09 November 2010

CHADEMA yaalika wanaotaka uspika.

Na Shukrani Kawogo

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimewataka wanachama wake wenye nia ya kuomba nafasi ya spika katika bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
kujitokeza kuomba nafasi hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyosambazwa katika vyombo vya habari juzi na kusainiwa na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Bw. Hamad Yussuf, fomu za kuomba uteuzi zinapatikana makao makuu ya chama hicho.

Ilieleza kuwa fomu hizo zimeanza kuchukuliwa kuanzia juzi na mwisho wa kurudisha fomu hizo ni leo saa 10:00 jioni.

Aidha ilieleza kuwa kikao cha kuchuja na hatimaye kupitisha jina la mwanachama mmoja kitafanyika Novemba 10 na jina la mwanachama litakalopitishwa litawasilishwa kwa katibu wa bunge kwa hatua zitakazofuata.

No comments:

Post a Comment