10 November 2010

Sitta kuigharimu CCM 2015.

Na John Daniel

MCHUANO wa nafasi ya uspika ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), umezidi kufichua mengi baada ya baadhi ya wabunge na wanazuoni wa chama hicho kutoboa siri kuwa kauli za
kejeli dhidi ya Spika Samuel Sitta ni maumivu yanayotokana na majeraha ya vita vya ufisadi.

Wabunge hao wameonya kuwa iwapo CCM kupitia Kamati Kuu (CC) itamwangusha Bw. Sitta katika kinyang'anyiro hicho, chama hicho kitajutia kitendo hicho katika uchaguzi Mkuu mwaka 2015.

Wakizungumza na Majira kwa nyakati tofauti jana, baadhi ya wabunge hao wateule na wanazuoni waliojipambanua kuwa ni wana-CCM walisema wanasikitishwa na hali iliyojitokeza juzi, ya mmoja wa wagombea, Bw. Andrew Chenge kumshambulia Bw. Sitta bila sababu za msingi zinazoeleweka kwa wananchi.

"Mhe. Chenge ni mzoefu ndani ya chama, anajua taratibu zote za kumjadili na kumwonya mtu ndani ya chama kupitia vikao. Inasikitisha na kuzua maswali mengi inakuwaje anamrushia mjumbe mwenzake wa Kamati Kuu shutuma za kizushi kiasi kile," alihoji mmoja wa wabunge CCM.

Mbunge huyo aliyekuwa akizungumza na Majira kutoka Dodoma, alisema kitendo hicho ni dalili mbaya ya mpasuko mkubwa ndani ya CCM.

Alisema kama angekwepo Baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius Nyerere angechukua maamuzi mazito dhidi ya Bw. Chenge na kumaliza tatizo hilo.

"Shutuma zote na vita vikali vinavyoelekezwa kwa Sitta ni kutokana na majeraha ya vita vya ufisadi, watu hao wanatafuta njia ya kujisafisha na kudanganya Watanzania kwa malengo yao binafasi hapo baadaye.

Kama angekwepo Baba wa Taifa angechukua fomu ya Chenge na kuitupa kwenye shimo la takataka, tena angefanya hivyo kwenye Kamati Kuu mbele ya wajumbe, alichofanya ni jambo la aibu na ameonesha ishara na dalili mbaya sana kwa chama mbele ya jamii," alidai mbunge mwingine.

Baadhi ya wanazuoni walisema baada ya uchaguzi Mkuu Mwenyekiti wa chama hicho Rais Jakaya Kikwete, anapaswa kuwa makini zaidi na kutambua kuwa ndani ya chama chake kuna kundi linalotaka kumwangusha kwa kuharibu mipango yake mziuri kwa Watanzania.

"Nadhani hawa jamaa sasa wanataka kumvuruga rais ili wananchi wachukie CCM kisha wao wajidai kuwa wanamsaidia kuimarisha chama kwa uwezo wao wa kifedha, hii ni hatari sana. Iwapo CCM itamwacha Sitta katika nafasi ya spika wa Bunge madhara yake makubwa zaidi yataonekana mwaka 2015," alisema Mbunge mwingine.

Walisema wamebaini mbinu zinazosukwa na kundi hasimu dhidi ya Bw. Sitta kuongeza nguvu kuhakikisha jina lake linakatwa kwenye Kamati Kuu kwa kuwa ikiingizwa bungeni litapita kutokana na kupendwa na wabunge wengi.

Vyanzo vyetu vilieleza kuwa Bw. Sitta anaandaliwa Wizara moja jina linahifadhiwa kwa sasa, iwapo hatapata nafasi ya uspika huku kundi hilo likimwekea mtego wa kumchafua katika wizara hiyo baadaye.

Ilielezwa kwamba kundi hilo linafanya mpango kupitia kwa watu walio karibu na Rais Kikwete ili kumpa wizara hiyo na kwamba wataandaa mtego kupitia bunge kumchafua ili kummaliza kisiasa.

Habari zaidi zilieleza kwamba kundi hilo hasimu linamwohofia Bw. Sitta kuwa iwapo hawatamdhibiti kwa mbinu chafu anaweza kuwa tishio kwao katika kinyang'anyiro cha urais mwaka 2015.

