA, HAPA TUNAPATA PICHA KWAMBA MCHONGANISHI SITTA ALIJUA DOWANCE WATAENDA MAHAKAMANI NA WATASHINDA KESI, NA SERIKALI ITATAKIWA KUILIPA DOWANS! KWA KUDHANI KWAMBA ATAENDELEA KUWA SPIKA ATAHAKIKISHA KWAMBA ATATUMIA BUNGE KUZUIA MALIPO!! MATOKEO YAKE NI KUZIDI KUVURUGA SERIKALI IONEKANE HAIFUATI SHERIA ZA KIMATAIFA!!
    USHAURI WANGU KWA HUYU KIDUDU MTU SITA:
    KWA KUWA UMESHAONA HUWEZI KUFANYA KAZI NA SERIKALI FISADI, ONDOKA!!!
    PIA KWAKUA PALE URAMBO UMEPATA UBUNGE KUTOKANA NA SIFA YAKO KUU YA KUPINGA UFISADI BILA KUMUOGOPA MTU, ONDOKA KWENYE CHAMA CHA MAFISADI UGOMBEE KUPITIA CHAMA CHA WAPAMBANAJI WENZAKO!! ILA NAKUHAKIKISHIA HUTAPATA KURA 100!!!

    ReplyDelete
  17. Pamoja sna Mh.Sitta we ndiye unayejua kila kitu kuhusu Dowans na Richmond, tunaomba ufuatilie kwa umakini hizo fedha zisilipwe wasiwafunge midom hao makchaa wa CCM, watanznania tunapenda sana kuona viongozi mnaopenda kukutetea maslahi ya nchi yenu kama Mh Sitta na Mwakyemb nawapa Big up sna, msiogope kuenguliwa madarakani.

    Anynmous wa 4 kweli umechemsha huwa wanakupatia ulaji ni au ndio wale vibaraka fuata upepo.

    Japokuwa nipo chadema nampenda sn Huyu Mh. Sitta yupo tofauti na wenzako, usitungushe Mh tunategemea support kwako.

    ReplyDelete
  18. DENI HALIFUNGI hii metali imepitwa na wakati? kwa nini tulipe tusichokuwa nacho? au ninyi mna hela? tz kwa porojo mmezidi . kwani hata hela hizo zikilipwa au zimelipwa mtajua ! sitta hela zimelipwa au bado? MBADO um um!er er this iz very WONDERABLE and FANTASTIC! watu husema usile na kipofu ukamgusa mkono ni kweli? watz wamelimika lakini elimu kama huwezi kuiweka katikaa vitendo hiyo siyo elimu TUigeni TUNISIA

    ReplyDelete
  19. hongera sana mchangiaji unaemwita bwana SITA mchonganishi, kidudumtu nk, watanzania tunatakiwa kuwaelewa hawa wanasiasa, mwaka 2015 atagombea URAISI mwanachama tofauti na kikwete kupitia chama chenye mtandao mkubwa sana nchini (C.C.M) na ambae kwa mategemeo ya wengi ndiye atakaekua RAIS wetu!! mheshimiwa sita anachofanya ni kujaribu kutafuta umaarufu na kujipendekeza kwa wananchi kwa gharama yoyote ili ikifika wakati huo ionekane ndani ya C.C.M mwanachama anaependwa sana na wananchi ni Samweli SITTA, c.c.m kwa vyovyote wampitishe yeye au anaeungwa mkono na mheshimiwa SITTA!!
    Mheshimiwa sitta usituvuruge, tunakujua ulivyo mlafi wa madaraka na pesa, ulitumia bilion mbili kujitibu, na zaidi ya bilioni tatu kujenga ofisi ya SPIKA URAMBO!!! ACHA UNAAFIKI, Utaliangamiza taifa kwa tamaa zako!!!

    ReplyDelete
  20. "Lakini, hii haraka ya kuilipa Dowans ni ya nini? Nchi hii ina madeni ya muda mrefu kama yale ya Benki ya Dunia na IMF, lakini hakuna uharaka wa kulipa kama huu sasa kasi hii inatoka wapi?" alihoji. haya yalikuwa maneno ya huyu mnaafiki SITTA ambaye nashindwa kuelewa ni kwa nini RAIS WETU hamfukuzi kazi na C.C.M kumfukuza uanachama ili aungane na MAHAYAWANI wenzake (CHADEMA)!!!
    Kama kweli sitta ana uchungu na fedha za walipa kodi ni kwa nini alitumia bilioni mbili kujitibu????? na ni kwa nini alitumia bilioni tatu kujenga ofisi isiyotumiwa tena na spika URAMBO??????
    angeuliza swali hilo kwa serikali "kuna uharaka gani wa kujenga ofisi ya spika kabla ya kujulikana spika ajae atatoka jimbo gani la uchaguzi" kwa kua kulikua na 10% yake kwenye ule ujenzi akaharakisha bila kuzingatia anaweza kuukosa uspika!!!!
    madeni ya BENK YA DUNIA NA IMF hayana athari za kisheria yakichelewa kulipwa, hili la dowans tukichelewa tutajikuta tunalipa hata mara kumi mbele ya safari!!! SITA ACHA KUPOTOSHA UMMA!!!! ONDOKA SERIKALINI, NA ONDOKA C.C.M tumekuchoka!!!

