01 February 2011

Djokovic bingwa tenisi Australia

MELBOURNE, Australia

MCHEZAJI Novak Djokovic, aliibuka bingwa wa tenisi wa mashindano ya Wazi ya Australia.Djokovic baada ya kumaliza mechi na kuibuka mshindi
aliirusha raketi yake kwa mashabiki, kisha alivua fulana yake na kuirusha sambamba na viatu vyake kutokana na furaha.

Mchezaji huyo raia wa Serbia, mwenye miaka 23 alimshinda mpinzani wake ambaye ni mwingereza, Andy Murray kwa 6-4, 6-2, 6-3 katika mechi iliyochezwa Jumapili usiku.

Djokovic ametwaa ubingwa wa mashindano hayo kwa mara ya pili na kufanya awe mchezaji wa nne, kati ya wanaopendelea kucheza kwa wanaume kutwaa makombe mawili makubwa katika mashindano ya kila mwaka.

Rafael Nadal na Roger Federer ni wachezaji wengine walioshinda mara 21 kila moja katika mechi 23, huku Lleyton Hewitt alitwaa mara mbili kwenye ya mashindano ya Wimbledon  mwaka 2002.

"Ni mashindano ya kusisimua kwangu mimi," alisema Djokovic na kuongeza, "sitaki kuruka hadi kwenye anga na kusema, "Nimekuwa mzuri sana."

Alisema hawezi kujilinganisha na Rafa na Roger kwa mafanikio.

Nadal alikuja katika mashindano ya Australia, akitaka kutwaa kwa mara ya nne mfulilulizo lakini alifungwa kwenye robo fainali.

Federer alikuja kama bingwa mtetezi, alifungwa na Djokovic katika nusu fainali.

Murray ameumia mno kwa kufungwa na mchezaji namba tano kwa kiwango.

Djokovic na Murray ni marafiki tangu walipoanza kucheza pamoja wakiwa na miaka kati ya 11 na 12, wamekuwa na kawaida ya kufanya mazoezi pamoja.

Katika mechi nyingine ya wanawake wachezaji wawili wawili, Katarina Srebotnik wa Slovenia na Daniel Nestor wa Canada waliibuka washindi kwa kuwabwaga, Chan Yung-Jan wa Taiwan na Paul Hanley wa Australia kwa 6-3, 3-6, 10-7.

No comments:

Post a Comment