Na Daud Magesa, Mwanza
MFUNGWA wa Gereza la Butimba mkoani Mwanza ambaye hajatambuliwa jina lake anatuhumiwa kumlawiti mwanafunzi wa darasa la kwanza wa Shule ya
Msingi Butimba.
Akizungumza na waandishi wa habari mijini Mwanza jana ofisini kwake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Bw. Simon Sirro, alisema mtuhumiwa alitenda kosa hilo baada ya kumlaghai mtoto huyo baada ya kukutana njiani.
Hata hivyo Bw. Sirro hakuweza kutoa ufafanuzi kuhusu hatua zitakazochukuliwa na Jeshi la Polisi kuhusu tuhuma hizo.
Katika tukio lingine Bw Sirro alisema tukio la kwanza gari dogo la abiria lilimgonga mwenda kwa miguu na kusababisha kifo chake saa 3:00 usiku Novemba 7 mwaka huu wakati wakijaribu kuvuka barabara na mwenzake.
Alisema ajali hiyo ilihusisha gari lenye namba za usajili T 664 BLB ambalo lilimgonga Bi. Penina Starton (23) na kufariki papo hapo, pia mbali na kumgonga marehemu na kumjeruhi, Bw. Musa Mage (23) mwanafunzi wa shule ya sekondari Sengerema na kumsabashia maumivu mwilini.
Kwa mujibu wa Sirro dereva wa gari hilo aina ya Hiace Gerald Njau (40) anashikiliwa na jeshi hilo kwa kusababisha kifo cha mwenda kwa miguu huyo na majeraha kwa Mange na atafikishwa mahakamani baada ya taratibu za kipolisi kukamilika.
Katika tukio tatu, Bw. Sirro alieleza kuwa, Bw. Juma Mpola (38) mkazi wa kijiji cha Bufinda Kata ya Nyakamawa wilayani Geita aliuawa na wananchi wenye hasira kali kisha mwili wake kuchomwa moto.
Tukio hilo lilitokea katika kijiji hicho Novemba 6 mwaka huu saa 4:00
usiku, ambapo marehemu alikuwa akituhumiwa kuiba fedha tasilimu sh. 85,000 na simu mbili aina ya Nokia zenye thamani ya sh. 100,000.
Ilidaiwa kuwa alidaiwa marehemu alivunja kibanda cha duka mali ya Bw. Twaha Kalamba (50) na kuiba fedha hizo na simu.
sasa hiyo ni ajabu iweje mfungwa atembee njiani peke yake bila ya askari magereza, hao askari wana kazi gani,
ReplyDeletemfungwa kupewa fursa ya kutembea njiani na kulaghai na kufanya ngono, hiyo ni ajabu, sana wahusika wawajibike, sio mfungwa peke yake ila hata hao makamanda wazembeee