Na Elizabeth Mayemba
VIONGOZI wa Matawi ya Yanga Mkoa wa Dar es Salaam wamemshtaki Mwenyekiti wa Kamati ya Ligi
Kuu, Wales Kalia kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),
Leodegar Tenga kwa madai ya kuitishia klabu hiyo ambayo inapanga kuandamana.
Katika barua yao iliyowasilishwa jana
TFF wanachama hao, wamemtaka Kalia ajiuzulu nyadhifa zake zote ndani ya TFF kwa
kuwa ameshindwa kusimamia mpira.Barua hiyo
iliyosainiwa na Katibu wao Supa Nyamu, inadai kusikitishwa na kitendo cha
kiongozi huyo wa Kamati ya Ligi kupandikiza chuki katika klabu yao kupitia katika kituo kimoja cha redio
nchini kwamba atapambana na wanaotaka kuandamana Yanga.
Barua hiyo
inaeleza kuwa maneno aliyoyasema Kalia, yanaonesha wazi kuwa si kiongozi kwani
anapandikiza chuki binafsi na kuegemea upande mwingine wakati yeye hapaswi
kuegemea upande wowote.
“Sisi wanachama
na wapenzi wa Yanga wakati timu yetu inahujumiwa yeye anashabikia vitendo viovu
vya uvunjifu wa amani inavyofanyiwa klabu yetu ya Yanga.“Kalia kwa
matamshi yake aliyotoa katika redio ni kuwadhalilisha wana Yanga wote vitendo
vinavyofanywa na waamuzi wanaochezesha Ligi Kuu ni ukiukwaji wa sheria 17 za
mpira wa miguu,” ilisomeka sehemu hiyo ya barua.
Barua hiyo ilieleza kuwa kwa kauli za kiongozi
huyo anaidhalilisha Yanga na kuihujumu, hivyo anapaswa kujiuzulu nafasi zake
zote zinazompa mamlaka TFF na kuomba vyombo husika, vimchukulie hatua ya
kuondolewa kwenye mchakato wa Uchaguzi Mkuu kwa kuwa naye ni mgombea
No comments:
Post a Comment