25 September 2013

YANGA SASA WAOMBA DUA ZA MASHABIKI    Na Andrew Ignas na Mosi Mrisho
Wachezaji wa mabingwa watetezi Ligi ya Vodacom,Ya n g a wameomba kuombewa dua ili washinde katika mechi zao za ligi hiyo badala ya kuwashutumu.

   Akizugumza mara baada ya kumalizika mazoezi jana yanayofanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Loyola iliyopo Mabibo, Dar es Salaam nahodha wa timu hiyo, Nadir Haroub‘Canavaro’ alisema mashabiki wanatakiwa kuiombea timu hiyo,ili waweze kufanya vizuri kwenye mechi zijazo.
 “Waandishi kwa kweli Yanga tunacheza vizuri mno tofauti na msimu uliopita, ila bado hatuna bahati hivyo tunahitaji dua za mashabiki na wanachama wetu ili tufanye vyema,” alisema Canavaro.
   Wakati huo huo, nahodha huyo amewaomba wachezaji wenzake kuhakikisha wanatumia kipindi hiki kujinoa na kulipa kisasi kwa timu watakazocheza nazo kutokana na matokeo mabaya waliyoyapa katika mechi zilizopita.
  “Mvua, jua, majonzi na machungu tunatakiwa kuyaonesha katika mechi zote zinazokuja ikiwemo mchezo wa Jumamosi dhidi ya Ruvu Shooting,” alisema. Hata hivyo ametamba kwamba kikosi chake kitahakikisha kinarudisha furaha ya ushindi,ambayo imetoweka kupitia mchezo wao wa Jumamosi.

No comments:

Post a Comment