28 November 2013

JELA MAISHA KWA KULAWITI MTOTO



 Na Prosper Mgimwa, Katavi
  Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi imemuhukumu, Leonald Wiliamu (19), mkazi wa Kijiji cha Mwese Namba Moja Wilaya ya Mpanda kifungo cha maisha jela kwa tuhuma ya kumlawiti mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka saba (jina tunalo).

  Hukumu hiyo ilitolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda, Chiganga Ntengwa, baada ya mahakama kutokuwa na mashaka na ushahidi uliotolewa mahakamani wa mashtaka.
Katika kesi hiyo ambayo ilikuwa na washtakiwa wawili mshtakiwa mwingine alikuwa na umri wa 17 ambaye alihukumiwa adhabu kuchapwa viboko vinne kutokana na kuwa na umri chini ya miaka 18.
  Washtakiwa hao walidaiwa kutenda kosa hilo la kumlawiti mtoto huyo Julai 31, mwaka huu saa mbili usiku nyumbani kwao. Watuhumiwa hao walikuwa wameajiriwa kufanya kazi ya kuchunga mifugo kwa baba mzazi wa mtoto huyo.
  Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Chiganga alisema baada ya kusikiliza mwenendo mzima wa kesi, mahakama iliwaona washtakiwa wanakabiliwa na kosa hilo la kulawiti.
  Washtakiwa kabla ya kusomewa hukumu walipewa nafasi ya kujitetea, ambapo waliiomba mahakama iwaachie huru kutokana kwa kile walichodai kuwa walisingiziwa kutenda kosa hilo na baba wa mtoto huyo kwa kuwa walikuwa wakimdai mshahara kwa muda mrefu.
  Akisoma hukumu hiyo, Ntengwa alisema Wiliamu anahukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti mtoto huyo na mwenzake, Yohane anachapwa viboko vinne

No comments:

Post a Comment