Na Amina Athumani
MASHINDANO ya ligi ya mpira wa kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (RBA), yamesongezwa tena Januari 2 mwakani baada na timu kushindwa kukamilisha usajili wa wachezaji.Awali mashindano hayo yalipangwa kuanza Novemba 27, mwaka
huu lakini yalisogezwa mbele kutokana na timu kushindwa kuthibitisha mapema na yalipangwa kufanyika tena Desemba 18, lakini pia ilishindikana.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Ufundi wa Chama cha Mpira wa Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BD), Mbaga Mwamboma alisema wameyapaleka hadi mwakani ili kuzipa nafasi timu kujipanga vyema.
"Kwa sasa tumepanga hii kuwa ni tarehe ya mwisho na timu itakayoshindwa kukamilisha taratibu haitaweza kushiriki, kwani tungekuwa tumeyaanza mapema hivi sasa tungekuwa tunaelekea ukingoni kuyamaliza," alisema Mwamboma.
Alisema BD imepanga hadi Desemba 26, mwaka huu iwe mwisho wa kupokea usajili wa timu na kukamilisha taratibu zote zinazotakiwa na kwamba kinyume na hapo hawataruhusu timu kushiriki.
No comments:
Post a Comment