12 November 2013

CHADEMA: HATUHUSIKI MADAI YA ZITTO

 Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema Ofisi ya Katibu Mkuu wa chama hicho imepokea barua iliyoandikwa na Naibu Katibu Mkuu, Bw. Zitto Kabwe, anaripoti Rose Itono.

Barua hiyo, inamtaka Katibu Mkuu wa chama hicho, Dkt
 Wilbrod Slaa athibitishe madai ya ripoti inayosema“Taarifa ya Siri ya CHADEMA”iliyosamba zwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii.
Taarifa hiyo inadai kuchunguza mwenendo wa Bw.Kabwe tangu mwaka2008-2010 na kubaini amepokea fedha kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuivuruga CHADEMA.
Akizungumza na Majira jana, Ofisa Habari wa CHADE MA,Tumaini Makene,alisema barua aliyoiandika Bw. Ka bwe itafanyiwa kazi kwa mujibu wa taratibu, kanuni za katiba ya chama.
“Chama chetu kinaongozwa na vikao hivyo barua yake itafanyiwa kazi...CHADEMA haiendeshwi na taarifa za magazetini au mitandaoni,”alisema Bw. Makene.
Aliongeza kuwa,si mara ya kwanza makundi yasiyojulikana kusambaza taarifa za kutaka kumchafua Bw. Kabwe kupitia mitandao hiyo ambapo Ofisi ya Habari,ilishughulikia suala hilo na kuhakikisha taarifa hizo zinaondolewa .
“Hivi sasa ni mara ya pili, Bw. Kabwe anali fahamu hilo hivyo CHADEMA hakihusiki, lakini kitashughulikia s uala hili kupitia vikao ili kupata majibu sahihi,” alisisitiza Bw.Makene.
Katika taarifa yake aliyoitoa juzi kwa vyombo vya habari, Bw.Kabwe alisema taarifa hizo zimesambazwa katika mitandao ya kijamii hivyo alimtaka Dkt.Slaa, athibitishe ki nachoitwa“Taarifa ya Siri ya CHADEMA”,kama ni taa rifa ya chama au kuikanusha ili kumpa fursa ya kuchukua hatua za kisheria dhidi ya waandishi wa taarifa hiyo.
Hata hivyo, Bw. Kabwe ambaye pia ni Mbunge wa Kig oma Kaskazini,aliziita taarifa hizo za kutunga zilizojaa uongo wa kiwango cha kutisha hali ambayo imemfedhehesha, kumsikitisha na kumkasirisha.
Alisema taarifa hizo ziliibuliwa katika kipindi ambach o alikuwa safarini kutetea haki zaWatanzania na Afrika amb ao utajiri wao wa rasilimali unafaidiwa na watu wachache waliohifadhi fedha katika akaunti nje ya nchi.

4 comments:

  1. Mbona kuna mambo mengi ya chadema mitandaoni. Ama hili tu ndilo hamtaki lionekane.

    Vikao gani visivyo na demokrasia!

    ReplyDelete
  2. Ww demokrasia kwako ina maana hata mambo ya ofisini? Mbinu hizi hizi tuliziona wakati wa NCCR na CUF kwa hiyo sisi hatuoni ni jipya. Hata jiwe tutalipa kura zetu. Tumechoka kudharauliwa na kuuwawa.

    ReplyDelete
  3. Ndugu zangu watz hizi habara tuzipuuze kabisa kabisa, kwan lazima tuweze kutambua vyema kwamba maadui wa demokrasia nchi hii ni wengi sana sana, na pia c mara ya kwanza kusikia watu wametishiwa na hata kuamua kubadili maamuz yao, tusikubal kwa wepesi sana mambo yanayozungumzwa hasa kwenye mitandao ya kijamii.

    Cha msingi cha kufanya ni kusonga mbele na tusikubal jambo lolote lile lenye lengo la kuturudisha nyuma litusumbue vichwa vyetu

    Mi nasisitiza Tz ni yetu wote na kila mtu ana uhuru wa kuafanya jambo jema kwa manufaa ya watz wote bila kuvunj sheria

    ReplyDelete
  4. Demokrasia ikitawala mamangimeza wanaofaidi keki ya taifa pekee yao watakuwa hawana lao ndo maana unaona wanajaribu kila mbinu kufifisha juhudi za watanzania kupata uhuru na haki ya kweli Peoples Power

    ReplyDelete