01 October 2013

REDD'S MISS TANZANIA ATEMBELEA RASMI TBLNa Ibrahim Mussa
   Redd’s Miss Tanzania, Happiness Watimanywa jana alitembelea rasmi Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), ambao ni wadhamini wa Mashindano hayo, ambapo alikutana na uongozi wa juu ili kujitambulisha.
   Katika ziara hiyo, Happiness alifuatana na mshindi wa pili, Latifa Mohammed, mshindi wa tatu, Clara Bayo pamoja na Kamati ya Redd's Miss Tanzania.

   Akizungumza mara baada ya kukutana na mrembo huyo, Mkurugenzi Mkuu wa TBL, Robin Goestache alisema, wao kama wadhamini wakuu wanajisifu kuwa sehemu ya mafanikio ya Redd's Miss Tanzania, huku akimsifu mrembo huyo kwa ushindi wake.
  "Kila mmoja kati yetu anajua shindano lilivyokuwa gumu, warembo wote walikuwa na sifa na ninawapongeza ninyi mlioshinda na tunawakaribisha katika familia ya TBL," alisema.
   Mkurugenzi wa Masoko wa TBL, Kushillah Thomas, naye alitumia fursa hiyo kuwapongeza warembo hao na kusema ana imani kubwa nao; watafanya vizuri zaidi katika kipindi chao, kwa upande wake Meneja Masoko wa TBL, Fimbo Butallah alisema, tangu waanze kudhamini shindano hilo wamepata mafanikio makubwa mno, huku kukiwa na kazi nyingi za jamii wanazozifanya na warembo waliofanikiwa kutwaa taji hilo.
  Happiness naye aliishukuru TBL kwa kudhamini shindano hilo na kusema anajivunia kwa kiasi kikubwa kuwa sehemu ya familia ya Redd's. "Kwa kiasi kikubwa nawashukuru kutokana na kudhamini shindano hili kwa muda wa miaka 13, kwani mmewasaidia mengi warembo; na najivunia kuvaa sura ya Redd's," alisema.

No comments:

Post a Comment