- ACHAFULIWA MTANDAONI, AITUHUMU UVCCM TAIFA
Queen
Lema, Arusha na Mariam Mziwanda, Dar
Katika hali isiyo ya kawaida, Mbunge wa
Arusha Mjini, Bw. Godbless Lema, ameutuhumu uongozi wa Umoja wa Vijana wa Chama
Cha Mapinduzi (UVCCM), Taifa kwa mada ya kusambaza picha zinazoonesha
akiingiliwa kinyume na maumbile katika mitandao ya kijamii.
Mbali ya uongozi huo, Bw.
Lema pia alimtuhumu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Bw. Sadifa Juma Khamis, kwa
kushiriki kumchafua hivyo amemtaka Spika wa Bunge, Bi. Anne Makinda, achukue
hatua na kudai ushahidi wa jambo hilo
upo hadharani.
Bw. Lema aliyasema hayo
Mjini Arusha jana alipokutana na waandishi wa habari ili kuzungumzia jambo hilo na kusisitiza kuwa, suala hilo
limemsikitisha sana.
“Ushahidi wa namba za simu zilizohusika kusambaza picha hizo upo, Khamis
(Mwakilishi Jimbo la Donge, Zanzibar),
anahusika na udhalilishaji uliofanywa na vijana wa UVCCM Taifa,” alisema Bw.
Lema.
Alisema picha hizo
zimesambazwa katika mitandao ya kijamii na watumiaji wa simu za mkononi zikiwa
na ujumbe unaodai Lema akilawitiwa na wanaume wenzake.Aliongeza kuwa, Oktoba 29
mwaka huu, mkewe aliyemtaja kwa jina la Bi. Neema Lema, alipata picha hizo
zilizotumwa moja kwa moja katika simu yake zikiwa na ujumbe usemao “Hiyo ndiyo
kazi anayoifanya mume wako”.
Bw. Lema alisema, suala hilo halikuishia hapo kwani picha hizo
zilitumwa kwa mama mkwe wake na kusababisha familia ya mke wake na wazazi wake
kukosa amani “Mke wangu alitumiwa picha hizi katika mtandao wa WhatsApp na
baadaye ilisambazwa zaidi hadi kwa wapigakura wangu jimboni na kudai ndiyo kazi
inayofanywa na Mbunge wao,” alisema.
Aliongeza kuwa, uchafu huo
ulikuwa ukifanyika wakati akiwa bungeni Dodoma
ambapo Bw. Khamis, alionekana akisambaza picha hizo kutoka kwenye kompyuta yake
(mpakato), kuwapa wabunge jambo ambalo lilichangia amani ya bunge kuharibika
siku hiyo.
“Wakati picha hizi
zikisambazwa, nilijulishwa suala hili na wabunge wanawake wa CCM, ilibidi
niende kwa Spika ambaye alikiri picha hizo zimesababisha akose morali ya
kuendesha vikao. “Pia nilizungumza na uongozi wa Bunge nikilalamikia
kudhalilishwa kwa kutengenezewa picha zinazoonesha nikiingiliwa na wanaume
wenzangu... Spika aliahidi kulishughulikia,” alisema Bw. Lema.
Bw. Lema alisema, kutokana
na picha hizo, bado hazimnyimi kinga ya kuendelea kusema ukweli juu ya jambo
lolote badala yake ataendelea kupambana ili kuwatetea wanyonge.“Kamwe siwezi
kuwatafuta waliotengeneza picha hizi na kuzisambaza kwenye mitandao na simu za
watu bali atawasaidia viongozi wa UVCCM kuzisambaza kwenye Makanisa, Misikiti,
mikutano ya hadhara ili kuwaonesha wananchi ukatili dhidi yake unavyozidi
kushika kasi asiwe na sauti ndani ya nchi,” alisema.
