LONDON, Uingereza
KLABU ya Chelsea itakomesha matumaini ya klabu ya AC Milan kuweza kumsaini, Jose Bosingwa kwa kukumwongezea mwaka mmoja katika mkataba wake wa
sasa.
Mkataba wa mchezaji huyo unaisha katika majira ya joto yajayo na klabu hiyo ya Serie ilikuwa ikimmendea kwa kutaka kumsaini katika dirisha dogo au kusubiri kumchukua bure, baada ya mkataba wake kuisha.
Lakini Klabu hiyo ya Stamford Bridge, inataka kutumia kipengele cha uamuzi wa kuongeza mkataba kwa kumpatia mkataba wa mwaka mmoja zaidi, kitu ambacho kitazima matumaini ya Milan kuweza kumtwaa Bosingwa.
Wakati huohuo, Didier Drogba amesema kuwa ugonjwa wa malaria alioupata ulikuwa umeanza kwa dalili za mafua.
Mchezaji huyo kutoka Ivory Coast amefunga mabao mawili tu katika Ligi Kuu kuanzia Oktoba, kiwango chake kimeathiriwa na ugonjwa huo.
Drogba alisema: "Ilikuwa mbaya sana, ilikuwa mbaya kwa miezi miwili. Ilitakiwa kuwa ni kitu cha kuisha kwa wiki chache. "Kwa mara ya kwanza vipimo havikuonesha alikuwa ni malaria, daktari alifikiri kuwa ilikuwa ni mafua, ndiyo maana tulipoteza muda.
"Wakati tulifikiri kuwa ilikuwa ni mafua nilikuwa nikiendelea kucheza, kwa kuwa kwangu ninaweza kuyakabili mafua. Nilipoteza hali ya ufiti, lakini nilijituma na kujaribu kusaidia timu.
No comments:
Post a Comment