05 November 2010

Kortini kwa tuhuma za kujeruhi .

Na Yvonne Mussa

MKAZI wa Tandale, Bw. Michael Edward (28) amefikishwa katika Mahakama ya Ilala kwa tuhuma za kumjeruhi, Bw. Ally Abdallah kwa kumpiga na jiwe kwenye
paji la uso na kumsababishia majeraha.

Akisoma shtaka hilo mbele ya Hakimu wa mahakama hiyo,  Bi. Flora Mujaya, Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Bi. Lucy Rutabanzibwa alidai kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo  Novemba 28, mwaka huu saa moja usiku katika mtaa wa Msimbazi.

Bw. Abdallah amekiri kosa hilo na amerudishwa rumande hadi  Novemba 17, mwaka huu hadi hapo kesi hiyo itakapotajwa tena.

Wakati huo huo, Mkazi wa Kariakoo, Bw. Joshua Mziku alifikishwa mahakamani hiyo kwa kosa la kujaribu  kumnyang'anya, Bw. Darshit Chohan baiskeli yenye thamani ya 200,000 na runinga.

ilidaiwa mahakamini hapo na Mwendesha Mashtaka huyo kwa kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo saa 8:00 mchana katika  mtaa wa Akhiri Upanga.

Mshtakiwa amekana shtaka hilo na amearudishwa rumande hadi Novemba 17 na kesi itakapotajwa tena.

No comments:

Post a Comment