    ReplyDelete
  21. hongera sita kama mliweza kugoma chuo kikuu cha Dar 1966 tufanye kugoma kulipa deni hili mzalendo mwanamapinduzi halisi kaza buti tutafika tu kwa luga yetu punda atakamuliwa tu hata akirusha mateke ugushengwa duhu a milk milker adonkey sorry an ass,sorry Punda ,sorry nzobe.

    ReplyDelete
  22. Bw. Luhanjo unakana nini kuwepo kwa huo mkutano wakati gazeti la guardian la tarehe 19 Jan limechapisha picha ya ministerial cabinet meeting ktk ukurasa wake wa 4? au na hiyo picha ni ya kughushi? A kukanusha kila jambo ni desturi tu! tutamwomba Assange afanye vitu vyake

    ReplyDelete
  23. TUACHE USHABIKI WA KUFILISI NCHI, MBONA MADENI YA WAZEE WASTAFU WA AFRIKA MASHARIKI HAWAJALIPWA MIAKA KIBAO, LEO MNATAKA KULIPA MATAPELI WA DOWNS!

    ReplyDelete
  24. " We can be right but sometimes right in wrong direction".

    Uwajibikaji wa pamoja hauna maana ikiwa "Upamoja" huo hauna manufaa kwa jamii husika.Ni vema tuwape nguvu Sitta na Dr. Mwakyembe, ili waweze kuzuia hilo ndani ya chama chao.....

    ReplyDelete
  25. samweli sita ni mnafiki mkubwa na hana hata maana zee zima tena linajua sheria bado linataka lipate umaarufu sioni sababu ya kupingana na watu wanaojua sheria zaidi yako wewe na wanafiki wenzako mlikomaa mpaka mikataba ikavunjwa bila kufaata taratibu unafikiri wenzako ni mambumbu kama ulivyofikiria?sheria wanazijua zaidi ya ww mwenye msimamo wa wizi ulipokuwa na mabasi tabora na urambo miaka ya sabini na thamanini mwanzoni we hela uliitoa wapi?sasa umenyimwa shavu unajifanya unachongo hutufai mchonganishi mkubwa usitafute umaarufu usiokuwa na msingi

    ReplyDelete
  26. Nyie mnaopinga Sita ndio wanafiki na mahayawani. Hamna mtu yoyote mwenye akili timamu atakayekubali kumlipa mwizi. Hamna cha Mahakama ya Usuluhishi wala nini. Hii ni International Chamber of Commerce; siyo International Criminal Court. Ndio maana China wanawapita risasi mafisadi wao; Tanzania wanatukuzwa.

    ReplyDelete
  27. MZEE NDESAMBURO ALISEMA BUNGENI,MAFISADI CHINA WANAPIGWA RISASI,WABUNGE WAKACHEKA,MAANA WALIONA KULA YAO IPIGWE RISASI TENA, MAFISADI WAMEKAA PALE BUNGENI KIMYA,USEME ROSTAM AKUWEKE ALAMA,UTAKUWA HUJIPENDI AU.KUWAFUNGA MAFISADI HAPA KWETU HUWEZI,NDIO RISASI TENA,HAYO NDO MAMBO YA BATA NA KUKU,YALEYALE!!!!

    ReplyDelete
  28. Nadhan watu wote mmechambua na kuandika vizuri kila mtu kwa uelewa wake jambo ambalo nadhani ni sahihi ila tuu niseme yafuatayo:-
    1).sijapenda matumizi ya maneno ya kashifa kwani inaonyesha ni kwa namna gani hatujakomaa katika kutoa hoja na kutetea maslahi yetu na Taifa zima kwa ujumla.
    2). Tunatakiwa kuonyesha kwamba hatuongei tuu,kwa sababu haya ni mambo ya kitaalamu ambayo pia yanakwenda kwa utaratibu wa kisheria na kufuata muda,hivyo Watanzania ambao wamebahatika kwenda shule za sheria wawaelekeze Watanzania wenzao ni nini kinaweza kufanyika ili kulinusuru Taifa hili na ulipaji wa pesa hizo ambazo watu hawajaridhika ni kwa nini zilipwe na mimi nikiwemo.
    3) Nakumbuka Mh.Mwakyembe kwenye mahojiano na vyombo vya habari baada ya kugundua kwamba Richmond ni kampun hewa hoja yake ilikuwa inawezekanaje kampuni hewa ilete kampuni isiyohewa kuchukua nafasi yake?,Bunge lazima likubali kwamba chini ya Spika Sitta lilichangia kuliingiza Taifa mahali lilipo kwani walikuwa na nafasi baada ya kuiondoa Richmond na Mhe.kujiuzulu, kuwa makini katika kusainisha mikataba makampnu yanayopewa kazi hapa nchini kwa kufuata taratibu za kisheria,na kuhakikisha kuwa hakuna nafasi ya udanganyifu.

