09 October 2013

...YAMUOMBA RADHI AMIS TAMBWE

Na Fatuma Rashid
  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limemuomba radhi mshambuliaji wa Simba, Amis Tambwe aliyenyimwa mpira na mwamuzi aliyechezesha mechi ya Ligi Kuu kati ya timu yake dhidi ya Mgambo Shooting, baada ya kupachika mabao manne.
  TFF imesema kutokana na hatua hiyo ambapo katika mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Simba ilishinda mabao 6-0, mwamuzi huyo hataadhibiwa.

  Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura alisema kitendo cha mchezaji kupewa mpira pale anapofunga mabao kuanzia matatu katika mechi moja halipo kwenye sheria ya ilani imani ya haki katika mpira wa miguu 'fair play'.
  Wambura alisema walimuita, Tambwe wakamuomba msamaha ambapo muda wowote kuanzia sasa anajipanga, ili kuuchukua mpira wake. Katika mechi hiyo mabao mawili yalifungwa na Haruna Chanongo hivyo kufanya idadi ya mabao kuwa 6-0

No comments:

Post a Comment