Katika hatua nyingine, mkazi mmoja wa Dar es Salaam aliyejitambulisha kama Cathy, alipiga simu chumba cha habari na kueleza masikitiko yake kwa kitendo cha Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuibuka na kumsafisha Bw. Chenge wakati huu ambapo anawania uspika.

"Hivi hii TAKUKURU ilikuwa wapi siku zote hadi isubiri wakati huu anapowania uspika ndipo itoe taarifa kumsafisha?" alihoji Bi. Cathy na kuongeza:

"Hii TAKUKURU ni ya matajiri, si ya maskini. Wanatuamuliwa mtu wanayemtaka. Inaendeshwa kwa maslahi ya watu fulani, si ya wananchi.

"Kinachonisikitisha ni kwamba hata chama chenyewe kimeshindwa kuwawajibisha watu wake, wameachwa kulindwa na TAKUKURU. Hata Mungu amekasirika ndio maana wamepata asilimia 61 licha ya mabango yao kuwekwa kila sehemu nchi nzima," alisema Bw. Cathy.

28 comments:

  1. Wewe John Daniel, acha umbeya. Napenda Sita aridi uspika, lakini uandishi wa namna hii hauna maslahi kwa taifa. Hoja zinajengwa kwamba Sita arudi kwa gharama yoyote. Lazima arudi kwa njia ya demokrasia. Kusema Nyerere angechana form ya chenge huo ni udikteta ambao umepitwa na wakati. CCM ya sasa ni chama cha kidemokrasia ambapo kila mtu ana nafasi. Kila mtu anachukuwa form na kura zinapigwa. Watu wasilazimishe kuwa lazima Sita arudi kwa gharama yoyote ile. Basi hakuna haja ya watu kuchukuwa forms. Hii staili tunaiona kwenye vyama vya upinzani siyo ccm. Kwa upende wangu ningependekeza Slaa awe spika kama wabunge wanataka maendeleo ya nchi.

    ReplyDelete
  2. Muta said ulilosema kuhusu mwandishi wa makala hii ni maoni yako,lakini CCM si chama cha demokrasia,ila ni cha wenye nacho,tena ni chama kinachokubatia mafisadi haijapata kutoke.uko hapo?? labda wewe ujaijua CCM vizuri

    ReplyDelete
  3. Mh! ni bure kumzungumzia Nyerere hapa! keshakufa zamani! lililopo ni kuawashawishi wabunge wetu tuliowapigia kura wamchague tunaeona anafaa! basi! Nyerere! Nyerere! Nyerere! alokufa hayupo!

    ReplyDelete
  4. Kuchukuwa fomu kugombea uspika ni wazi kwa kila mwana CCM,binafsi au chama cha upinzani, illa njia aliyojinadi Chenge ni kuonyesha bado ana chuki binafsi na ni kuleta mpasuko zaidi ktk Chama.Wengi wamechukuwa fomu CCM zaidi ya watu 6,lakini hawakutoa maneno,kashfa wala kejeli yeye ni nani? CCM wana busara, demokrasia na wako makini hata kama mnawaita mafisadi.Na kama wewe Muta unashauri Slaa basi ungemshauri yeye mwenyewe akachukuwa fomu kwa sasa muda umeisha.Sasa wewe unapendekeza achaguliwe kwa njia gani au lipi zaidi,kwani yumo ktk kinyang'anyiro?

    ReplyDelete
  5. Kama wananchi wangepewa nafasi ya kumchagua Spika bila shaka Sita angeshinda kwa kishindo simply kwasababu aliongoza vizuri katika kipindi chake. Ushujaa wake ndio umewezesheza wananchi kuwafahamu mafisadi akiwemo huyo mhishimiwa saaana Chenga. MUNGU WALAANI MAFISADI WOTE WAFE VIFO VIBAYA NA PESA WALIZOKWIBA ZITAFUNWE NA NYUMBA ZAO NDOGO AMENI

    ReplyDelete
  6. Tusitake kujifanya tunajuwa kila kitu na kuwapaka wengine matope.Mchakato wa kampeni umeisha sasa tuungane tujenge Nchi yetu, hivi mnapozidi kudai CCM chama cha mafisadi mnajuwa tutokako na tuendako?Unajuwa kisa cha Muasisi wa chadenma mzee Mtei kuondolewa CCM na Nyerere
    unajuwa mali anazomiliki Mbowe alivyozipata? je unajuwa Mzee Ndesamburo nae?Unajuwa Slaa kisa cha kuasi Kanisa? na hata Muadham Pengo alivyosema kabla ya uchaguzi kuhusu Slaa( kuwa kalitia doa kanisa)? Tusitake kuwekeana chuki zisizona msingi na hazisaidii Nchii yetu, unaona hata hivyo viti Maalumu vya Chaga Dev Manifesto vingi vimetoka Kanda gani? tuache longolongo