    4) kwa sababu hukumu inakwenda na muda kile kinachotakiwa kufanyika kifanyike ili kuzuia ulipwaji wa pesa hizo haraka iwezekanavyo kwani tutakalia kurumbana na mwisho wake watanzania tulioko vijijini ambao hatujui kama kuacha kulipa ni sahihi au siyo sahihi tutaishia kula nyasi wakati wachache wananeemeka na fedha zetu.
    5)Niwatake Watanzania wenzangu kuto kaa kimya katika kudai haki zetu ila tuu tufuate utaratibu ili Kuuonyesha ulimwengu na wale ambao tunahsi kuwa ni wahusika wa DOWANS kwamba tumechoka na hatutavumilia vitendo vya kinyama wanavyotutendea Watanzania wenzao.

    MUNGU WABARIKI WACHANBUZI NA UWAPE HEKIMA YA KUANDIKA MANENO YANAYOJENGA

    ReplyDelete
  29. Tatizo letu ni kupoteza mwelekeo badala ya kushugulikia chanzo tunahangaikia matokeo. Mtu nyama akulindie. Badala yake anawapa mbwa kama Richmond, Dowans n.k. Hawa mbwa wamepewa hiyo nyama kihalali na mikataba wamesaini na mwakilishi wako ambayo pamoja na mambo mengine ni

    haƮruhusiwi kutaja majina ya wamiliki wa hao mbwa. Sasa sisi badala ya kumwaandama yule ftuliyemkabidhi ile nyama tunakadha kumwandama huyo mbwa. Mara eti amtaje mmiliki wake, mara eti yeye ni hewa. Hao mbwa wala hawakuwa hewa. Hela walichukua na mitambo walileta na umeme walizalisha hata kama ilichukuwa kipindi kirefu kiasi gani kwani mkataba uliwaruhusu. Mkataba tunambiwa ni wa siri, sisi wamiliki wa hiyo nyama haturuhusiwi kuuona.
    Sisi tumekazana tu kuwaandama hao mbwa na jamaa
    linaendelea kuwapa mbwa wengine ambao wengi hatuwajui. Hivi tuna akili kweli, tunapaswa kuzinduka nakuwashughulikia wote waliotuwakilisha kuwapa hao mbwa.

    ReplyDelete
  30. Hivi mtu akitoa msimamo wake kwa masilahi ya walio wengi ndio aitwe mchonganishi? Mimi nadhani dhana ya pamoja ni kujali waio wengi na siyo masilahi ya wachache kwa mujibu wa quotes za sheria. Sheria iko kwa ajili ya wakosaji HAIKO KWA WENYE HAKI JICHO LA MUNGU LINALOWAANGALIA. Mkate hautokani CCM hata wakifukuzwa CCM na kupokonywa UWAZIRI wataishi MBONA akina Mambo, Maganga na Maskini tunaishi, je MWENYEZI MUNGU katukataa? Ushabiki wa kichama uachwe kwenye hili...kama kweli tunataka MUNGU AIBARIKI NCHI HII tuanze na kuwalipa WASTAHAFU wa Jumuiya ya Afrika Mashariki la sivyo LAANA YA WAZEE HAO itaiandama CCM. Maneno makali ya shutuma kwa Sitta yana mwelekeo wa chuki za kisiasa..hapa si mahali pake..hasa Watanzania tunapoharakishwa kulipa deni wakati options zengine hazijafanyika. Kwa nini tusiFIKIE MAHALI pa kuHARAKISHA KUONDOA UMASKINI kwa WATANZANIA kwa fedha hizo na KUIEPUSHIA NCHI LAANA YA WAZEE WETU wa EAC? Mimi nasema Sitta na Mwakyembe lenu ni KUMWOGOPA MUNGU SIKU ZOTE WACHA MUNGU WENGINE WANAOMWOGOPA MUNGU WATAWAUNGA MKONO. Uamuzi wa pamoja usioendana na ANAYOSEMA MUNGU NI BATILI. HUWEZI KUAPA UMESHIKA KITABU KITAKATIFU KILICHO NA NENO LA UZIMA HALAFU U-COMPROMIZE-MUNGU HADANGANYIKI.

    ReplyDelete