10 November 2010

Nafasi ya Pinda yazua hofu mpya.

Vigogo CCM waanza kuimezea mate, wajipanga.
Kikwete kuunda baraza 'dogo' la mawaziri.

Na Tumaini Makene
WAKATI duru za siasa za Tanzania zikielekezwa mjini Dodoma ambako wiki hii itajulikana mbivu na mbichi juu ya nani atakuwa spika, naibu wake na waziri mkuu, wachambuzi wa
mambo wameanza kudodosa Baraza la Mawaziri la Rais Jakaya Kikwete, katika awamu yake ya pili na ya mwisho ya utawala, huku nafasi ya waziri mkuu ikimezewa mate na vigogo.

Duru ndani ya serikali iliyomaliza muda wake, hususan sehemu ya baraza la mawaziri na katika mtandao wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) zinasema kuwa kuna uwezekano mkubwa wa Rais Kikwete kuja na kile walichokiita 'Baraza la Mawaziri la Slaa', wadodosaji hao kutoka ndani wamelijuza Majira kuwa baraza la namna hiyo litakuwa na sifa kuu tatu.

Wamezitaja sifa hizo kuwa ni; Kwanza baraza dogo likiwa na mawaziri wachache huku kazi nyingi za serikali zikifanywa na watendaji kama vile makatibu wakuu na wakurugenzi wa idara na taasisi mbalimbali, pili likipatikana kwa kutegemea utendaji kazi wa mtu zaidi, bila kujali eneo anakotoka mhusika wala ukaribu wake na raia, lakini kwa kujali uzoefu wa mtu katika masuala ya uendeshaji wa serikali.

Itakumbukwa kuwa wakati akitafuta wadhamini ili ateuliwe na chama chake kuwa mgombea urais na hata wakati wa kampeni, Dkt. Willibrod Slaa CHADEMA alikuwa akisema moja ya vipaumbele vyake ni kupunguza ukubwa wa serikali, ambapo alitaka katiba ya nchi iwe na kipengele cha idadi ya mawaziri, huku yeye akiahidi mawaziri wasiozidi 20 kwa baraza zima.

Alipata kusikika akisema kuwa uwaziri haupaswi kugawiwa kwa kufuata kanda, ili kuwaridhisha watu wote wa kila eneo nchini, bali msingi mkubwa unapaswa kuwa ni uwezo wa utendaji kazi wa mtu.

Wachambuzi hao wameliambia Majira kuwa kuna uwezekano mkubwa Rais Kikwete akaamua kuepuka kuteua mawaziri wake wa awamu hii kwa misingi ya kujuana au urafiki kama ilivyokuwa inaelezwa katika baraza lililopita, wakidai kuwa hali hiyo ilimgharimu katika utendaji kazi wa serikali yake na yeye mwenyewe kwa miaka mitano iliyopita.

"Huyu bwana anaweza kuja na baraza la mawaziri la Slaa, maana kwa kweli hii staili ya kuchagua mawaziri wengi, kwa kujuana, hata serikali ikaitwa ya kishikaji au kutaka kila kanda au mkoa nchi hii utoe waziri umeligharimu taifa kwa kuwa na mawaziri wasiokuwa na uwezo kabisa, kama...(anataja jina la mmoja wa mawaziri vijana ambaye pia amepita ubunge).

"Lakini hiyo itategemea na msimamo wake, maana tayari kumeanza kusikika minong'ono kuwa kuna watu wanapigana, hawalali usiku na mchana kuhakikisha baadhi ya mawaziri hawarudi katika baraza au wasirudi katika wizara walizokuwa nazo awali hata kama wana uwezo.

"Hii yote ni mikakati ya kundi la wana mtandao wanaopanga safu zao sasa serikalini kujiandaa na uchaguzi mkuu 2015," kilisema chanzo chetu kikiomba kuhifadhiwa jina kutokana na ukaribu wake na watu serikalini na CCM.

Aliongeza "Hawa watu (wana mtandao) mpaka sasa wanapigana na wanatoa mbinyo kweli kweli kuhakikisha Kikwete haendelei na Pinda (Mizengo, waziri mkuu aliyepita) katika nafasi yake, wanataka akae mtu wao hapo, wakishaweka itakuwa rahisi pia kuweka baadhi ya mawaziri katika sehemu fulani fulani, hasa inayolengwa ni Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

"Wizara hiyo sasa inaonekana kuwa ni 'dili', maana wanahisi kila mtu anayekaa pale kwa muda mrefu anakuwa njia pana ya kwenda ikulu kuwa rais, kama ilivyotokea kwa Mkapa (Rais Mstaafu Benjamin) na kisha kwa Kikwete. Wanajipanga kuhakikisha wanaweka mtu wao, kama si hivyo basi atakayepewa asiwe na ambition (tamaa) ya kwenda ikulu, ndiyo maana hawako radhi Membe arudi hapo lakini wako tayari apewe hata Profesa Anna Tibaijuka," alisema kwa kirefu mtu huyo.

