Siku moja baada ya gazeti hili kuripoti habari za watoto wanadaiwa
kutekwa na kufichwa katika handaki lililopo kwenye msitu wa Mabwepande, Wilaya
ya Kinondoni, Dar es Salaam,
ambalo ndani yake kuna jengo kubwa lenye vyumba, Jeshi la Polisi limeanza uchunguzi
mkali, anaripoti Masau Bwire.
Chanzo chetu cha habari kimedokeza kuwa, uchunguzi huo unafanywa
na Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni kwa kushirikiana na Jeshi la
Polisi mkoani Pwani.
"Polisi wapo katika uchunguzi mkali tangu leo (jana),
asubuhi, si vyema kuzitoa taarifa mapema kabla uchunguzi haujakamilika,
tunaweza kuharibu upelelezi na wahusika kukimbia.
" Watoto wal i o j i o k o a w a m e p e l e k w a h o
s p i t a l i kuchunguzwa afya zao baada ya kuhojiwa na kutoa picha kamili ya
eneo lenye handaki, hivyo uchunguzi ukikamilika mtaambiwa," kilisema
chanzo hicho kwa sharti la kutotajwa jina lake.
Utekaji watoto wanaodaiwa kuwa zaidi ya 60 katika handaki hilo, unadaiwa kufanywa
na raia wa kigeni (Wazungu), wakishirikiana na Watanzania ambapo watoto hao
hufungiwa katika vyumba hivyo, kuteswa, kulawitiwa na kubakwa.
Watoto waliodai kutoroka kwenye handaki hilo
ni Emmanuel Robert (11) anayesoma darasa la tano Shule ya Msingi Maendeleo
iliyopo Tabata, Segerea, Dar es Salaam
na mdogo wake Godianus Robert (8), anayesoma darasa la tatu shuleni hapo.
Watoto hao walidai kutekwa na Wazungu wawili asubuhi ya Septemba 2
mwaka huu, wakati wakienda shuleni na kufanikiwa kutoroka katika jengo hilo Septemba 23 mwaka
huu.
Wakiwa wamechoka na afya zao kuzorota katika Kituo kidogo cha
Polisi, Kibaha Maili Moja, mkoani Pwani, watoto hao walisema ndani ya jengo hilo kuna watoto wengi wa
kike na kiume.
Wa l i s e m a w a t o t o h a o wanafanyishwa kazi na kuteswa kwa
kutandikwa fimbo, kuchomwa moto na kupigwa shoti ya umeme hasa wanapowaulizia
wazazi wao ambapo baadhi yao
hubakwa na kulawitiwa.
Akizungumza na Majira, Emmanuel alisema baada ya kutekwa
yeye na mdogo wake, walifungwa na vitambaa vyeusi usoni hadi walipofikishwa
ndani ya jumba hilo
la mateso.
Aliiomba Serikali kufanya jitihada za hali na mali ili kuwaokoa watoto wengine waliopo katika
jengo hilo.
Mama mzazi
wa watoto hao, Martha Godianus (29), ambaye anafanya shughuli za mama lishe,
njia panda ya Barakuda, Tabata Manispaa ya Ilala, alisema amehangaika zaidi ya
miezi mitatu kuwatafuta watoto hao bila mafanikio. Juzi Kamanda wa Polisi
mkoani Pwani, Ulrich Matei alikiri kupata taarifa za tukio hilo na kuanza kuzifanyia kazi
No comments:
Post a Comment