09 November 2010

Ngulume atakiwa kuwasilisha nyaraka za rufaa.

Na Rabia Bakari

SERIKALI imemtaka aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Bi. Hawa Ngulume kuwasilisha nyaraka za rufaa kutoka kwa madaktari, ili Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii iweze
kushughulikia matibabu yake nje ya nchi.

Kauli hiyo ya serikali imekuja siku moja baada ya Bi. Ngulume kutoa malalamiko kupitia gazeti moja kuhusu ugonjwa unaomsumbua wa vichomi na mapafu, na kudai kutelekezwa na serikali pamoja na Chama cha Mapinduzi (CCM).

Akijibu tuhuma hizo, Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt. Deo Mtasiwa alisema kuwa, kwa mujibu wa taratibu za matibabu, wizara hutoa kibali cha kwenda kutibiwa nje ya nchi, endapo ikipata ushauri pamoja na nyaraka za rufaa  kutoka kwa madaktari wasiopungua watatu, na kwa bahati mbaya, Bi. Ngulume hakufanya hivyo.

"Alikuwa anashughulikiwa katika Taasisi ya Saratani Ocean Road, na huko ndiko alikotakiwa kufanyiwa kila kitu, ikiwa ni pamoja na kuandikiwa rufaa na madaktari wake, sasa ingekuwa vizuri mumuulize imekuwaje?" alisema Dkt. Mtasiwa na kuongeza "kwanini hawajamuandikia, nadhani hapo kutakuwa na tatizo la kimawasiliano, ni vizuri mngemtafuta mwenyewe (Bi. Ngulume) aweze kuelezea vizuri."

Aliongeza kuwa serikali haina tatizo katika kutoa kibali cha mtu kwenda kutibiwa nje, endapo taratibu zitafuatwa, na pia haina tatizo na suala la Bi. Ngulume kinachotakiwa ni kufuata utaratibu.

Kwa mujibu wa madai ya DC huyo, kuna kipimo alichotakiwa kufanyiwa Ocean Road cha kuwekewa mdomoni, ambapo ilishindikana kutokana na kutokuwa na pumzi, ambapo alishauriwa na madaktari kwenda India kwa kuwa wana vipimo mbalimbali, lakini haikuelezwa alifikia wapi katika mchakato wa kufuata ushauri huo wa madaktari.

12 comments:

  1. Too little too late. Mpaka alalamike kwenye media ndiyo mmkumbuke! Kweli CCM chama cha mafisi na mafisadi!

    ReplyDelete
  2. mlikuwa mnajua kila kitu kuhusu kuumwa kwake ila ni utaratibu wa ccm miaka yote kumjali mtu akiwa vizuri na si kwenye matatizo

    ReplyDelete
  3. Hivi jamani kazi alizozifanya mama huyu hazionekani na ccm hadi afikie hali hii.Ama kweli tenda wema nenda zako.

    ReplyDelete
  4. Kumjali kiongozi ni pamoja na kufuata taratibu za nchi. Wizara ya Afya haiwezi kuvunja taratibu kwa sababu ni kiongozi. Cha msingi sasa Viongozi wamsaidie akamilishe taratibu hizo ili hatimaye akatibiwe ipasavyo.
    Pole mama Ngulume Mungu atakusimamia.

    ReplyDelete
  5. Bi mkubwa Ngulume, ukiona CCM wanazidi kukusumbua kuhusu matibabu ya nje ya nchi nenda Ihefu kwa yule mganga wa jadi mjasilia mali atakusaidia, hata sisi wenzio tukiambiwa hospitali dawa hamuna jambo ambalo nilakawaida, huwa tunatibiwa na mitishamba.Siunaona Dk.Mtasiwa anavyokuwekea kiwingu? wala hajali mchango wako mkubwa kama kada wa chama katika kuwaongezea wafugaji umaskini wa kipato na waakili.

    ReplyDelete
  6. ama kweli hujafa hujaumbika,mkuu wa wilaya!!kupata matesa ya namna hiyo vipi kama ni raia wa kawaida ambaye hajui namba ya magazeti? si kufa kifo cha mbwa mwizi!
    nafikiri huyu mama ndiyo wale masalia ya baba wa taifa mwalimu nyerere!kwamba yeye si fisadi na wala hajawahi kufisadi!mkuu wa wilaya awe hoe hae namna hii!tangazeni ili wananchi tumsaidie ili apate matibabu!

    ReplyDelete
  7. Afuate tu utaratibu kama wengine na nafasi hiyo ya kwenda ataipata. kwanini mnamtaka asifuate utaratibu?

    ReplyDelete
  8. Matunda ya chichiem

    ReplyDelete
  9. Wakuu wa wilaya wengi ni makada wa ccm, acheni kumzingua mama huyu mbona pesa za kampeni mnapata sembuse uhai wa mtu?

    ReplyDelete
  10. Huenda hizo ni laaana za kuwapiga wafugaji faini zisizo halali katika zoezi lililoghubikwa na ukiukwaji wa haki za binadamu. Mama tumia zile elfu thelathini thelathini ulizowapora wafugaji Ihefu akiwemo mgombea wa chadema mbarali,bw Kazamoyo labda zitasaidia

    ReplyDelete