Kwa mujibu wa chanzo hicho, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, sasa imegeuka kuwa lulu, ikionekana kuwa ni ngekewa au ngazi ya kupandia kwenda ikulu, ikitokea mtu amekaa katika wizara hiyo kwa muda mrefu, hivyo inapiganiwa huku kundi la wanamtandao lililoasisiwa na Rais Kikwete na rafiki zake tangu mwaka 1995, lililoko ndani ya serikali na CCM, likiimezea mate.

Mwanazuoni wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Bw. Bashiru Ally alisema uteuzi wa baraza la mawaziri unategemea mambo kadhaa ukiwemo uzoefu, uadilifu, jinsi, usikivu wa mtu na agenda ya rais katika kipindi husika.

"Suala la uadilifu limekuwa likiachwa na CCM katika suala la uteuzi na tumekuwa na chaguzi mbili ndani ya serikali moja. Yaani wakati tunasubiri uteuzi wa rais, kuna watu wanajipanga pembeni kutaka nani akae sehemu gani ili kujipanga na uchaguzi wa mwaka 2015," alisema Bw. Ally ambaye aliweka wazi kuwa hatashangaa kuona baraza hilo linakuwa na wanawake wengi, kwa kuwa wameonesha kuweza.

Msomi huyo alizungumzia nafasi 10 anazoepewa rais kuteua wabunge kuwa mantiki yake ni kumsaidia rais kupata watu ambao hawawezi kuomba kura na wakapewa lakini ni watu wazuri kwa utendaji, hivyo zikitumika vizuri zinaweza kutoa mawaziri wazuri.

Mbali na Bw. Ally, vyanzo zaidi vimesema kuwa wengine 'watapewa' wizara kwa lengo la kuwamaliza kisiasa.

"Iko mikakati ya kuhakikisha baadhi ya watu ambao watakuwa tishio kwa kundi la wanamtandao kwa urais mwaka 2015, wanapewa uwaziri katika wizara zenye kashfa au zitakazoundiwa zengwe la kashfa, kisha wachafuke katika jamii na watemwe serikalini.

Huku jina la mtu atakayekuwa waziri mkuu likianza kudodoswa zikiwepo tetesi kuwa kuna 'mbinyo' Bw. Pinda asiendele, huku upande mwingine hasa wa wanaotaka Rais Kikwete amalize 'salama', ukitaka aendelee na waziri mkuu wake huyo kwa miaka mingine mitano kama alivyofanya mtangulizi wake, Mkapa. Tayari kuna majina yameanza kutajwa kuwa yanaweza kuingia barazani.

Ingawa majina yamekuwa hayaendi na vigezo, walau mpaka sasa vipo vigezo kadhaa ambavyo kutokana na kauli na mwenendo wa Rais Kikwete kwa miaka mitano iliyopita haviwezi kuepukika, kama vile ujana, usawa wa kijinsia. Suala la uzoefu serikalini limekuwa likiwekwa kando katika teuzi kadhaa kwa muda mrefu sasa serikalini.

Mpaka sasa majina yanayotajwa yanatokana na ama uhodari wa kuchapa kazi au ukaribu na Rais Kikwete, kama vile Profesa Anna Tibaijuka, Bernard Membe, Lawrence Masha, Edward Lowassa, Emmanuel Nchimbi, Zakia Meghji, Samuel Sitta, Rostam Aziz, Profesa Juma Kapuya, Dkt. John Magufuli, Profesa Mwandosya na Pinda.

24 comments:

  1. Kupunguza Baraza la Mawaziri tu hakutasaidia kama Rais Kikwete hatakomesha tabia yake ya matanuzi na kuihusisha familia yake kutumia rasilimali za nchi.
    Familia ya Kikwete imeligharimu taifa hili gharama kubwa kulikoza ma Rais wote waliopita.
    Tanzania ni nchi masikini isiyowezakumudu matumizi makubwa ya familia nzima ya Rais kama ilivyoshuhudiwa katika awamu ya kwanza na ambayo ilikera wakati wa kampeni zake ambazo bila aibu familia nzima ilitumia rasilimali za serikali "kumfanyia" kampeni.
    Mlipuko wa bei za bidhaa mbalimbali kupanda unaweza kuwa kielelezo cha kuyumba kwa uchumi. Kwa kifupi Rais Kikwete ajifunze toka kwa sera za mwenzake Slaa na kitendo chochote cha kumbeza au kumnyanyasa kitasababisha maafa makubwa kwa CCM mwaka 2015.

