10 November 2010

Tamsha la Str8 Muzik kufanyika mikoa mitatu.

Na Mwandishi Wetu

STR8 Muzik imerudi tena mwaka huu huku wasanii maarufu Afrika Mashariki na wa kimataifa wakitarajiwa kutumbuiza mashabiki wa muziki nchini hususan wanafunzi wa
vyuo mbalimbali.

Akizungumza Dar es Salaam jana Meneja Msaidizi wa Chapa ya Sweet Menthol (SM), Isamba Kasaka, alisema tukio hilo linatarajiwa kuanza kufanyika Jumamosi mjini Marogoro.

Alisema tamasha la pili litafanyika mkoani Dodoma katika Ukumbi wa Royal Village Novemba 20, wakati tamasha la tatu litafanyika Dar es Salaam Novemba 27, mwaka huu katika viwanja Posta, Kijitonyama.

Alisema katika mikoa ya Morogoro na Dodoma mashabiki watalipa kiingilio cha sh. 3,000 na kwenye tamasha la Dar es Salaam kiingilio kitakuwa sh. 10,000.

Isamba alisema STR8 Muzik, imepania kuwatangaza wasanii wa ndani na pia kuwaleta pamoja wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali.

Mwaka jana, katika tamasha la Str8Muzik lilimleta mwanamuziki maarufu kutoka Nigeria D Banj.

“Kwa miaka mingi, tamasha la Str8 Muzik limeiwezesha jamii kujumuika pamoja katika furaha na kupata burudani za kidunia kupitia wasanii maarufu kama vile Eve, Fat Joe, Maya, Shaggy, Wayne Wonder, Malaika na Sean Paul,” alisema.

Alisema mwaka huu mashabiki watarajie mambo makubwa ya burudani kutoka kwa wasanii maarufu kama T Pain, Elephant Man, Gyptian na Mims pamoja na wasanii wengine wa Afrika Mashariki kama vile Michael Ross wa Uganda, Fid Q, Mwana FA, Joh Makini, Chege na Sam Wa Ukweli

No comments:

Post a Comment