    ReplyDelete
  7. DUA LA KUKU HALIMPATI mwewe! Tunajua mafisadi ni wabaya, ila kuwalaani na kuwaombea mabaya hakusaidii. DAWA NI KUWAKATAA!!! KAMA KURA ZIMESHINDWA KUWAONDOA, TUWAKATAE KWA KUINGIA MITAANI NA KUANDAMANA - KWA HOJA. kikatiba wana haki kuchukua fomu. lakini kama hatutawakataa hadharani, hata tukiwalaani, hawataachia ngazi. kura wanahesabu wao, unatarajia nini! wakitaka Chenge awe spika wanaweza. Tuwaombe tu wabunge wa CCM wamchague yeyote hata wa upinzani kuwa spika, hasa Dr. slaa kama akichukua fomu kwa vile ana rekodi nzuri ya kufuatilia kilichoandikwa kwenye hizo sheria zinaotungwa. Wengine huwa hata robo ya hizo sheria hawazisomi. Hivi kweli kwa miaka mitano unaweza kuwa bungeni bila kuchangia hata mara moja, kama kweli unasoma na kusikiliza mijadala?
    Tunaomba kigezo kimojawapo kiwe rekodi ya uchangiaji bungeni, maana wachangiaji ndio wasomaji wazuri. na kama hajawahi kuwa mbunge, msomaji mzuri lazima awe na rekodi nzuri kazini kwake!

    ReplyDelete
  8. Wewe unaeuliza kuhusu mali za mtei,slaa, ndesamburo nk sio mahali pake naona umetumwa. ukweli ni kwamba rasilimali za nchi hii hazisimamiwi ipasavyo na hao tulowapa dhamana ya kutuongoza, badala yake wanajishibisha wenyewe na familia zao....tuwakatae mafisadi kwa nguvu zote. Ukweli ni kwamba bado tunamhitaji spika atakaeweza kuendesha midahalo kwa fair play kama sita. Mtu kama Chenge CV yake ni chafu na anaonekana yuko ki visasi zaidi.

    ReplyDelete
  9. Chenge amechengwa sasa. Hana hoja za msingi kumtukana Samwel SITTA.
    Sote tunajua alivyoiba kupitia rada na mikataba bomu ya madini.
    Hastahili kupewa nafasi ya SPIKA, ina wenyewe.
    OMARY

    ReplyDelete
  10. CHENGE NA HOSEA NI WATU WA KARIBU KABILA MOJA LUGHA MOJA NA WANAALIKANA KUNYWA BRAND PAMOJA MARA NGAPI TUNA MWONA CHENGE KWA DR HOSEA MBEZI,KINACHO CHEFUA KAMA VILE VIJISENTI NI SAFI VIPI KUHUSU WALE MAREHEMU ALIOWAGONGA KESI BADO IKO MAHAKAMANI,CHENGE AMENDASHA GARI BILA YA BIMA AMEGONGA NA AMEUWA,KWENYE VIFUNGU VYA SHERIA YA NCHI KUNA ADHABU YA MAKOSA HAYA,SASA AKIWA SPIKA KWELI HAKI ITATENDEKA KWA NDUGU WA MAREHEMU.KWA NCHI ZILIZOENDELEA TAYARI ANGEKUWA AMESHA POTEZA SIFA YA KUWA KIONGOZI LAKINI KWA NCHI YETU LOLOTE LINAWEZEKANA CHA KUSHANGAZA KUNA KIBURI CHA AJABU HIVI KWELI CHENGE HAJUI 99% YA WATANZANIA HAWAITAJI MCHANGO WAKE KAMA KIONGOZI?ANAKUBALIKA KULE KWAO ALIKOFANYA KAMPENI KWA KUTUMIA LUGHA YA KISUKUMA.CCM IKIFANYA KOSA KUMUONDOA SITA WATALIJUTIA. WABUNGE WOTE WADILIFU WA CCM NDIO WAKATI MUAFAKA WAKUJIUZULU UBUNGE KUONDA KATIKA CHAMA KWANI UPINZANI ULIONANGUVU UTATOKA KWENU KWAKUWA MNAIJUA VYEMA CCM NA SISI WANANCHI WAKAWAIDA NAMINI WENGI TUTA WAUNGA MKONO.CCM SASA IMEKAA KISULTANI YANI KUNA KIKUNDI FULANI KINAONA NI MALI YAO.CHENGE NA WENZAKO MUOGOPENI MUNGU WENU.ZUGA YAKO KUGOMBEA USPIKA,MNAE MTAKA AWE SPIKA TUNAMJUA KWA GIA KUEPUSHA MAKUNDI MUMPE MTU WENU KAMA KU NEUTRALIZE,HAITOWASAIDIA KUMBUKENI WATANZANIA WA SASA SIO WA MUNDO SABA.