    ReplyDelete
  2. Muhimu kupunguza ukubwa wa baraza la mawaziri, kuzuia magari ya kifahari yasinunuliwe tena,semina zisizo na msingi ni jukumu la idara ya maelezo watume waraka kupitia mitandao
    mfano miaka iliyopita semina kwa baraza la mawaziri halafu ikaja makatibu wakuu, halafu wakuu wa mikoa baadae wakurugenzi ni gharama kubwa sana,na kuzuia mlipuko wa bei za mahitaji,kuhusu Mama Salma na familia ktk kampeni hakuna gharama kubwa kiasi hicho, unachodai toa vielelezo mwaka 2005 zilitumika kiasi, gani na mwaka huu kiasi gani kwa wapiga debe tuu!!acha ya mgombea mwenyewe na mgombea mwenza,Sidhani kama hilo la kumbeza au kumnyanyasa Dr, Slaa hilo halipo wala usitegemee,illa yeye mwenyewe labda aanze kuleta chokochoko,watu ni WASTAARABU sasa ni wakati wakujenga Nchi

    ReplyDelete
  3. Napenda baraza dogo na linalopambana na Ufisadi. Napenda wawajibikaji na Mawaziri wenye maamuzi mazito. Napenda Mawaziri wanaopenda kushughulikia mambo yaliyoshindikana na kuibua mikakati mipya. Napenda Waziri mkuu mkali na asiye muoga mwenye maono na muelekeo wa Dr. Slaa au Dr. Magufuli. Napenda waziri wa mambo ya nje mwenye diplomasia ya juu na msomi ambaye anatafuta mazuri ya nje na kuyaleta hapa na anayeweza kuthibiti mabalozi watembezi au watalii. Napenda uwajibikaji wa dhati yaani waziri anayeshirikiana na wananchi katika shughuli za kimaendeleo ikibidi ashike jembe! Walipatikana wachache nao ni Sokoine na Nyerere! Napenda Rais mwenye maono kama Lula wa Brazil au Prime Minister Raila wa Kenya. GOD BLESS TZ. Out!

    ReplyDelete
  4. Ni vyema tukawa na baraza la mawaziri wachache zaid na hata ikiwezekana 20 bila kuadhiri idara muhimu za serikali,kupunguzu matanuzi na kuwajibika zaidi katika afya,makazi,elimu na ajira.sihitaji rais mhemea vibaba,nahitaji rais mbunifu na mwenye mwono wa hata miaka 100 mbele.nahitaji rais makini zaidi na asiyefumbia macho uovu wa aina yeyote lakini mwenye kuheshimu sheria na haki za binadamu.rais wa namna hii ataweza kusimamia vizuri baraza la mawaziri wachapa kazi.Ningependa rais ambaye atakaa na watendaji wake kuweka mikakati ya kuletea nchi yetu heshima na siyo omba omba.Mwisho baraza la mawaziri litokane na sifa ya mtu na hasa utendaji kazi uliotukuka.MUNGU IBARIKI TANZANIA

    ReplyDelete
  5. Ni vyema akapunguza baraza la mawaziri kupunguza gharama za kuwahudumia na matanuzi huu ni wakati wa mabadiliko!

    ReplyDelete
  6. Baraza dogo la mawaziri ni sahihi kwa sasa kulingana na hali ya uchumi wa nchi yetu. Ni vyema tukajifunza hata kwa majirani zetu walivyofanya mageuzi ya kiuchumi ikiwemo kubana matumizi na kutumia vyema raslimali za nchi hii ambazo ni nyingi isipokuwa zinakosa usimamizi wa dhati kutokana na dhana mbaya ya ubinafsi miongoni mwa watendaji wanaopewa nafasi ya kuwatumikia watanzania maskini. Isitoshe baraza litakoloundwa liangalie uwezekano wa kuondoa kilio cha umaskini kwa mtanzania. Mungu ibarika Tanzania.

