- SASA WAFIKIA TISA, WAKUTWA NA MAPANGA,SIMU YAKE
Rehema Maigala na Isaya
Ng wijo
Jeshi la Polisi nchini, linawashikilia
watuhumiwa tisa wanaosh ukiwa kumvamia, kumjeruhi na kuiba vitu mbalimbali vya
Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu yaC
hama cha
NCCR-Mageuzi, Dkt.Sengondo Mvungi.
Akizungumza na
waandishi wa habari Dar es Sa laam jana, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt.
Emmanuel Nchimbi,alis ema kukamatwa kwa watuhumiwa hao, kumechangiwa na
ushirikiano uliotolewa na familia ya Dkt. Mvungi.
Alisema watuhumiwa
hao wamekamatwa jijini Dar es Sa laam kwa nyakati tofauti ambapo awali walikamatwa
sita lakini majina yao
yalifichwa ili kutovuruga upelelezi.
Kamanda wa
Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova,ambaye alikuwepo
katika mkutano huo, waliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Msigwa Mpopela (30) ,Shabago
Magozi na Hamadi Ally, jina maarufu‘Hatibu’.
Wengine ni
Zakaria Raphael (dereva wa bodaboda), Mmanda Saluwa,Juma Hamisi,Longisho Semeriko(muuza
ugolo), Paul Jeirosina mwingine aliyemtaja kwa jina moja la Kilimimazoka,am bao
wote ni wakazi wa Dar es Salaam.
“Watuhumiwa hawa walikutwa
na mapanga, kigoda ambavyo vim ethibitika kuwa vilitumika katika tukio hilo, pia wa likutwa na simu ya m kononi mali ya Dkt.
Mvungi,”alisema.
Kamishna Kova alisema,
katika mahojiano ya awali na watuhumiwa, walikiri kuhusika na tukio hilo na ushahidi
umekamilika kwa asilimia 80.
“Watuhumiwa wote wamekiri
kosa hivyo tunakamilisha upelelezi ili wafi kishwe mahakamani mara moja,”alisema
.
Dkt. Mvungi alivamiwa,
kujeruhiwa na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi usiku wa kuamkia Novemba 3 mwaka
huu , nyumbani kwake Kibamba, Dar es Salaam.
Hivi sasa,Dkt. Mvungi
anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Milpark, nchini Afrika Kusini na
hali yake inaendelea kuimarika .
Akizungumzia suala la kuwakamata wahamiaji haramu, Dkt.Nchimbi
alisema mpango walionao ni kuweka Ofisa mmoja wa Polisi kila Tarafa nchini
aweze kusaidiana na Polisi Jamii pa moja na wananchi kuwabaini watu hao.
Ningependekeza kuwepo na road blocks pembezoni mwa mji zitakazokaliwa na jkt na polisi za kudumu.
ReplyDelete