28 November 2013

MHARIRI GAZETI LA UHURU AFARIKINa Rose Itono

  Mhariri na Msanifu Mkuu Msaidizi wa gazeti la Uhuru, Dunia Mzobora, amefariki dunia usiku wa kuamkia jana katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kutokana na ugonjwa wa shinikizo la damu.


Akizungumza na Majira kwa njia ya simu jana, Mhariri Mtendaji wa gazeti la Uhuru, Josia Mufungo, alisema marehemu kabla ya mauti yake alikuwa kazini kama kawaida ambapo saa mbili usiku alimaliza kazi zake na kurejea nyumbani.

Alisema usiku wa saa sita walipata taarifa kutoka kwa familia yake kuwa Dunia amezidiwa na kukimbizwa haraka hospitali kwa ajili ya matibabu.

"Marehemu alikimbizwa Hospitali ya Agha Khan lakini walishindwa na kuamua kumpeleka Muhimbili kwa matibabu zaidi na saa 12 za asubuhi alifariki", alisema.

Mufungo alisema marehemu alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa shinikizo la damu kwa muda mrefu na kuongeza kuwa msiba wake utafanyika nyumbani kwake Tabata Kimanga, ambapo anatarajiwa kuzikwa leo saa 7.00 za mchana na shughuli zote za mazishi zitakuwa hapo hapo nyumbani kwake.

Alisema marehemu ameacha mjane na watoto watano. Alijiunga na gazeti la Uhuru mwaka 1989 kama mwandishi mwanafunzi ambapo baadaye alipanda hadi kufikia nafasi aliyokuwepo

No comments:

Post a Comment