    ReplyDelete
  11. Ni sawa mtei,mengi,ndesamburo na mbowe kuwa na hela,lakini wanapokuwa nazo wengine wanakuwa mafisadi,shame on you!Ni sawa Sitta kugombea uspika na kutamba kuwa yeye ni chuma cha pua,o mara sijui yeye ana ngozi ngumu,lakini wakitamba wengine wanakuwa mafisadi,shame on you the nation of the unthinking!Huyu ibilisi Sitta kawatesa sana wenzake na sasa ni zamu yake kuchakachuliwa,he must be given the taste of his own bitter pills,anyamaze aache kulialia tuone kama kweli anayo ngozi ngumu,kakutana vyuma vya pua kweli!!!

    ReplyDelete
  12. Jamani huyo Chenge ni nani? mpaka afikie hatua za kuweka vikwazo kwa sitta, jamani wabunge na waomba mchagueni spika bora asiyependelea upande wowote, nadhani tutatokomea mafisadi katika nchi yetu. Kwa mtazamo wangu ningependa Sitta aendelee na hatamu zake za uspika.

    ReplyDelete
  13. NYIE MWAGOMBANA BURE, SPIKA WA BUNGE ATAKUWA ANNA ABDALLAH MKE WA MSEKWA. CHENGE HANA CHAKE, TENA AMEWAHALIBA MAFISADI WENZAKE KWAMBA WAMEMTUMA ILI AGOMBEE, UKIANGALIA ILE HUTUBA YA LOWASA NA ROSTOM JUU SLAA, NI MANENO YALEYALE CHENGE AMEYATUMIA KUMTOLEA UVIVU SITA.
    MAJINA YATAKAYO PITISHWA NI ANNA ABDALLAH(MKE WA SPIKA WA ZAMANI MSEKWA)ANNA MAKINDA(NAIBU SPIKA)NA JOB YULE MBUNGE WA DODOMA.

    ReplyDelete
  14. Jamani mbona mnaongea kama vile ccm imeshamchagua Chenge? Kuna wengine waliochukuwa forms. Kabla nilisema ningemtaka Slaa apite, lakini kutokana na wingi wa wabunge wa ccm sijui kama atapita. Ukweli ni kwamba Sita amekuwa polarizing figure katika CCM. Ili chama kiweze kutawala nchi lazima kiwe na mshikamano siyo in a negative sence. Kwa maoni yangu ningependekeza mama Makinda. Tumemuona uwezo wake alifanya kazi nzuri ya unaibu Spika. Tumechoka kuongozwa na wanaume. Msiniseme jamani hayo ni maoni yangu.

    ReplyDelete
  15. Kwa kweli aliyesema Anna Abadala ni spika kapatia,Jana Makamba kakatngaza majina ya wanawake akijidai anafanya gender mainstreaming,tokea lini Makamba au CCM wamejipambanua kutetea wanawake,navyojua CCM inajikaanga kwa mafuta yake,wakikaa vibaya Marando anakuwa spika.Pia naona fitina wameianza mapema safari hii,yetu macho na masikio najua wengi watakuwa punished kwa kisingizio cha kuikosesha kura CCM,CCM ikiendelea kumkumbatia Makamba na Kinana ndio kiama chao,stairi yao ya kuendesha chama kwa fitna imepitwa na wakati,pia kwa umri wao na mawazo yao hawawezi ku reason na kupambana na challenge za kizazi kipya,hapo ndio mwisho wa fikra zao.You can not teach the old dog new tricks,CCM jipange sawa saw vinginevyo 2015 BAI BAI.

