LIVERPOOL, England
MACHO ya mashabiki wa soka nchini Uingereza, yameelekezwa katika mechi ya Ligi Kuu nchini humo kati Liverpool na Chelsea, itakayochezwa katika Uwanja wa Anfield
jijini London, leo.
Liverpool imekuwa na msimu mbaya katika ligi hiyo, lakini juzi kwenye michuano ya Ulaya (Europa), iliichapa Napoli ya Italia mabao 3-1, yote yakifungwa na Steven Gerrald.
Mahasimu wao, Chelsea, wameendelea kufanya vizuri katika Ligi Kuu England na kushika usukani na kufanya vizuri katika michuano ya Klabu Bingwa Ulaya.
Mshambuliaji wa kimataifa wa Uholanzi, Dirk Kuyt, anaweza kurejea uwanjani katika mechi hiyo baada ya kukaa nje kwa majeraha, wakati Lucas Leiva anatarajiwa kuanza katika mchezo huo.
Timu hiyo itamkosa Joe Cole, aliyehamia timu hiyo akitokea Chelsea, baada ya kuumia nyama za paja walipocheza na Bolton.
Kocha wa Chelsea Carlo Ancelotti, amethibitisha kuwa, nahodha John Terry, atarejea kwenye Uwanja wa Anfield kuikabiri Liverpool, ataungana na kiungo Frank Lampard aliyekosa mechi 12 za kikosi hicho.
Chelsea watakuwa katika nafasi nzuri ya mchezo huo, baada ya Florent Malouda kupona majeraha yake ya kifundo cha mguu, lakini hofu ni kwa Michael Essien anayesumbuliwa na kidole.
Mechi nyingine ya leo itawakutanisha Arsenal na Newcastle katika Uwanja wa Emirates, wakati Man City watakuwa ugenini dhidi ya West Brom Albion.
No comments:
Post a Comment