- NI KWA KUTEKELEZA ILANI YA UCHAGUZI CCM
Na Mwandishi Wetu,
Monduli
Waziri Mkuu aliyejiuzulu na Mbunge wa
Monduli, mkoani Arusha, Bw. Edward Lowassa, ameisifu Serikali ya Awamu ya Nne
na kudai ndiyo iliyotekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),
kwa kiwango kikubwa sana
kuliko awamu nyingine zilizopita.
Bw. Lowassa aliyasema hayo jana wakati akihutubia mkutano
wa hadhara baada ya kuweka jike la msingi la ujenzi wa hospitali ya kisasa
wilayani humo na kusisitiza kuwa, ujenzi huo ni matokeo ya utekelezaji wa ilani
ya uchaguzi.
"Ndugu zangu wana
Monduli, huu ni uthibitisho wa utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya chama chenu,
lazima niseme wazi kuwa, hakuna kipindi ambacho ilani hii imetekelezwa kwa
kiwango kikubwa kama awamu hii chini ya Rais
Jakaya Kikwete," alisema.
Hospitali hiyo ambayo
majengo yake yatakamilika Februari 2014, ujenzi wake utagharimu zaidi ya sh.
bilioni mbili ikiwa na uwezo wa kulazwa wagonjwa 72 katika wodi nne.
"Nilipotoa ahadi ya
kujenga hospitali hii, nilizingatia ilani ya CCM hivyo chama chetu kinastahili
pongezi na Rais Kikwete kwa kusimamia kidete ilani yetu ya uchaguzi,"
alisema.
Bw. Lowassa aliongeza
kuwa, hospitali hiyo ikikamilika itakuwa na vifaa vya kisasa na kuifanya moja
ya hospitali bora nchini.
Alisema alimfuata Rais Kikwete na kumuomba fedha kwa ajili ya
mradi wa maji na kupewa sh. bilioni tatu ambazo ziko benki ambapo msaada huo
umelenga kutimiza ilani ya CCM.
"Ndiyo maana nasema
hakuna wamu ambayo imetekeleza ilani ya uchaguzi kwa asilimia kubwa kama awamu hii ya Rais Kikwete, pia Shirika la Nyumba la
Taifa (NHC), limeingia mkataba na Halmashauri ya Wilaya ya Monduli.
"Mkataba huu ni wa ujenzi wa nyumba
100 na kati ya hizo, 50 zitapangishwa na nyingine za kuuza," alisema.
No comments:
Post a Comment