01 February 2011

Madiwani Moshi waishika pabaya CCM

Na Heckton Chuwa, Moshi

MADIWANI wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro jana waliweka pingamizi kwa Msajili wa Mahakama ya Ardhi kuzuia
ubadilishaji au uendelezaji wa viwanja na nyumba ambavyo vinamilikiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Moshi Mjini na jumuiya yake ya Umoja wa Vijana  (UVCCM) mkoani hapa.

Akitoa tamko kuhusiana na uamuzi huo kwa niaba ya meya wa halmashauri hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Mipango Miji na Mazingira wa Halmashauri hiyo, Abdrahman Sharif, alisema madiwani wa halmashauri hiyo wameamua kuchukua hatua hiyo kutokana na taarifa za kiintelejinsia zinazoonyesha kuwa CCM wanahaha kubadili umiliki wa mali hizo.

“Tumefanya uchunguzi wa kina kwa kuzingatia sheria zote na kubaini kuwa mali hizo ni mali halali za halmashauri ya manispaa ya Moshi,” alisema Diwani Sharif ambaye pia ni katibu wa madiwani wa CHADEMA katika Baraza la Madiwani wa halmashauri hiyo.

Akitolea mfano wa uchunguzi huo, Bw. Sharif alisema kuwa viwanja na jengo linalotumiwa na UVCCM vyenye ukubwa wa ekari 2.7 vina hati miliki nambari 15686 na kwamba imemilikishwa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi kwa miaka 33.

“Kufuatia uhalali huu, CCM ilitakiwa iwe inailipa halmashauri sh. milioni 20 kwa mwaka na kiwanja na jengo ambalo CCM wilaya Moshi Mjini imefanya kuwa ofisi zake vina ukubwa wa square futi 18,790 na vimesajiliwa kwa hati nambari 056038/94,” alisema.

Aliongeza kusema kuwa hatua walizochukua ni muhimu na zenye manufaa kwa umma na kwamba hazilengi kumkomoa mtu au taasisi yoyote zaidi ya kuzikomboa na kuzilinda mali za halmashauri hiyo.

“Mchezo huu wa CCM umekuwa ukiidhulumu halmashauri ya manispaa ya Moshi zaidi ya sh. milioni 100 kwa mwaka na tunachotaka ni fedha hizi zitumike kwa ajili ya maendeleo ya watu wa Moshi,” alisema.

Akijibu maswali kuhusiana na swala hilo, Bw. Sharif alisema uamuzi huo ni wa madiwani wa halmashauri hiyo na kwamba pamoja na kuwashirikisha madiwani wenzano wa CCM madiwani hao wa chama tawala hawakujitokeza wakati wa kutolewa kwa tamko hilo.

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Moshi Mjini, Bw. Godfrey Mwangamilo alisema swala hilo linafuatiliwa na Katibu wa CCM wilaya ya Moshi Mjini na kwamba chama hicho kina uhalali kuhusiana na mali hizo, hivyo madiwani hao wamekurupuka.

6 comments:

  1. Hawa CCM wameshika mali nyingi sana za serikali na halimashauri na kuzifanya mali yao. Pia huko nyuma kabla ya mfumo wa vyama vingi walijenga majengo ya ofisi mikoani na wilayani kwa michango ya kulazimisha wananchi au kuongeza bei ya bidhaa kama vile sukari, nk. Ipo haja ya kuorodhesha mali hizo, sio huko Kilimanjaro tu bali nchi nzima zirudishwe kwa wananchi haraka. Enzi ya kutumia mabavu imeshapitwa na wakati.

    ReplyDelete
  2. CCM WANAHITAJI KUBADILIKA KUJALI MASLAHI YA WANANCHI KWANZA. WAO BADALA YAKE WAMEKUWA MSTARI WA MBELE KUPORA VIWANJA NA MAJENGO KITU AMBACHO HAKITOI PICHA NZURI, KWANI HUU NI WIZI NA UNYANG'ANYI WA MALI ZA WANANCHI AMBAO CCM INATUMIA MABILLIONI YA SHILINGI KILA BAADA YA MIAKA MITANO, KUGOMBEA KUWAONGOZA. KULE MIKOANI PIA, CCM IMENG'ANG'ANIA VIWANJA VYA MICHEZO, AMBAVYO WANANCHI WOTE WALICHANGIA UJENZI WAKE. HII NI HALALI KWELI? WAKATI WA KUCHANGIA VIWANJA HIVYO NA HATA BAADHI YA MAJENGO WANAYOYATUMIA, KULIKUWA NA CHAMA KIMOJA TU, LAKINI SASA TUNA VYAMA VINGI NA HIVYO SI HALALI KWA WAO KUHODHI MALI HIZO. MWISHO TUTAAMBIWA HATA SHULE ZA KATA NI ZA CCM. MATOKEO YAKE NI KUWA VIWANJA HIVYO NA MAJENGO HAYO YANAENDELEA KUCHAKAA, HUKU KODI NA MAPATO VINAYOINGIZA VIKILIWA NA CCM BILA KUWA NA MIPANGO YA KUVIENDELEZA. KWA NINI HALMASHAURI ZISIKABIDHIWE KUVIENDELEZA, KWANI HATA WAKATI WA UJENZI, VIFAA VILIVYOTUMIKA VILIKUWA VIKITOKA KWENYE HALMASHAURI ZA MIJI NA IDARA ZA UJENZI, NA SIYO CCM. CCM WENYEWE HAWAKUCHANGIA HATA SENTI TANO, HUU NI WIZI.

    ReplyDelete
  3. JAMANI WACHA CCM WAJIFIE MBALI MAANA WATU WAKE WAMEKUWA WAROHO NDIO MAANA WANASEMA HATA JESHI LA POLICE NI LAO......CCM ACHENI MALI ZA UMA ZIMELIKIWE NA UMA WENYEWE MTAJALETA MAAFA

    ReplyDelete
  4. NDIO MAANA WANANG'ANG'ANIA uongozi, wanajua watapata hasara ya mambo mengi.

    Chadema tumewapa nafasi ya upinzani bungeni kwa kupitia kura zetu. Tunaomba mfanyie uchunguzi suala la umiliki wa viwanja, majengo na mali zingine za wananchi nchi nzima.

    Mali zote zilizomilikishwa kwa CCM kinyume na sheria zirudi haraka mikononi mwa wananchi.

    ReplyDelete
  5. Binafsi yanghu mimi nasema yale ya misri yapo njiani si uongo kwani wananchi washachoka mnoooooooo! hata cc tuliopo ULAYA huku tunasikia hayo tumechoka wakuu nchi ni ya wananchi si ya MASISADI jamani! hebu sasa hao wasenge wajua watu wameamka ndo maana tunakimbia nchi kuja kusoma nje wakati tuna nchi nzuri sana huku ulaya wanatamani wangekuwa na nchi kama yetu lkn viongozi hawa wa chama cha matapeli. wameharibu nchi , na wanazidi kuhiaribu. ni mimi AFANDE TUMAINI WA POLICE DAR. nikiwa masomoni EUROPE.

    ReplyDelete
  6. sasa mambo yameanza. ya Moshi ni madogo sana.ila bado mengi yapo njiani yanakuja. ma faili yatachomwa moto, dokumenti zitagushiwa ama kubadilishwa nk. tusubiri tu

    ReplyDelete