31 December 2010

Lady Jay Dee aibuka na maji

Na Amina Athumani

MSANII maarufu wa kizazi kipya, Judith Wambura 'Lady Jay Dee',  amezindua bidhaa yake mpya ya maji yanayojulikana kwa jina la Jay Dee.Akizungumza Dar es Salaam jana,  wakati wa uzinduzi wa bidhaa hiyo ya
maji, Lady Jay Dee alisema kuanzia mwaka 2011, atafuta shoo zake zote na kubakiza moja ili apate nafasi ya kufanya ujasiriamali na shughuli mbalimbali za kijamii.

"Nafuta shoo zangu zote na kubakiza moja ambayo itakuwa kila Ijumaa pale Mzalendo Pub, ili niweze kuwa na nafasi kubwa ya kutembea sehemu mbalimbali ya kufanya kazi za kijamii,¡± alisema.

Alisema mbali na kuzindua bidhaa hiyo ya maji, pia anatarajia kuanzisha mgahawa wake wa vyakula Januari mwakani ambao utakuwa na hadhi ya kimataifa na utakuwa ukipika vyakula vya kiswahili vyenye asili ya kiafrika.

Alisema ataendelea kufanya muziki kama msanii, huku bendi yake ikiendelea kufanya kazi kama bendi na kupanua muziki wake kwa kutembea sehemu mbalimbali na kujumuika  katika kazi za kijamii.

Alisema kwa sasa anajiandaa kutoa albamu yake aliyowashirikisha wasanii mbalimbali wa ndani na nje ya nchi.

No comments:

Post a Comment