02 October 2013

MWANANCHI,MTANZANIA WAONYWA

Assah Mwambene


 Na Mwandishi Wetu

    Siku chache baada ya Serikali kuyafungia magazeti ya Mtanzania na Mwananchi yaliyokuwa yakitoka kila siku, jana imetoa tamko lingine kwa uongozi wa kampuni hizo.Msemaji wa Serikali ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Bw. Assah Mwambene, ameitaka Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), kuacha mara moja kuchapisha gazeti hilo katika mtandao.


    Alisema Serikali imelifungia gazeti hilo kwa kipindi cha wiki mbili kuanzia Septemba 27, mwaka huu, lakini limeendelea kuchapishwa kwenye mtandao wa intaneti kinyume cha amri iliyotolewa."Kufanya hivyo ni kosa,...Serikali tumewaandikia barua ya kuwataka waache kufanya hivyo mara moja, Serikali italazimika kuchukua hatua kali zaidi kama amri hii itapuuzwa," alisema.

   Bw. Mwambene pia aliitaka Kampuni ya New Habari 2006, ambayo inamiliki gazeti la Mtanzania ambalo limefungiwa kwa kipindi cha miezi mitatu, kuacha kuchapisha gazeti la Rai kila siku ambalo awali lilikuwa likitoka kwa wiki.

   Alisema Gazeti la Mtanzania lilifungiwa Septemba 27 mwaka huu, ambapo hivi sasa kampuni hiyo inachapisha Gazeti la Rai kila siku badala ya wiki bila kibali cha Msajili wa Magazeti."Hilo nalo ni kosa, Serikali inawataka kuacha mara moja kuchapisha gazeti hilo kila siku na warudie ratiba yao ya kuchapisha mara moja kwa wiki hadi maamuzi mengine yatakapofanyika," alisema.

   Aliongeza kuwa, Serikali imeyafungia magazeti hayo kwa kuzingatia Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976 na kanuni zake za mwaka 1977 hivyo hawakukurupuka kuchukua uamuzi huo.Alisema uamuzi huo ulitolewa baada ya kufuata taratibu zote za msingi pamoja na kuwasikiliza wahusika

No comments:

Post a Comment