04 October 2013

CRDB YAIBUKA MWAJIRI BORA   Benki ya CRDB imeibuka mshindi wa jumla kutoka miongoni mwa waajiri nchini wanaowasilisha michango ya wafanyakazi wake kwa wakati katika Mfuko wa Pensheni wa PPF, anaripoti Reuben Kagaruki.

  Kutokana na ushindi huo, benki hiyo ilitunukiwa tuzo na Waziri wa Fedha, Dkt. William Mgimwa, wakati wa ufungunzi wa mkutano wa 23 wa mwaka wa wanachama na wadau wa PPF uliofanyika mjini Arusha.
Mshindi wa pili miongoni mwa waajiri wanaowasilisha michango ya wafanyakazi kwa wakati ni Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA). Washindi wengine waliozawadiwa zawadi hizo kulingana na makundi yao ni Bodi ya Sukari Tanzania (Mshindi wa Kwanza) na Bodi ya Kahawa Tanzania (2) kwa upande wa sekta ya Kilimo.
Kwa upande wa sekta ya madini mshindi wa kwanza alikuwa ni Barrick Bulyanhulu na kufuatiwa na mgodi wa madini wa Geita, huku upande wa sekta ya usafirishaji na umeme mwajiri aliyeongoza kwa kulipa michango ya wanachama kwa wakati EWURA ikifuatiwa na Kampuni ya Simu ya Airtel Tanzania.
Upande wa waajiri wa sekta ya fedha, Benki ya CRDB iliibuka kinara ilifuatiwa na Benki ya NMB wakati kwa upande wa waajiri wa sekta ya elimu na mafunzo mshindi ni Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Bugando.             Mshindi wa upande wa sekta ya afya alikuwa Research Triangle Institute na HJF Medical Research International, upande wa ujenzi mshindi ni Bodi ya Usajili wa Makandarasi na Kampuni ya Ujenzi ya Konoike, huku upande wa viwanda na biashara mshindi wa kwanza akiwa Kampuni ya Sigara Tanzania (TCC) na Kampuni ya Saruji Mbeya.
  Waajiri walioibuka washindi kwa upande wa vyombo vya habari ni wachapishaji wa magazeti ya serikali (TSN) akifuatiwa na Multichoice Ltd, wengine wakiwa Puma Energy Tanzania Ltd na HakiElimu huku mwajiri wa kujitegemea aliyeibuka mshindi akiwa ni Dkt. Shukuru Kawambwa

No comments:

Post a Comment