    ReplyDelete
  16. Msongombane jamani mbona spika wa bunge ameshajulikana kuwa ni Anna Makinda wamefanya hivyo kwa makusudi ili bunge la 2010 liongozwe na mwanamke ndio maana hakuna mwanaume hata mmoja Sitta, Chenge hawana chao la msingi ni kuangalia huyo mwanamama ataongoza kikamilifu hilo bunge? Bila kujali upendeleo wowote? Yote tutayaona baada ya kuchaguliwa hao wa mama nani atakuwa juu zaidi.

    ReplyDelete
  17. Wewe Muta Said, kama wewe kweli ni mwana ccm halisi huwezi ku-suport alichokifanya Chenge. Ni kweli Nyerere asingefurahi na angetupa form yake kweny kapu. unaposema Daniel John kasema umbeya na kama anamtaka Sitta arudi basi hakukuwa na haja ya watu kuchukua form, mbona fedha za mlala hoi, maskini mtz zimeangamia bure kwenye kampeni wakati wakijua jk ataingia tena madarakani kwa gharama yoyote kwa kutumia taasisi za serikali na vyombo vya dora na usalama wa taifa ukageuzwa kuwa usalama wa ccm? kwani siri iko wapi? Kama matokeo yaliisha pangwa kwanini kuharibu fedha za mlala hoi? Nani asiye jua kama kura zimeibwa, kawaulize waliokuwa katika vituo (vyanzo vikuu vya takwimu) na observors utapata jibu, lakini jibu unalo moyoni mwako unajua kilichofanyika ila ni aibu kwenu. Kila lenye mwanzo lina mwisho. Isije ikawa ya Mhesh. Mkapa, kipindi cha mwisho ndipo wanachukua chao mapema, wa tz tuwe macho.

    ReplyDelete
  18. The farmer, wewe unaonekana wazi ni fisadi. Hebu jaribu kuwaza si watu/wabunge wa ccm tu wanaompenda Sitta, kwa sababa interest zake si za ccm peke yake, wala si mbinafsi, bali interest zake ni za kitaifa, ndio maana kama unafuatilia watu walio wengi wanasema 2015 anfaa kuwa rais. Wewe umepitwa na wakati tena huna jipya kama uko kinyume na the majority.

    ReplyDelete
  19. pole mshikaji mbio za sakafuni uishia ukingoni,mwisho wa ccm ndiyo huu.marando anachukua uspika kwa ulaini.hii ni pius msekwa kwa dhana yake ya kiimla aliyokuwa nayo tanu hapo hawali.yeye ni mrengo wa mafisadi bwana.

    ReplyDelete
  20. Nashangaa sana mtu wangu.mchapakazi kwa ajili ya watanzania wamememtupa na kumchinjia baharini wakidhani wamemueza mr sita,wanasahau watanzania kwa sasa siyo wale wa enzi ya picha na giza.wataumbuka kesho saaa sita mchana baada ya spika kutangazwa rasmi kutoka chama cha upinzani.
    lakini huyu mdudu makamba anajua madhara ya mafisadi wanaomtumia kwenye cheo alichonacho?
    tunamuomba mwenyekiti wa chama cha ccm aangalie huyu mtu anaweza kuleta madhara nchi hii.

    ReplyDelete
  21. Kweli ccm kaeni chonjo, kuwakingia kifua mafisadi, uonevu katika kura za maoni,kuchakachua kura, kuwachukia waadilifu na watenda haki, siku zaja tena zaja upesi ambapo Mungu atawapokonya mamlaka na kuwakabidhi watenda haki. Mungu amewaacha ccm wajikaange kwa mafuta yao wenyewe ili watakapoiva, wapinzani waje kutafuna na kumeza. Sitta usife moyo katika kipindi hiki cha majaribu ya mafisadi, kusulubiwa kwako ndio kunazidi kufungua milango ya ukombozi wa kweli wa watanzania.

