07 November 2010

Waziri, Manoti kuzichapa leo.

Na Addolph Bruno

MABONDIA Njiri Waziri na William Manoti, leo watapigana kuwania ubingwa wa ngumi Mkoa wa Dar es Salaam, katika ukumbi wa Southern Park
, jijini Dar es Salaam.

Pambano hilo litakuwa la uzani wa light heavy, raundi nane litatanguliwa na mapambano ya mabondia wengine wanaochipukia.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mratibu wa pambano hilo, Omari Yazidu, alisema maandalizi ya pambano hilo yamekamilika, ikiwa pamoja na kupima afya za mabondia hao.

Alitaja mapambano ya utangulizi ni kati ya Said Yazidu na Yusuph Jibaba, Mbaruku Heri atapigana na Chusa George, Kadoda Machupa atazichapa na Ali Bugingo.

Alisema mgeni rasmi katika pambano hilo atakuwa ni Diwani Mteule wa Kata hiyo, Green Chilambo.

No comments:

Post a Comment