28 November 2013

YANGA WATINGA NUSU FAINALI ‘UHAI CUP’ Na Fatuma Rashid
 Timu ya vijana chini ya miaka 20 ya Yanga B, imefanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali katika michuano ya Uhai Cup baada ya kuwafunga wenzao wa Ashanti mabao 2-1.

  Katika mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, timu zote zilianza mchezo kwa kushambuliana huku kila timu ikionesha nia ya kutafuta bao la ushindi ili kuweza kuingia hatua ya nusu fainali.
  Timu ya Yanga dakika 15 za mwanzo walikuwa wakilisakama lango la Ashanti lakini wachezaji wao hawakuwa makini kwani kila walipokuwa wakipata nafasi walishindwa kuzitumia.
  Dakika ya 32 Yanga walipata bao la kwanza kupitia kwa mshambuliaji wake Juma Ally, baada ya kupata pasi ndefu kutoka kwa Bakari Ally, ambapo aliwachambua mabeki wa Ashanti na kulenga mpira wavuni.
  Pamoja na bao hilo kwa Yanga, Ashanti hawakukata tamaa na badala yake nao walizidisha kasi dakika ya 42 mshambuliaji Haruna Rashid aliisawazishia timu yake ya Ashanti bao baada ya kupiga shuti kali lililomshinda kipa kudaka.
  Mp a k a t imu h i z o zinakwenda mapumziko zilifungana bao 1-1. Kipindi cha pili kilianza huku kila timu ikishambulia, dakika ya 47 na 48, Ashanti walijikuta wakipoteza nafasi za kufunga baada ya washambuliaji wao kupata nafasi nzuri za kufunga l a k i n i wa k a s h i n dwa kuzitumia.
  Dakika ya 75 Yanga walipata bao la pili baada ya mshambuliaji wao Bakari Ally kufunga kwa shuti kali baada ya kuwatoka mabeki wa Ashanti na kutumbukiza mpira wavuni.
Mpaka mpira unamalizika ni Yanga ambao walikuwa washindi na hivyo moja kwa moja kutinga hatua ya nusu fainali

No comments:

Post a Comment