Na Mwandishi Wetu
Kocha
aliyeachana na timu ya Azam FC raia wa Uingereza, Stewart Hall amepata ulaji wa
kufundisha soka katika Academy mpya ya Symbion Power itakayoanzishwa hivi
karibuni.
Academy hiyo itaanzishwa nchini kwa ushirikiano wa Klabu ya
Sunderland AFC ya Uingereza na Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo.
Kabla ya kuanzishwa mradi huo, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni
na Michezo, Dkt. Fenella Mukangara alikwenda nchini Uingereza na kwenda katika
Klabu ya Sunderland akiwa na Rais Jakaya Kikwete kufikia makubaliano ya mradi
huo.
Akizungumza Dar es Salaam jana Mtendaji Mkuu wa Symbion Power
Tanzania, Peter Gathercole alisema Academy hiyo itakuwa na vituo eneo la
Kidongo Chekundu na Elite Football Academy, Dar es Salaam.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Sunderland, Margaret Byne alisema
mradi huo utasaidia kuinua soka la vijana, timu za taifa na klabu.
Alisema ili soka liweze kupiga hatua ni lazima lianzie kwa vijana
wadogo ambao wanatakiwa kufundishwa mbinu, maarifa na kujengewa uimara.
No comments:
Post a Comment