09 November 2010

CCM Musoma wapiga waandishi wa habari.

Benjamin Masese na Veronica Modest

SIKU chache baada ya kuapishwa Rais Jakaya Kikwete na kusema kuwa muda wa malumbanon umekwisha na kuwataka  waandishi wa habari nchini kutibu majeraha yatokanayo
na uchaguzi hali ni tofauti kwa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Musoma baada ya wafuasi wake kuwashambulia waandishi wa habari mkoani humo.

Waandishi ni kutoka katika wa gazeti la Uhuru na Mzalendo Bi.Ghati Msamba (32) na Bi. Eva-Sweet Musiba (35) wote wakazi wa Manispaa ya Musoma Mjini baada ya kukaa pamoja na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) huku wakipata vinywaji.

Akizungumzia tukio hilo, Bi. Msamba alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa tatu usiku eneo la Kivukoni katika Baa ya Busamba ambapo palikuwa na watu wengi wakiendelea kupata vinywaji.

Alisema kuwa wakati wanaingia katika baa hiyo kulikuwa na makundi ya watu wakiwemo wa CCM, CHADEAMA, CUF na wengine wakipata vinywaji na bila kujali itikadi za vyama waliamua kukaa meza iliyokuwa karibu na wafuasi wa CHADEMA kitu kilichokera wafuasi wa CCM.

Kati ya watu waliokuwepo katika baa hiyo ni Mwenyekiti wa Vijana Mkoa (UVCCM),Bw. Marwa Mathayo, dereva wa mbunge mteule wa Jimbo la Musoma Mjini Bw. Vicent Nyerere, aliyefahamika kwa jina moja la Bw. Simba, Naibu Meya wa Manispaa ya Musoma na aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mwisenge kupitia CCM, Bw. Daudi Misangwa, mmiliki wa baa hiyo Bw. Charles Koko na wafuasi wa vyama vyote vya siasa.

"Wakati tukiendelea kunywa tukiwa katika meza yetu ambayo ilikuwa na wafuasi wa CHADEMA bila sisi kuwajua baadhi ya watu walikuwa wakisema People na wengine kuitikia Power wakiashiria CHADEMA, ghafla hali ilianza kubadilika na kutoa matusi yaliyoashiria uvunjifu amani.

"Matusi yalielekezwa kwetu wakisema kuwa mnajifanya waandishi wa chama kumbe mnatushika miguu na ndio maana mlikuwa mnaripoti kwa upendeleo na tutawashugulikia...tulipohoji ndipo vurugu zilianza kwa kumkaba Meneja wa Baa Bw. Aprili Koko na wengine kuturukia na kutupiga,"alisema Bi. Msamba.

Waandishi hao walichaniwa nguo zao na kupigwa sehemu mbalimbali za miili yao na kuumia sikio, koo, kiuno, bega na mkono ambao ulipata mshtuko wa mishipa.

Hata hivyo waandishi hao walikimbizwa Hospitali ya Mkoa na wanaendelea na matibabu na hali zao zinaendelea vizuri.
wakati shambulia hilo likiendelea taarifa ziliwafikia Polisi Kituo cha Kati amabao walifika na kutuliza ghasia hizo ambapo waliondokana na waandishi hao kutoa maelezo na kupewa RB yenye namba MUS/RB/ 6431/2010 ya shambulio.

Tayari kesi hiyo imefunguliwa katika kituo hicho na kupewa namba ya kesi ni Mus/IR/4608/2010.

Hadi jeshi hilo linamshikilia Mwenyekiti wa CCM wa wilaya, Bi. Diana
Mkono ambaye ni kada wa CCM ambapo watuhumiwa wengine walikimbia.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Bw.Robert Boaz alithibitisha kutokea tukio hilo na kusema kwamba wahusika wote wanatafutwa ili kuchukuliwa hatua za kisheria.

No comments:

Post a Comment