01 February 2011

Kostadin Papic akwama kuondoka

*Anadai mpaka kieleweke

Na Elizabeth Mayemba

KOCHA Mkuu wa Yanga  Kostadin Papic jana amekwama kuondoka nchini kwenda kwao Serbia kwa madai kwamba
hadi uongozi wa klabu hiyo, utakapomlipa fedha zake.

Papic amelazimika kuachana na Yanga ghafla, baada ya kusigana na viongozi wa klabu hiyo kwa madai ya kutoshirikishwa kwa baadhi ya vitu vya kiufundi ikiwemo kumteua, Felix Minziro kuwa msaidizi wake kitu ambacho hakuafikiana nacho.

Kocha huyo awali aliutaka uongozi wa Yanga, kumtafutia msaidizi ambaye atakuwa hajatoka kwenye timu zinazocheza Ligi Kuu kama ilivyo kwa Minziro ambaye kabla ya kuteuliwa alikuwa Kocha Mkuu wa Ruvu Shooting.

Habari zilizopatikana Dar es Salaam jana kutoka kwa mtu wa karibu na kocha huyo zilidai kwamba, Papic alikuwa aondoke nchini jana lakini ameshindwa kwa kuwa kuna vitu vinamkwamisha ikiwemo malipo yake kutoka kwa viongozi wa Yanga.

"Jamaa amekuwa mgumu kubaki nchini ameng'ang'ania kurudi kwao na uongozi umeshindwa lakufanya na kumuacha aamue analolitaka, kwani kama kumbembeleza wamefanya hivyo sana, lakini amekuwa mgumu kuelewa," alidai rafiki wa karibu na kocha huyo.

Alidai kwamba kocha huyo kuna fedha za nyumba, ambazo anaidai klabu hiyo hivyo wakimalizana wakati wowote anarudi kwao Serbia.

Habari hizo zinadai kuwa kocha huyo ameweka msimamo wake wa kuondoka kwa madai kwamba hawezi kufanya kazi na Minziro wala Meneja wake Salvatory Edward.

Alipotafutwa Mwenyekiti wa klabu hiyo, Lloyd Nchunga ili kupata ufafanuzi zaidi kuhusu madai ya Papic, hakuweza kupatikana baada ya simu yake ya mkononi kuwa imezimwa.

2 comments:

  1. papic inatosha,,ondoka zako kwani kuwepo hapo tena,,utaigawa yanga yetu,,waserbia hamna jipya zaidi ya 50% za kusajili wachezaji hewa kina mba,,boakye...wa tz wengi wanajua mpira,,tumwache mzawa,,akiwezeshwa ataweza,..

    ReplyDelete
  2. aondoke haraka sana ni msanii huyo jamaa ,mbona anajiona kama kocha wa hali ya juu sana! hata akina mourinho hawaringi kama huyo jamaa.aondoke tu asiwachanganye wanayanga.

    ReplyDelete