31 December 2010

...Kuitangaza nafasi ya Mpangala

Na Elizabeth Mayemba

UONGOZI wa klabu ya Yanga unatarajia kuitangaza nafasi ya Meneja wa timu hiyo mwakani.Kwa sasa nafasi hiyo inashikiliwa na Emmanuel Mpangala, ambaye katika uongozi uliopita alikuwa Katibu wa Kamati ya Mashindano.Habari za
kuaminika zilizopatikana ndani ya klabu hiyo Dar es Salaam jana, zilidai kuwa, uongozi huo tangu wiki iliyopita ulikuwa ukiitafakari nafasi hiyo.

"Meneja wa sasa mwisho wake ni Desemba mwaka huu, hivyo kuanzia mwakani atatafutwa mwingine, kwa upande wetu hatuoni kama Meneja wa sasa ni mbaya, lakini kwa kuwa uongozi umeamua hatuna budi kukubaliana nao," kilieleza chanzo cha habari.

Chanzo hicho kilieleza kuwa, sifa mojawapo inayotakiwa kwa Meneja huyo, anatakiwa awe mwanachama halali wa Yanga, aliyewahi kuichezea timu hiyo, elimu na awe karibu na wachezaji.kilieleza kuwa, meneja wa sasa, Mpangala hatakatazwa kuomba nafasi hiyo kama anajiona anavigezo vinavyotakiwa, kwani ni haki ya kila mwanachama kuomba nafasi hiyo.

Hata hivyo, kuna baadhi ya viongozi ambao wameliafiki suala hilo, lakini mmoja wa viongozi wa juu wa klabu hiyo, hakubaliani na maamuzi hayo ambaye alisema haoni sababu ya kuitangaza nafasi hiyo.

No comments:

Post a Comment