14 November 2013

MBUNGE LEMA AMEVUNA ALICHOPANDA-UVCCM Na Darlin Said
  Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umekanusha vikali kauli iliyotolewa na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, kwa kuhusisha umoja huo na picha zinazomdhalilisha mbunge huyo kwenye mitandao ya kijamii.

  Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkuu wa Idara ya Hamasa na Chipukizi wa UVCCM Taifa, Paul Makonda, alisema UVCCM haihusiki na tukio hilo, hivyo alimtaka Lema atafute mchawi wake.
  Alisema watu waliofanya tukio hilo ni wale ambao amewatengeneza yeye mwenyewe katika mikutano yake ambao aliwahamasisha kutokuwa na nidhamu na kutotii sheria na taratibu za nchi."Sasa anamtafuta mchawi kwa kuishutumu UVCCM wakati hao waliofanya hivyo ndiyo matunda yake mwe n y ewe , " a l i s ema Makonda.
  Makonda alisema CHADEMA kila kinapopatwa na changamoto kinaishutumu CCM wakati hivi sasa ndani ya chama hicho hali sio shwari."Hivyo wasimtafute mchawi kwani bundi ameshatua,kazi ya UVCCM ni kuwatetea vijana, hatuna muda wa kumtafuta Lema," alisema Makonda.
  Makonda aliongezea kwa kusema kuwa Serikali imekuwa mstari wa mbele kusimamia amani,utulivu pamoja na watu kutii sheria na taratibu za nchi, lakini vyama vya upinzani vimekuwa vikitaka wananchi kutotii sheria.
  Alisema kilichomkuta Lema ni matunda yake mwenyewe, hivyo atambue hilo na si kuichafua UVCCM kama anavyodai.Lema juzi aliutuhumu uongozi na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Sadifa Juma Khamisi, kuwa alishiriki kumchafua kwa kusambaza picha katika mitandao ya kijamii zinazoonesha akidhalilishwa.
  Kutokana na tukio hilo, Lema alimtaka Spika wa Bunge, Anne Makinda achukue hatua kwa kuwa ushahidi wa jambo hilo upo hadharani.

8 comments:

 1. UVCCM,
  KWA MSIMAMO HUO UNAUNGANA NA UNACHODAI LEMA NA CHADEMA WANAFANYA. MUUNGWANA NA MTII WA SHERIA ANGELAANI KITENDO HICHO NA KIASI FULANI INAONYESHA UENDA MMEHUSIKA. TATIZO TULIOWAKABIDHI NCHI WAMEAMUA KUJISAHAU NA KUONA LEMA HANA HAKI YA KULINDWA. HISTORIA INASEMA NI DALILI ZA KUFIKIA A DECLINING STAGE.

  ReplyDelete
 2. Kama Lema amefanya mambo ambayo sio sawa, la kufanya si kutuma picha chafu za kumdhalilisha mtandaoni. Kwa UVCCM kusema kwamba Lema amevuna alichopanda, tunapata picha kwamba UVCCM wanajua watu waliofanya kitendo hicho Maneno ya UVCCM sio sawa kabisa..

  ReplyDelete
 3. LEMA Hawezi kuwa mtendewa na hakimu mwenyewe. mambo hayo yanaweza kufanywa na mtu yeyote mwenye nia mbaya. kutuhumu UVCCM ni kudhoofisha upelelezi. Toa taarifa polisi uanze uchunguzi.

  ReplyDelete
 4. MWENZIO AKIKUPIGA NGUMI NENDA MAHAKAMANI. UKIMRUDISHIA WW NDIE MWENYE KOSA UNATAKIWA UFIKISHWE MAHAKAMANI. POLISI SIO MAHAKAMA MNAWAPA UJIKO WA BURE KWA VILE NI CCM MPAKA WAMECHUKUA KAZI YA MAHAKAMA? HAO ANONYMI WANAZUNGUMZIA UUNGWANA WALA HAWAKUSEMA KUSHITAKIANA TATIZO LAKO VIROBA VYA CCM

  ReplyDelete
 5. Hili nalo la ajabu sana. Mwanasiasa maarufu saaaana! Umaarufu unaotokana na huruma ya jamii (social sympathy). Unazua skendi alafu unahurumiwaaa! Unasingizia wenzako, unahurumiwaaaa! Unapiga wenzako vitofali alafu unahurumiwaaaa!

  ReplyDelete
 6. ARE TALKING ABOUT SOCIAL OR POLITICAL SYMPATHY? LEARN HOW TO DIFFERENTIATE THINGS OTHERWISE YOU END UP MATONYA AWAITING DONATIONS FROM OTHERS

  ReplyDelete
  Replies
  1. Yes, kila toto tundu lina mbabe wake anayelilinda!

   Delete
  2. Rafiki yetu Mcharuko hako kachama ni kadogo sana, kametumia mbinu ya waganga wa kienyeji kujipatia umaarufu tu. Bado hakajapewa dola lakini ubabe kibao na migogoro kibao. Kumbuka waswahili husema "lakuvunda halina ubani" Hao kina Matonya ndio wananchi, ndio watanzania! JK ndie mkuu wao. Anatembeza bakuli wanakula! Usitafte mchawi. Tathmini tabia zenu na mitusi yenu na mibezo yenu!
   Mtaji wenu mitusi na kejeli kwa umma masikini unajitahidi kujikomboa!

   Delete