31 December 2010

'Chelsea' waua shabiki wa Arsenal

KAMPALA, Uganda

JESHI la Polisi katika Wilaya ya Bundibugyo nchini Uganda, linawasaka mashabiki watatu wa timu ya Chelsea kwa kumpiga na kumuua shabiki wa Arsenal.Kamanda wa Polisi wa Wilaya hiyo, Dennis Namuwoza, alimtaja marehemu kuwa
ni  Bernard Mugenyi (18), ambaye ni mfanyabiashara ya chapati na ni mkazi wa kijiji cha Bunyaruta kilichopo Tarafa ya Bubukwanga.

Kamanda Namuwoza, alisema Mugenyi aliuawa Jumatatu usiku na wanaume watatu ambao walitambulika kwa jina moja moja la Ronald, Sedrack na Abbasi, baada ya  Chelsea kufungwa mabao 3-1.

Namuwoza alisema baada ya mechi kumalizika watuhumiwa walienda katika meza ya Mugenyi na kula chapati sita, lakini wakakataa kulipa na baada ya majibizano ya maneno Mugenyi, anadaiwa kuwatania kuhusu kipigo ambacho timu yao ilikipata, jambo ambalo liliwatia hasira na kuanza kumshambulia na watu hao kutimka baada ya kubaini Mugenyi amefariki.

No comments:

Post a Comment