    ReplyDelete
  7. Tunamuomba rais awachague mawaziri kutokana na uhodari wao sio urafiki, wasichaguliwe watu kwa ajili ya kulipa fadhila rais azingatie udogo wa baraza lakini lenye ufanisi. Awachague watu mahiri wanaofahamu kuwa uchumi wetu hauridhishi shilingi inapoteza thamani kila siku bidhaa zimepanda bei karibu mara tatu tangu kuanza kwa awamu hii ya uongozi. Chonde rais unaovijana wazuri na waaminifu kama Pinda, Magufuli wanaofanya kazi bila kujali kupata 10% wachague hao ili utakapoiacha nchi hii watu wako wakukumbuke

    ReplyDelete
  8. Dr Slaa sasa yuko nje ya ulingo wa siasa. Mambo yake mengine yalikubalika na Watanzania. Vile lengo ni kujenga nchi yetu yale ya Slaa mazuri yasije yakabezwa yafanyiwe kazi. Ikiwezekana tusimpoteze kabisa sisi kama nchi, apewe nafasi ya kuchangia. Rais mmoja wa Marekani simkumbuki vizuri alimchukua mpinzani wake kwenye serikali na alipoulizwa kwanini alisema upinzani wake ulikuwa mkali kiasi siwezi kuwanyima Wamarekani mchango wake katika kuhudumia taifa.

    ReplyDelete
  9. Kwa kweli kama Kikwete anaipenda Tanzania, asiogope kutumia mawazo ya Slaa na CHADEMA. Ikibidi atafute ushauri zaidi namna ya kulipunguzia taifa mzigo wa mawaziri wengi.
    na akubali katiba iandikwe upya. Tume ya uchaguzi iundwe kwa katiba mpya. kama anaipenda CCM, aache mtindo wa kuwachukua wabunge kuwa mawaziri, kwa vile kufanya hivyo kunawanyima wananchi kuwakilishwa bungeni. wabunge wanatakiwa waiwajibishe serikali. Wanatakiwa kufuatilia utekelezaji wa sheria walizozitunga, sio wao kuzitekeleza.

    ReplyDelete
  10. Huyu bwana Kikwete haeleweki kabisa, usishangae mwanae Ridhiwani akapewa ubunge wa viti maalumu na kurithi nafasi ya Masha

    ReplyDelete
  11. Ni kweli upunguzaji wa baraza la mawaziri unaweza kuongeza ufanisi na kuwapa uwezo watendaji kufanya kazi kwa upana zaidi. Kwa muda mrefu Tanzania tumeshindwa kuwa na mipango mizuri ya Michezo.JK ameanza vizuri katika katika miaka 5 ili aweza kuendelea vizuri kwa kuleta maendeleo ya michezo ushauri wangu ni kuweka wazoefu katika nyanja hizo hasa Mawaziri wanaomaliza muda wao sasa wao ni wataalamu wa michezo hasa Mhe.JB na waliendesha vizuri wizara hiyo na inaweza tenganishwa na Habari iwe Wizara ya Michezo na Utamaduni pekee kama enzi za Mwalimu wakati wa Waziri Mgonja Chediel. JK juu!!!

    ReplyDelete
  12. Tafadhali Waheshimiwa zingatieni mishahara ya watumishi iendane na elimu zao.Hiyo mishahara ya TGS D I kwa watumishi wenye degree ni aibu tupu.Sijui wote tujitoe muhanga na kutujitosa kama mr II na kumpongeza Shibuda? Kabla wabunge hawajachaguliwa kuwepo na vigezo vya elimu tosha sababu ni aibu tupu kwa wabunge wengi walio wengi.

    ReplyDelete
  13. kweli ridhiwani aweza pewa nafasi ya masha,lol!

    ReplyDelete
  14. Napenda kuunga mkono mawazo yaliyotolewa na wengi kubwa zaidi likiwa kupunguza matumizi kwa baraza dogo lenye watu makini,waaminifu na jasiri wenye kusimamia ukweli na haki kama Dr.amagufuri.

    Natoa mfano wa Dr. Magufuli kwa sababu amefanya mambo mengi yanayokumbukwa na watanzania wengi kama kusimamia ujenzi wa barabara za lami zilizopo kwa lengo la kuunganisha Tanzania nzima.Sasa tujiulize tangu aondoke Wizara ile zimejengwa ngapi?

    Tunasubiri baraza hili makini.


    Bernard Zelamula
    MBA Student
    University of Birmingham
    United Kingdom.

    ReplyDelete
  15. mi nafikiri hakuna mjadala sana wa kuongea hapa
    naomba mheshimiwa rais ampe tena miaka mitano mingine spika Sitta na Mizengo pinda kila mmoja aendelee na post yake,kwani nafasi hizi mbili ni chachu kubwa ya maendeleo ya Taifa letu na zinahitaji akili sana, busara,unyenyekevu,fikra nyingi na pia unatakiwa uwe ni mtu usiesomeka kirahisi,unakuwa mchapa kazi ambaye undefined.MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE.

