09 November 2010

Hukumu ya wastaafu EAC leo.

Na Gladness Mboma

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania leo itatoa hukumu kuhusiana na hatima ya mafao ya Wazee wa Afrika Mashariki ambayo wameyasotea kwa muda mrefu.
Akizungumza mbele ya Wazee hao waliokuwa wamekusanyika mahakamani hapo kwa ajili ya kusikiliza hukumu yao, Wakili wao, Bw. Charless Sangarawe alisema kuwa maelezo ya hukumu hiyo bado hayajakamilika.

"Wazee wangu maelezo ya mwisho ya hukumu yenu bado hajamalizika, mpaka kesho (leo) saa tatu yatakuwa yamekamilika tunaomba mje kesho (leo)," salisema.

Wakizungumza mara baada ya kupewa maelezo hayo, Bibi Jamila Bakari alisema kuwa kuna mchezo mchafu ambao unafanyika ili kunyimwa haki yao ya msingi.

"Hapa watu wametoka mikoani kwa ajili ya kuja kusikiliza hatima ya mwisho wa mafao yetu ili waweze kuondoka, leo hii wanatuambia mpaka kesho na kesho napo tukifika watatupiga kalenda, kwa nini wanatunyanyasa na fedha ambazo si zao ni haki yetu," alisema.

Bi. Bakari alisema kuwa fedha hizo zilitolewa kwa nchi tatu Tanzania, Kenya na Uganda na Malkia Elizabeti wa Uingereza kwa ajili ya kupewa Waliokuwa wafanyakazi Afrika Mashariki, Uganda na Kenya wazee walikwishalipwa miaka mingi bila ya kusumbuliwa.

Alisema kuwa cha kusikitisha serikali ya Tanzania imekalia fedha hizo kama mali yao na kuacha kuwalipa wahusika na badala yake wanawazungusha kama wakimbizi.

Bi. Bakari alisema kuwa wamechoshwa na hali hiyo ni vema serikali ingetamka wazi kwamba fedha hizo hazipo ili ijulikane moja, kuliko kuwazungusha mara kwa mara na kusababisha vifo vya wazee wengine.

1 comment:

  1. Kwani ulipiga kura wewe? Kama ndiyo na ukapigia chama cha mafisadi basi jua haki ni jambo gumu sana. Sipendi unyimwe haki yako lakini kwa sababu ya kudanganywa na ccm na mkakubali kuwarudisha ikulu, vumilieni tu.

    ReplyDelete