14 November 2013

KONTENA LA MENO YA TEMBO LANASWA Na Mwajuma Juma, Zanzibar
  Kontena lililobeba meno ya tembo limekamatwa katika bandari ya Malindi mjini Zanzibar ambalo lilikuwa linasubiri kusafirishwa jana.Kamishna wa Polisi Zanzibar, Musa Ally Musa, alithibitisha kukamatwa kwa kontena hilo jana lililokuwa na magunia 98 yaliyowekwa meno ya tembo tayari kwa kusafirishwa.

  "Ni kweli tumekamata kontena lililobeba meno ya tembo ila mpaka sasa bado hatujafahamu uzito na idadi ya meno yaliyokuwemo ndani ya magunia yaliyokuwa na idadi tofauti ya meno hayo kwani ukaguzi unaendelea," alisema Kamishna Musa Ally Musa.
  Kamishna Musa Ally Musa alisema hadi sasa wanawashikilia watu wawili kwa mahojiano ili kufahamu kama wanahusika na mzigo huo na wapi mzigo huo ulikuwa unapelekwa .Aliongezea kwa kusema taarifa kamili juu ya kontena hilo zitatolewa baada ya kupakuliwa na kufahamu uzito na idadi ya meno hayo.

1 comment:

  1. NI VEMA KATIBA MPYA IPITISHWE YENYE IBARA YA KUMPIGIA KURA YA KUTOKUWA NA IMANI NA MBUNGE AMBAYE ANATETEA MAASI INAPOFIKIA WABUNGE WANASIMAMISHA OPERESHENI ONDOA MAJANGILI ILI KUTOA FURSA KUUZWA NYARA ZA SERIKALI ZILIZOKO MKONONI HAIINGII AKILINI WABUNGE WALIONEKANA KUTETEA UJAMBAZI HUU INGEBIDI NGUVU YA UMMA IWAENGUE

    ReplyDelete