LONDON, England
KOCHA Jose Mourinho, amevunja ukimya kuhusu tetesi zinazohusu hatma yake katika timu ya Real Madrid, baada ya kusema kuwa huenda akarudi
nchini England mapema isivyotarajiwa.
Mourinho, ambaye yupo katika mvutano na Mkurugenzi wa Michezo wa Real Madrid, Jorge Valdano aliliambia gazeti la Sunday Mirror kuwa mara zote amekuwa akiwazia kurudi kufundisha soka nchini England, baada ya kuondoka Chelsea mwaka 2007.
"Mara zote ni jambo la msingi kwa mimi na familia kuwa na furaha na nalipenda soka la Uingereza na familia yangu wanaipenda England," aliliambia gazeti hilo la Mirror.
"Na mara zote nimekuwa nikiwaza kwamba siku moja nitarejea nchini Uingereza na huenda ikawa mapema isivyotarajiwa," aliongeza.
Mourinho ambaye alitua katika klabu hiyo ya Bernabeu majira ya kiangazi yaliyopita baada ya kuingoza Inter Milan, amekuwa akipigania kuhakikisha timu hiyo inatwaa ubingwa wa Klabu Bingwa Ulaya.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 48 ambaye aliiwezesha, Chelsea kutwaa mataji mawili ya ligi katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wake, alisema kuwa kamwe hatarajii kurudi katika klabu hiyo wakati mfanyabiashara raia wa Russia, Roman Abramovich ataendelea kuwa mmiliki wa timu hiyo.
No comments:
Post a Comment