    ReplyDelete
  22. Wewe unayemsema Slaa eti katoka kanda gani,una mawazo mgando,hujui utokako wala uendako.Ubaguzi umekujaa,mtu makini haijalishi kanda anayotokea,na unaposema Mzee Mtei yuko hivi na vile je huko Mwanza na Musoma nao wanatoka kaskazini?.Fikiri vizuri na ulitegemea alipoanzisha Chama apate wanachama kamili nchi nzima?Lazima aanzie nyumbani ndio asambae nchi nzimz kama unavyoona sasa.Jamaa wanakuja na hakuna wa kuwazuia,we lala na ufisadi wako tu badala ya kujibu hoja unakurupuka kuleta ubaguzi eti kwa ajili ya eneo analotokea mtu.Wewe huenda sio Mtanzania unatakiwa ujiunge na wasio watanzania wenzako.Siasa za ukanda,ukabila,udini sio za kitanzania,peleka Somali,Kenya,Uganda,Burundi ulikotokea sio kwetu.Chenge amechemka under room temperature inabidi apoozwe kwanza.

    ReplyDelete
  23. Haya mambo yanapangwa na Mungu,huenda anamwepushia jambo zito ambalo asingeliweza,hivyo atafutwe mwenye kuweza.Sitta kukosa isiwe taabu tumjaribu mwingine tuone umahiri wake.Miaka 50 tumepita katika mikono mbalimbali na huyu naye atapita.Huenda ili njia iwe rahisi kuwaondoa mafisadi tumeletewa huyu ili tupite kirahisi bila kipingamizi.Sitta ni kiongozi wa watanzania,waliopendekezwa ni kwa masilahi ya kikundi kidogo cha watu i.e.wenye meno ya kuila nchi.Hivyo Sitta asingeweza kulisimamia jambo hili.

    ReplyDelete
  24. Nashauri ndg yangu na mzee wangu SITTA AUKATAE UWAZIRI KAMA ATATEULIWA NA RAISI JK.ATAMPAMBA KWAMBA ANATAKA AMSAIDIE KWENYE CABINETI KUMBE NDO ANAMALIZWA KABISA.ABAKI MBUNGE WA KAIWADA

    ReplyDelete
  25. MZEE SITTA AKICHAGULIWA UWAZIRI AKATAE,TABIA ZA KUWANYANG'ANYA WATU HAKI ZAO NA KUWAHARIBIA KISHA KUWATUPIA VYEO VIDOGO KAMA MATAULO YA KUFUTIA JASHO LAZIMA IKOMESHWE.KAMA ALIRUHUSU UKAANGWE NA CC YA CCM MWAKA JANA,NA AMERUHUSU UTOLEWE KTK USPIKA.USIMWAMINI KWA YAJAYO,KAA PEMBENI NI YOTE YAACHE,ILA MAADUI ZAKO WAJUE KUWA SAUTI YA WATU NI SAUTI YA MUNGU TUNAKUOMBEA NA WAO WATAUMBUKA TU!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  26. dont worry everything will be alright

    ReplyDelete
  27. Huyu anayeuliza sababu ya mtei kufukuzwa CCM anaonekana hajasoma shule kabisa. Anajua aliye design logo ya benki kuu ni nani? Kilichomtoa Mtei CCM wakati ule ndicho hicho ilicho kuja kukubali serikali wakati wa Mwinyi- Masharti ya WB and IMF! Mzee Mtei alipingana na Nyerere kuhusu suala la kukuballi masharti hayo tofauti na Nyerere!!!! Nani alikuwa sahihi???
    Kitu cha wazi cha kujua ni kuwa Tanzania ni ya watu wote, ujanja ujanja wa kudhani genge la watu fulani ndiyo limepewa mamlaka ya kukamua watu maskini kwa kodi na kujilipa posho kubwa milele haujawahi kuendelea milele. Walikuwepo kina Chiluba, Kina Moi, Kina mzee wetu Kaunda, wapo kina Mugabe nk. Tutaona mwisho wake. Dawa ya CCM kuwepo ni kwanza kutambua kuwa serikali haina mali, mali ni za watu. serikali inapewa tu dhamana ya kuzigawa na kuzipanga kwa niaba na kwa faida ya wananchi, wenye mali hizo. Ni aibu kwa CCM kuendelea hata kutaja tu jina takatifu la Nyerere!

    ReplyDelete
  28. CCM haiwezi kukubali kumkumbatia mtu ambaye anaweka maslahi yake kwanza kuliko ya chama na kutumia mabega ya wenzake kujipandisha yeye kisiasa. Kama kweli yeye ni mpambanaji wa ufisadi kutokuwa spika si mwisho wa mapambano bado ccm imempa Sitta nafasi kubwa zaidi ya kupambana na mafisadi akiwa ndani ya ccm au chama cha upinzani. hajazibwa mdomo. by kilomo chohonza

    ReplyDelete