    ReplyDelete
  16. KWANZA KWA WALE ULOWATAJA ONDAO WAISLAM HATUWEZI KWA NA VIONGOZI WOTE WAKUU TANZANIA KUWA NI WAISLAMU.PINDA HAFAI NI MPOLE MNO ANAOGOPA KUNDI LA MTANDAO HASA KUJIBU TUHUMA ZA MEREMETA.SAFARI HII TUNATAKA WAZIRI MKUU AWE MWANAMKE NA ATOKE KANDA YA ZIWA, BILA HIVYO TUTAIANGAMIZA CCM.

    ReplyDelete
  17. Nadhani wajuzi wa mabo mmemsahau kamanda wa ufisadi ambaye anaweza kupewa nafasi hii,bila shaka huyu ni MHE.ANNA KILANGO MALECELA asiye na chembe ya dosari

    ReplyDelete
  18. mwandishi umeingiza ushabiki.kusema baraza la slaa sio sahihi.kwanini usiseme baraza la lipumba kwani alianza kulisema hili tangu mwaka 2000.Au una ajenda ya siri?
    Acha kumkatisha tamaa raisi wetu.Kama ataunda baraza dogo tutafurahi na litakuwa la raisi Kikwete si la mwingine.
    Huyu ni mtu wa watu,anasikia ushauri sio jeuri.Na kama atafuata mazuri ya wapinzani basi hiyo ni ishara kuwa ni kiongozi mzuri wa kupigiwa mfano.

    ReplyDelete
  19. Ndugu zangu, naona tunachanga sana mambo, mara twaleta udini, mara ukabila, mara ujinsia na mara nyingine maeneo ya KiJiografia, kwa kweli mambo hayo si ya maslahi kwa taifa letu hata kidogo, tuchague au tupendekeze viongozi wetu kufuatana na sifa njema za uongozi bila ya kujali dini, kabila,jinsia au eneo la mhusika. Kiongozi msomi, mwenye uzoefu, muadilifu, mpenda haki na kuchukia maovu, aliye jasiri, anayeweza kukabiliana na hali zote kwa hekma na busara, mwenye wivu wa maendeleo na anayehisi hisia za raia.

    ReplyDelete
  20. Napenda kutoa ushauri kidogo kwa Dr. J. Kikwete aige mfano wa Rais Kagame wa Rwanda, Tazama alivyopambana na kuirudisha Rwanda katika chati, amebana matumizi, ameondoa ununuzi wa magari ya kifahari yanayotumiwa na wabunge, mawaziri, makatibu wakuu, Wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya. Na Sasa Rwanda imekuaa kiuchumi na kuitupilia mbali Tanzania yenye rasilimali nyingi. Najua sasa ivi anajiandaa na kusitaafu hataomba tena kula, lakini na hayo hayazingatia

    ReplyDelete
  21. Huwezi kuilinaginsha Rwanda ambayo hata ukiitazama ramani yake ukubwa wake ni sawa na mkoa mmoja wa Tanzania, na watu wake ni wachache.

    Tena usiseme usilolijua au unataka na sisi tukavamie Kongo kwenda kupora madini ya kutengeneza cells yenye bei kubwa kuliko gold? Watu wengine wanakurupuka tu na kujifananisha na tusolingana nao. Ukubwa wa nchi hii peke yake ni changamoto tosha kuitawala!

    ReplyDelete
  22. We mwandishi umechemsha. Unapowataja Masha,Nchimbi unachefuwa. Kubwa gani wamelifanyia Taifa?Munaandika porojo za mitaani subirini JK awape surprise.

    ReplyDelete
  23. Kiwete usiogope maneno ya wavimba macho,angalia Mseveni alivyofanya uongozi wa familia mbona nchi inaenda,mpe RIZWANI wizara ya mambo ya ndani ya nchi,Mama Salma mpe wizara ya elimu na ufundi,Miraji/Siraji mpe waziri wa michezo,January Makamba waziri wa habari,Hussein Mwinyi waziri wa Afya,Zainabu kawawa na binti sokoine naibu waziri bila kusahau wana mtandao wote,watapiga kelele we lakini nchi itakwenda na miaka mitano ikiisha zigo unalitua na kumuachia mwingine.

    ReplyDelete
  24. Naomba nanakuomba saana raisi wetu mpendwa ukitaka mambo yako yaende vema usimpe tene uwaziri huyu kapuya...........sina zaidi

    ReplyDelete