Wakati huo huo, Mke wa Mbunge huyo, Bi. Neema, alisema
hicho ni kitu kidogo sana
dhidi ya mumewe na waliofanya vitendo hivyo walilenga kuvunja ndo yake lakini
haitatokea. Sadifa azungumza
Akijibu tuhuma hizo akiwa
njiani kwenda nchini Ethiopia,
Bw. Khamis alisema jumuiya hiyo au yeye mwenyewe hawezi kutumia cheo chake
kufanya vitendo hivyo.
“Mimi na Mheshimiwa Lema wote ni wabunge,
tofauti yetu ipo katika vyama na majimbo...tomefahamiana bungeni na wala simjui
kwa undani, tuhuma dhidi yangu si za kweli kwani siwezi kufanya kitendo hicho
ambacho si cha kibinadamu hata kama tuna
tofauti za kisiasa.
“Mimi ni Muislamu na dini
yangu hairuhusu kufanya hivyo, binafsi sijui kutumia kompyuta na Mheshimiwa
Lema analijua hilo...hivi
sasa Ofisi ya Bunge imeanza kutoa mafunzo kwa wabunge wasiojua kutumia
kompyuta, nami najifunza,” alisema.
Alisema simu anazomiliki
ni mbili, moja ni Nokia ya tochi na nyingine ya kichina yenye laini tatu na
hajui kama simu hizo zina mitandao na hajawahi
kujaribu.Bw. Khamis aliongeza kuwa, hulka yake hayupo karibu na makundi
yanayoweza kumuingiza au kumshawishi afanye vitendo hivyo hivyo yupo tayari
kukutana na Bw. Lema kwa amani ili wazungumze na kuwasaka waliofanya vitendo
hivyo ambavyo si vya kistaarabu.
“Mheshimiwa Lema akinitafuta nitampa ushirikiano, ninachokijua
mimi, mwenzangu ananitafutia umaarufu kwa sababu pamoja na vyeo nilivyonavyo bado
sifahamiki sana.
“Natumia cheo changu ndani
ya UVCCM kuijenga jumuiya na CCM... kwanza namuomba radhi kwa sababu tayari ana
imani potofu dhidi yangu, pili namshauri afanye utafiti,” alisema.
Alisema imani yake ni kwamba, tofauti zao kisiasa haziwezi kumshawishi
afanye vitendo hivyo kwani ipo siku Bw. Lema anaweza kurudi CCM na kufanya naye
kazi pamoja.
Aliongeza kuwa, umefika wakati wa Bw. Lema
kukumbuka kuwa, tofauti za kisiasa zilizopo ndani ya chama chao pia zinaweza
kutumika kumchafua katika mitandao
Yeye mwenyewe athibitishe kama ni uongo au la
ReplyDeleteMuoshwa huoshwa maumivu anayoyapata kwakusingiziwa ndivyo na wengine anaowatuhumu na kuwasingizia wanayapata busara itumike
DeleteWAKATI WENGINE WANAUMIZA VICHWA KUANGALIA MAENDELEO YA TAIFA YAKUWAJE,WAO NA MAJUNGU YA MTANDAONI.LEMA SONGA MBELE USIFE MOYO WAENDELEE KUPOTEZA MUDA WAO.SONGA MBELE KAMANDA.
ReplyDeleteMAELEZO HAYA YA BWANA KHAMIS YANAPINGANA NA TAARIFA YA UVCCM. MAALEZO HAYA ANGALAU YANA UUNGWANA NDANI YAKE LAKINI YALE YA UVCCM NI UUPUUZI MTUPU. KAMA HALI NDIYO YA KUCHAFUANA KIASI HICHO WA KULAUMIWA NI WANANCHI. TUMESHINDWA KUCHAGUA VIONGOZI
ReplyDeleteTanzania tunasema kuna amani, iko wapi hiyo amani kama m2 akitaka kukuchafua anakuchafua 2 awezavyo? siasa zinaliacha taifa la Tanzania kuwa MASIKINI.
ReplyDelete