14 November 2013

PONDA ATINGA MAHAKAMA KUU
 Na Rachel Balama
   Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, inatarajia kufanyia mapitio ya uamuzi wa kutupilia mbali ombi la upande wa utetezi la kutaka kufutwa kwa shtaka la kutotii amri halali ya mahakama linalomkabili Shekhe Ponda Issa Ponda.

   Ombi hilo lilitupiliwa mbali na Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro, Richard Kabate. Mapitio hayo yanatarajiwa kufanyika Novemba 18, mwaka huu.
   Mawakili wa Ponda wakiongozwa na Juma Nassoro, waliiomba mahakama hiyo kupitia uamuzi huo uliotolewa Oktoba mosi, mwaka huu na hakimu huyo.
  Hakimu Kibate alitupilia mbali ombi la upande wa utetezi uliokuwa ukiomba mahakama hiyo kuondoa shtaka hilo la kutotii amri halali linalomkabili mteja wake au lifutwe akidai kuwa ilitolewa na Mahakama ya Kisutu.
  Wakili Nassoro alidai kwamba amewasilisha ombi hilo baada ya kubaini kuwa mahakama hiyo ya Morogoro haina uwezo kisheria kusikiliza shtaka hilo, vinginevyo lifunguliwe katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambayo ilitoa hukumu hiyo.
  Hata hivyo, Hakimu Kibate alitupilia mbali ombi hilo na kusema kuwa kwa mujibu wa vifungu mbalimbali vya sheria vya uendeshaji wa kesi za jinai, shtaka hilo dhidi ya Ponda la kudaiwa kutokutii amri halali ya mahakama litaendelea kusikilizwa katika mahakama hiyo na sio kuhamishiwa Kisutu.
  Alizitaja sababu za shtaka hilo kuendelea kusikilizwa katika mahakama hiyo kuwa ni mshtakiwa huyo kutenda kosa hilo eneo la Kiwanja cha Ndege la Manispaa ya Morogoro.
  Hakimu huyo alisisitiza kuwa hakuna sababu ya kuhamishiwa shtaka hilo katika Mahakama ya Kisutu.Sababu nyingine ni mshtakiwa huyo kuvunja amri halali iliyotolewa na Mahakama ya Kisutu na sio sharti kama ambavyo upande wa utetezi ulidai na kufafanua kuwa hata kama mahakama hiyo ilitoa sharti, kisheria sharti linalotolewa na mahakama yoyote ni amri.
   Sheekhe Ponda anakabiliwa na mashtaka matatu anayodaiwa kuyatenda kwenye mhadhara huo. Ilidaiwa mahakamani kwamba aliwaambia Waislamu wasikubali uundwaji wa kamati za ulinzi na usalama za misikiti kwani zimeundwa na ambao ni vibaraka wa CCM na serikal

1 comment: