01 October 2013

WAZEE YANGA: TUNATAMBULIKA KIKATIBANa Neema Ndugulile
   Baraza la Wazee wa Yanga, wameendelea kuvutana na uongozi wa klabu hiyo kwamba wao wanatambulika kikatiba tofauti na viongozi hao kuwapinga.Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Katibu wa baraza hilo, Ibrahim Akilimali alisema hakuna shina lisilokuwa na mzizi na wao kama wazee ni mzizi wa timu ya Yanga.

Akilimali alisema kwa sasa Yanga ndiyo imeanza Ligi Kuu upya na wao kama mzizi wa klabu hiyo, watahakikisha timu yao inaendelea kusonga mbele. 
"Sisi kama wazee wa Klabu ya Yanga, tumesimama kuhakikisha tunasonga mbele bila kusuasua, sisi ndio mizizi wa klabu na hakuna shina lisilokuwa na mizizi na hata kama tukiondoka sisi watakuja wazee wengine," alisema. Aliongeza kuwa wao kama wazee, hawajajitenga na hawawezi kujitenga kwani wana umuhimu mkubwa katika kutoa ushauri, ili kuikuza klabu hiyo

No comments:

Post a Comment