LONDON, Uingereza
KLABU ya West Ham, iko katika foleni ya kutaka kumsaini mshambuliaji, Emmanuel Adebayor katika kipindi cha dirisha dogo Januari, mwakani.Hammers inataka kumsaini nyota huyo wa Manchester City, kutoka Togo kwa kuwa
katika timu yake amekua akisugua benchi na kwamba City, imemtangaza kuwa miongoni mwa inaotaka kuwauza.
Na wamiliki wa West Ham, David Sullivan na David Gold wako tayari kujipiga piga ili kumchukua mshambuliaji huyo wa zamani wa Arsenal.
Chanzo kutoka Upton Park kilisema: "Hakuna siri Adebayor hana raha katika City kwa hiyo tunataka kujaribu kujipanga kumchukua.
"Bila shaka kuna klabu kubwa zinamtaka katika majira ya joto, lakini sisi tuna nafasi ya kumleta hapa kwa mkopo."Timu hiyo inataka kumpata mshmabuliaji huyo, ikiwa ni jitihada zake ili kukwepa kushuka daraja, kocha wake Avram Grant, hivi sasa yuko katika wakati mgumu.
Kocha huyo ana mechi nne tu za kuweza kuokoa kibarua chake, ambapo wamiliki wa timu hiyo Gold na Sullivan wanamtaka apate pointi sita, katika mechi zijazo.Kutokana na uchezaji wa sasa wa timu hiyo, inaonekana inaweza kuwa ngumu. Timu hiyo imesema inataka kupata pointi 13, kutoka katika mechi 18 za msimu huu.
Katika mechi nne zijazo itachuanana na
Fulham, Everton na Wolves kabla ya ksuafiri kwenda kucheza na Newcastle.
No comments:
Post a Comment