Rais Jakaya Kikwete,
amerudisha zawadi ya dhahabu safi
gramu 227 aliyopewa na Kampuni ya Nyamigogo
Grand Vezir Holdings ya mkoani Geita na kutaka itumike kuwasaidia watoto yatima,
anaripoti Mwandishi Wetu
. Zawadi hiyo alikabidhiwa juzi katika sherehe ya uzinduzi
wa Mgodi wa Uchenjuaj iDhahabu wa kampuni hiyo uliopo nje kidogo ya Mji mdogo wa
Kharuma ambako ndiko Makao Makuu ya Wilaya Mpya ya Nyang’hwale,mkoani humo.
Dhahabu hiyo ina
thamani ya sh. milioni 16 kwa bei ya sasa katika soko la dhahabu duniani ambapo
baada ya kukabidhiwa, Rais Kikwete aliuliza; “Sasa nifanye nini na zawadi hii,
naomba kuirudisha hii dhahabu muiuze popote, fedha ambayo itapatikana tutawapa
watoto yatima,” alisema.
Akizungumza na wananchi katika mgodi huo, Rais Kikwete aliupongeza
uongozi wa mgodi na kusema umeongeza thamani ya dhahabu na ya maisha ya
wananchi katika eneo hilo.Aliushauri uongozi wa mgodi huo, kufanya jitihada za kuboresha
teknolojia inayotumika. “Mgodi huu ni mradi wa maana sana kwani umeongeza thamani ya dhahabu na
kuboresha maisha ya wananchi katika eneo hili, ubunifu huu unastahili pongezi.
“Lazima tuboreshe teknolojia, ile inayotumika katika mgodi huu ni
ya zamani kidogo, hii ni sawa na hadithi ya mtu mwenye chongo katika jamii ya
vipofu watupu, yeye anaonekana kama mfalme,”
alisema Rais Kikwete.
Mgodi wa Nyamigogo ni wa marudio kwa maana ya kuzalisha dhahabu
kutokana na mchanga ambao awali ulifukuliwa ili kutoa dhahabu na ulianzishwa
mwaka 2011 ambapo hadi sasa, sh. bilioni 1.6 zimewekezwa katika uendelezaji wa
mgodi huo.
Katika risala ya uongozi wa mgodi huo, ilisema mgodi huo
unazalisha kati ya gramu 500 na 600 kwa mwezi na umeajiri watu 45 wakiwemo
wanawake 10.Tangu kuanzishwa kwake, umekuwa unaunga mkono shughuli za jamii
inayouzunguka kwa kujenga zahanati na madarasa ya shule katika vijiji viwili.
Rais Kikwete amezindua mgodi huo kama
sehemu ya kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo akiwa katika ziara yake rasmi
ya kikazi mkoani humo ambao ni miongoni mwa mikoa minne aliyoianzisha mwaka
2012.
Ziara
hiyo imemalizika jana kwa kupokea ripoti ya maendeleo ya Wilaya ya Nyang’hwale
na kuhutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Mji Mdogo wa
Kharuma
Mimi sitashangaa iwapo vigogo wengine watakuwa wamepokea zawadi kama hii bila ya kutangaza.
ReplyDelete