09 November 2010

Shein ateua wanane baraza la wawakilishi.

Na Ali  Suleiman, Zanzibar

RAIS wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein amewateua watu wanane kuwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, wakiwamo manaibu mawaziri watatu wa serikali iliyopita ya
Rais Jakaya Kikwetwe.

Rais Shein amefanya uteuzi huo kwa mujibu wa katiba kifungu 66 ya mwaka 1984.

Manaibu mawaziri watatu waliokuwa katika serikali ya Rais Kikwete, Balozi Seif Ali Iddi (Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Mohamed Aboud Mohamed (Afrika Mashariki) pamoja na Bw. Omar Yussuf Mzee.

Wengine walioteuliwa ni Bw. Ramadhan Abdallah Shaaban, Bi. Zainab Omar Mohamed, Dkt. Sira Ubwa Mamboya na wengine wawili kutoka katika Chama cha Wananchi (CUF), Bi. Fatma Abdulhabib Fereji pamoja na Bw. Juma Duni Haji.

Bi. Fatma Fereji alikuwemo katika Baraza la Wawakilishi lililopita akiwa Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe pamoja na Juma Duni ambaye aliteuliwa na Rais Mstaafu, Amani Abeid Karume.

Bw. Aboud aliwahi kuwa mjumbe wa Baraza la Wawakilishi tangu mwaka 2000 akiwa Mwakilishi wa Jimbo la Wawi, Pemba, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, na baadaye naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, wakati Bw. Mzee alikuwa Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi katika Serikali iliyopita ya Jamhuri ya Muungano.

Alikuwa Mbunge wa jimbo la Kiembesamaki katika kipindi kilichopita ambapo mwaka huu aliacha kugombea nafasi hiyo.

Katika ya walioteuliwa na Rais Shein, sura mpya ni Dkt. Mamboya pekee ambaye alikuwa mkuu wa kitengo cha kupambana na ugonjwa wa kifua kikuu na ukoma katika hospitali ya Mnazi Mmoja, na baadaye alifanya kazi katika mashirika ya kimataifa ya afya.

Masikio ya wananchi wa Zanzibar yanasubiri uteuzi wa makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ambaye atakuwa kiongozi wa shunguli za Baraza la Wawakilishi na
Serikali kutoka katika CCM. Tayari CUF wamewasilisha jina pekee la Maalimu Seif Sharif Hamad kwa ajili ya uteuzi wa Makamu wa Kwanza wa Rais.

1 comment:

  1. kama bora amani ni sawa! lakini kimsingi serikali ya umoja huo ni gharama kwa nchi kama zanzibar! RAIS, MAKAMU 1, 2. ni mlolongo wa uongozi unaotia hasara nchi. yaani hii ni balaa tu! nchi ndogo viongozi kibao na wanalipwa pesa za walipa kodi! hii ni aibu.
    pia kikubwa zaidi ni zanzibar ni kuinyonga Tanganyika kwa vile viongozi wengi wa kitaifa wanatoka zanzabar huu si mfumo mzuri wa uongozi, ebu ona MAKAM WA RAIS BARA TOKA ZANZABAR,RAIS SHEIN, SELFU, ALI HI NI KUTUNYANYA SISI WATANZANIA BARA!!!! Wote hawa wanalipwa mamillioni ya shillingi kwa mwezi na posho kibao, marupurupu kibao.
    KUNA HAJA KUBWA MUUNGANO UANGALIWE UPYA NA MFUMO WA UONGOZI. vinginevyo tanganyika tunaibiwa.

    ReplyDelete