07 November 2010

Mjomba Band kwenda Uholanzi.

Na Tumaini Maduhu

BENDI ya Mjomba inayomilikiwa na Mrisho Mpoto, inarajiwa kufanya ziara nchini Uholanzi kwa ajili ya kujitangaza katika soko la kimataifa hivi karibuni.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mpoto alisema watahakikisha wanafanya vizuri katika ziara yao ili watambulike kimataifa.

Alisema anaamini ziara hiyo itawasaidia kuwajengea ujuzi, uzoefu na ubunifu kwenye masuala ya muziki wa kimataifa.
Tunawakaribisha wasanii wa jinsia zote, hatubagui kwani lengo letu ni kufanya kitu cha maendeleo,¡± alisema.

Mpoto alisema bendi yake iko tayari kufanya kazi na mtu yeyote ikiwemo kutengeneza matangazo mbalimbali ya biashara

No comments:

Post a Comment